Siioni amshamsha ya Forex, vipi watu wameshapigwa?

Screenshot_20171215-150016.png Tunaendelea kutengeneza za xmas
Screenshot_20171215-150016.png
Screenshot_20171215-150248.png
 
aliyefaidika sana na Forex trade ni Ontario tu na timu yake.. na faida kaipata kwenye training fees na commission ya broker wa forex.. hii ya commission ameipata indirect kwa akili nyingi sana hakuna mwanafunzi wake hata mmoja anaeweza kujua

Hahahha tz raha sana
 
Napenda kuleta Uzi huu mahususi kabisa kwa wale jamaa zangu wa FOREX !!! Nimeona niseme kitu coz hapo mwanzo kipindi ndugu na jamaa yetu bwana Antario alipoanzisha uzi wa Forex !!!
Naweza kusema nyuzi zake zilipata waafuasi wengi sana hata Mimi nikiwemo !!!
Ninachojiuliza kwa sasa je? Forex hii mbona imepoteza mvuto na lile amsha amsha kama la mwanzo mbona limekufa? Au tayari watu wameshalizwa? Au wanatengeneza mapesa kimyakimya?

Hapana !!! Hapa kunakitu haiwezekana Jf ipoe kiasi hiki kuhusu hii Forex !!!
Maana hakuna mlejesho wowote wa MTU ambaye tayali amesha nunua hata passo kwa kutumia pesa ya Forex !!!!
Povu linaluhusiwa !!!!!
Mkuu fanya unaloweza...au umbea ndo kitu pekee unachoweza zaidi hapa Duniani?,
Labda kwa kukusaidia ni kwamba hata daraani kuna wanaofaulu na kushindwa,ndivo ilivyo kwa Forex.
Halafu unaonekana unafurahia sana kushindwa kwa watu...hizo ndo roho zikomaa unashangaa mtu kawa mchawi
 
Back
Top Bottom