Siioni imani ya CCM kushinda uchaguzi mkuu 2025

Kila nikitazama maisha yanavyozidi kua magumu, watu wanavyolia na ugumu wa maisha na hali inazidi kua mbaya kuliko siku za nyuma, siioni imani ya CCM kushinda uchaguzi 2025. Ugumu wa maisha hua ni sababu tosha kukiondoshea mapema chama ukombozi.

Mtapiga watu, wagombea kupitia vyama vya upinzani watapitia mateso makali sana, wataumia sana lakini mwisho wa siku ndogo ndio wakaoongoza taifa kwa msaada wa wananchi waliochoka. Polisi wanaweza kupiga na kuumiza watu lakini hawawezi kulifanya hilo nchi nzima.

Kazi kubwa iliyopo kwa wapinzani na wanaharakati wengine ni kuondoa makada wa CCM kule NEC na wakurugenzi kutosimamia Uchaguzi. Na hilo ni lazima kwa namna yeyote ile haliwezi kuachiwa, hii ni nchi yetu sote.
Hapo meza inabidi ipinduliwe
 
Na hao watu lazima wapate mtu wa kuwaongoza, au unataka nchi iwe kama Sudan or Congo? Kila mtu afanye vile anataka yeye? Upinzani wetu umeonesha udhaifu sana since 2015, hawafai kupewa nchi
Huo Ni mtazamo wako ndugu....mtu yeyote au chama chochote chaweza pewa nchi ili mradi tu wenye nchi wakiamua
 
Ccm kiushawishi ilishakufa kitambo sana inabebwa na silo katibu mwenezi wa chama.ccm haiwezi bila silo katibu mwenezi
 
Sema ,wapinzani hawajajipanga vizuri.Mbona Zambia wapinzani wameshinda kwa katiba mbovu?Huku kwetu ,hatuna wapinzani tishio.Uchaguzi ukifika,lowassa njoo ugombee.Uchaguzi ukifika Lissu acha kuosha vyombo vya wazungu ,njoo ugombee.Kuna kushinda hapo?
Nafikiri sio kujipanga hata ujipange vipi hapa hutoboi hata angefufuka Magufuri leo awe mgombea wa upinzani hataishinda CCM huo ndio ukweli, majeshi yanasambaza kura fake na kukimbia na kura unategemea nini? Sikubaliani na kujipanga. Wapinzani walikurupuka kuanzisha vyama bila kuiangalia katiba, na tume huru ya uchaguzi wameula wa chuya. Wanalia lia tumeshika mpini. CCM hoyee.
 
Magufuli mwenyewe alishindwa uchaguzi wa 2015 na Lowassa, akashindwa tena 2020 na Tundu Lissu hadi akazima mitandao wiki nzima. Huyu mama ndo hawezi kabisa, yan atapata 20%. Kifupi CCM Hakuna mtu anaichagua...ni mabavu tu. Ila 2025 ndio itakuwa aibu ya karne
 
Hakipo Chama cha upinzani cha kuchukua nchi. CCM ipo sana madarakani. Kwa sababu nyingi tu:
1. Huwezi kutaka kuongoza dola halafu kuanzia viongozi hadi wanachama kazi ni kutakana vyombo vya dola na viongozi wake.

2. Huwezi kutaka kuongoza dola kazi ni kuchonganisha vyombo vya dola na wananchi.

3. Huwezi kutaka kuongoza dola halafu unadharau na kubeza historia ya Uhuru wa nchi yako, mnatukana waasisi (Rejea uwendawazimu wa Lissu kwa Mwalimu na Mzee Karume).

4. Huwezi kutaka kuongoza dola halafu huna ajenda zinazoeleweka zaidi ya kukurupuka tu mara hivi mara vile.

5. Hamna ajenda za wakulima. CCM inapita mikoani kusimamia ajenda za wakulima ambao ni asilimia zaidi ya 70.

Nchi hii kama huna sera zinazoeleweka ktk kilimo hufai. Kwa sababu utakuwa unatengeneza umasikini wa kurithi (generational poverty), kwani kizazi cha wakulima masikini kitaendelea kuzaa masikini na mnyororo kukua. Wapinzani hawana Dira ya kilimo. Wengi ni wenye kufikiria madini, gesi na vitalu vya utalii ili Walete tu mabepari mamboleo.

6. Huwezi kutaka kuongoza dola ktk dunia ya sasa kama huna sera ya gender equality. Suala la usawa wa kijinsia ni global agenda. Wapinzani wako primitive era. Wao ni mfumo dume tu.

CCM ina Dira na yote. Hakuna wa kumzuia Rais Samia 2025. Tumuunge mkono.
 
Tuaminike mara 2? Ndio maana tunataka tume huru ya uchaguzi kisha uje ulete mrejesho. Huku kupora uchaguzi ni kwa kuwa ukweli ulioko kwenye box la kura ni kinyume kabisa na matamanio ya ccm
ama mnaweza kuaminika kwa sasa sababu ya tabia mlizoonesha since 2015

Nyerere ni nani? Kama kweli upinzani wa kweli utatoka ccm tusingeona huu wizi wa kura wa sasa.
But viongozi wote wa Upinzani wa Kenya kwa sasa walikuwa ni makada waandamizi wa KANU, tunarudi kule kule kwa Nyerere, Upinzani wa kweli utatoka CCM
 
Washauri ccm wavunjike uone kama watapata uungwaji mkono wa watu.
viWqongozi wote wa Upinzani wa Kenya kwa sasa walikuwa ni makada waandamizi wa KANU, tunarudi kule kule kwa Nyerere, Upinzani wa kweli utatoka CCM
 
Huu uchafu ulioandika hapa kama CCM inakubalika tusingeona mabegi ya kura za wizi ili ccm watangazwe washindi kwa shuruti. Kama CCM ingekuwa inajali wakulima, basi wakulima wasingekuwa wanaoongoza kwa umasikini nchi hii.
Hakipo Chama cha upinzani cha kuchukua nchi. CCM ipo sana madarakani. Kwa sababu nyingi tu:
1. Huwezi kutaka kuongoza dola halafu kuanzia viongozi hadi wanachama kazi ni kutakana vyombo vya dola na viongozi wake.

