PANTHERA LEO
JF-Expert Member
- Jan 25, 2019
- 2,307
- 3,431
Leo asubuhi mida ya saa 12 wakati bado nipo kitandani muda huo nataka niamke lakini bado nipo ndani ya blanketi na nje mvua inanyesha kimenitokea kitu cha ajabu sana
Nakumbuka nilikuwa nawaza tu mambo ya kawaida kuhusu maisha yangu.. Ghafla nikasikia kama mtu anatembea nje ya nyumba, niliendelea kusikiliza kwa makini nikahisi kama geti linafunguliwa.. Basi nikaamua niamke nikaangalie
Kitu cha kunistaajibisha sikuweza kuamka.. Mwili wote ulikuwa umekakamaa na hakuna kiungo kilichokuwa kinafanya kazi, nilikuwa nimelala kiubavu na miguu nimekunja ( kama herufi Z)
nilijaribu kunyoosha miguu lakini wapi kiungo pekee kilikuwa kinafanya kazi ni macho.. Hata kusikia nilikuwa sisikii chochote tena...
Niliona kama mlango unasogea.. Lakini sina uhakika (nilihisi kama kuna mtu anachungulia mlangoni) lakini sioni kitu.. Naona kivuli kwa mbali sana
Hali hii ilidumu kama dakika tatu.. Ghafla nikaanza kujisikia kawaida, hali ya uwoga ikaniondoka, Mwili ukarudi kawaida na nikaenda nje nikakuta hamna chochote (mvua inanyesha)
Mwisho
Wakuu naomba kujua hii hali inasababishwa na nini maana tukio hili halinitoki kichwani?