Sijaelewa kauli ya AU dhidi ya serikali ya mpito Guinea

Bodaboda zilianza kitambo.

2922241_FB_IMG_16312777203767222.jpg
 
siku nyingine hao wanajeshi mashujaa wakifanikiwa kumchoa kiongizi mbovu wawe wanamchuna ngozi ya mboo kisha wanamwambia arudi kwake. liwe fundisho kwa wengine, ***** zao
Haa haaa Na akiwa kama huyu wa kwetu wamchune nini mkuu😄😄
 
Viongozi wa Africa wote Ni walewale, haya mambo ya ukiukwaji wa haki za Binadamu, ukandamizwaji wa Demokrasia huku watawala wakiwa Ni miungu watu yapo Africa tu ndo maana wanateteana kwa mgongo wa AU, wanahisi linaweza kuwapata kwenye nchi zao!

Bila shaka hata hapa tz watawala walishtushwa mno na hawawezi kuunga mkono maana wanajua kitaumana mda wowote!

So, AU ni wa kupuuza TU, maadam wenye nchi yao Wanayo furaha kwa kupata Uhuru Tena, hata AU wangesema nin Hamna madhara!

AU inalea Sana ukiukwaji na ukandamizwaji wa Demokrasia Africa, na c vinginevyo!

 
Viongozi wa Afrika kupitia AU wametoa kauli ya kutoitambua serikali ya mpito Guinea. Mimi binafsi siwaelewi .....waliofanya mapinduzi Ni watu wa Guinea waliokuwa wanapewa amri kuua na kuwasweka ndani wapinzani wa utawala uliopita. Moja ya sababu kubwa wanayotoa pia Ni nchi kuelemewa na tozo na ukiukwaji wa haki dhidi ya raia wema. Pamoja na njia iliyotumika haikuwa njema lakini angalau wananchi wamepumua na kushangilia Sana mapinduzi.

Swali kubwa hapa Ni umoja huu kukaa kimya kwa matendo na dhuluma dhidi ya demokrasia. Chaguzi nyingi ndani ya Afrika haziko huru na nyingi zimekuwa zikibugikwa na uporaji wa matokeo. Na vyama tawala kubaki madarakani kwa nguvu ya jeshi na polisi. Hakuna chaguzi huru kwa nchi nyingi. Sasa Hawa ndio wasemaji na waliouona mapinduzi ya juzi kukiuka misingi ya haki dhidi ya demokrasia. Viongozi wengine ndani ya umoja huo Kama kina Kagame na Museveni Ni matunda ya mapinduzi. Eti leo hii nao wanalaani vikali Hali iliyotokea Guinea.

Kitendo Cha jeshi kupindua na nchi kutulia Ina fundisho Fulani juu ya serikali iliyopinduliwa.
1. Ni kuwa hiyo serikali ilikanyagia demokrasia na hivyo ilibidi iondolewe tu na hao wanaoipa Kinga kudumu madarakani.

2. Waliopindua walipima with no doubt, kuwa wasipofanya Jambo kuiondoa serikali madarakani, raia wengi wataumia. Mfano kuuliwa, kufungwa na kuumizwa .

Unapokuwa na serikali isiyojali matakwa ya demokrasia na kuibadilisha katiba ili iipendelee unategemea nini, je, wananchi waendelee kuteseka au hiyo serikali ipishe? Na, Kama Ni kupisha njia iliyo sahihi Ni ipi....jeshi kuendelea kuwabana raia kwa kuendelea kuwakingia kifua wale wanaowatesa raia au kuungana na raia kukiondoa serikali dhalimu inayowatesa raia?

Kitu sahihi kwa umoja wa Afrika ni kuwa na jicho la kidemokrasia...kwa sababu wengi wanakandamiza demokrasia hakuna wanaosikiliza upande unaonyanyaswa kwa sharti tu nchi isiingiliwe Mambo yake ya ndani halafu wakati huo nchi za nje mfano Uingereza na Marekani wakiingilia masuala ya ndani ya Afrika viongozi hao hukaa kimya utadhani AU hawako.

Kwa tukio la Guinea Tuanze kujifunza kuheshimu demokrasia na kuwatendea wananchi wetu Yale wanayopaswa kutendewa kwa mujibu wa katiba. Kujiongezea madaraka kutumia idadi ya watu ulionao katika medani za utungaji Sheria Ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

View attachment 1932761
AU ni genge la Walafi wa Maslahi. Sijawahi kuwasikia wakikemia Viongozi wanaokiuka haki za msingi za Raia.

Ila wakipinduliwa ndio wa kwanza kulaani na kuto tambua..

Nadhani ni sawa tu kutowatambua hao wafanya mapinduzi sababu lengo leo ni kuwapa Raia kile wanahitaji...wakati hao wa AU ni kuwakandamiza tu Raia...nadhani ni sawa kuto watambua sababu wamejitoa ktk genge lenu.....

Na huko ndiko tunaelekea kwa Nchi nyingine za Africa zenye ukandamizaji wa kutisha wa haki za Raia kwa mgongo wa Amani na Utulivu.
 
Back
Top Bottom