2. Huwezi kutaka kuongoza dola kazi ni kuchonganisha vyombo vya dola na wananchi.

3. Huwezi kutaka kuongoza dola halafu unadharau na kubeza historia ya Uhuru wa nchi yako, mnatukana waasisi (Rejea uwendawazimu wa Lissu kwa Mwalimu na Mzee Karume).

4. Huwezi kutaka kuongoza dola halafu huna ajenda zinazoeleweka zaidi ya kukurupuka tu mara hivi mara vile.

5. Hamna ajenda za wakulima. CCM inapita mikoani kusimamia ajenda za wakulima ambao ni asilimia zaidi ya 70.

Nchi hii kama huna sera zinazoeleweka ktk kilimo hufai. Kwa sababu utakuwa unatengeneza umasikini wa kurithi (generational poverty), kwani kizazi cha wakulima masikini kitaendelea kuzaa masikini na mnyororo kukua. Wapinzani hawana Dira ya kilimo. Wengi ni wenye kufikiria madini, gesi na vitalu vya utalii ili Walete tu mabepari mamboleo.

6. Huwezi kutaka kuongoza dola ktk dunia ya sasa kama huna sera ya gender equality. Suala la usawa wa kijinsia ni global agenda. Wapinzani wako primitive era. Wao ni mfumo dume tu.

CCM ina Dira na yote. Hakuna wa kumzuia Rais Samia 2025. Tumuunge mkono.
 
watashinda tu maana hawana mpinzan mwenye sera nzur na hawana watu wa kupiga kura, hivyo watajipa ushindi wa98%....kama wapinzan wakibadirika kwanzia sasa na kuendana na matakwa ya wananchi, kwa kupinga ujinga wa ccm, na kumleta ama kumtambulisha mgombea anaejielewa, mwenye sera za ushawish angarau azibe pengo la yule bwana aliependwa na walala hoi, machinga, na wanyonge,kwa hapa ushindi kwa upinzan n nje nje yaan..

inauma ila ndyo ukwel, wapinzan kuchukua nchi bila kubadirika kwanza wao, ni ngumu sana
 
Kila nikitazama maisha yanavyozidi kua magumu, watu wanavyolia na ugumu wa maisha na hali inazidi kua mbaya kuliko siku za nyuma, siioni imani ya CCM kushinda uchaguzi 2025. Ugumu wa maisha hua ni sababu tosha kukiondoshea mapema chama ukombozi.

Mtapiga watu, wagombea kupitia vyama vya upinzani watapitia mateso makali sana, wataumia sana lakini mwisho wa siku ndogo ndio wakaoongoza taifa kwa msaada wa wananchi waliochoka. Polisi wanaweza kupiga na kuumiza watu lakini hawawezi kulifanya hilo nchi nzima.

Kazi kubwa iliyopo kwa wapinzani na wanaharakati wengine ni kuondoa makada wa CCM kule NEC na wakurugenzi kutosimamia Uchaguzi. Na hilo ni lazima kwa namna yeyote ile haliwezi kuachiwa, hii ni nchi yetu sote.
Kila akiwemo mmoja asiyeziona fursa wanakuwepo kumi wenye kuziona. Ndio maisha yalivyo, wapo wenye kupenda kulialia wasio na ubunifu wowote kichwani na wapo wenye ubunifu na wasio na kelele kabisa.
 
Kila nikitazama maisha yanavyozidi kua magumu, watu wanavyolia na ugumu wa maisha na hali inazidi kua mbaya kuliko siku za nyuma, siioni imani ya CCM kushinda uchaguzi 2025. Ugumu wa maisha hua ni sababu tosha kukiondoshea mapema chama ukombozi.

Mtapiga watu, wagombea kupitia vyama vya upinzani watapitia mateso makali sana, wataumia sana lakini mwisho wa siku ndogo ndio wakaoongoza taifa kwa msaada wa wananchi waliochoka. Polisi wanaweza kupiga na kuumiza watu lakini hawawezi kulifanya hilo nchi nzima.

Kazi kubwa iliyopo kwa wapinzani na wanaharakati wengine ni kuondoa makada wa CCM kule NEC na wakurugenzi kutosimamia Uchaguzi. Na hilo ni lazima kwa namna yeyote ile haliwezi kuachiwa, hii ni nchi yetu sote.
Imani ya ccm siku zote ipo kwa tume ya uchaguzi na jeshi la polisi.
 
Huu uchafu ulioandika hapa kama CCM inakubalika tusingeona mabegi ya kura za wizi ili ccm watangazwe washindi kwa shuruti. Kama CCM ingekuwa inajali wakulima, basi wakulima wasingekuwa wanaoongoza kwa umasikini nchi hii.
Ndiyo shida yenu. Mnafikiria kibwanyenye sana.
 
Back
Top Bottom