Sihitaji ufahari na ubishoo Jimboni Arumeru Mashariki - Nassari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sihitaji ufahari na ubishoo Jimboni Arumeru Mashariki - Nassari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 20, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145  [​IMG]  NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-MERU  MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari amesema kuwa yeye hataki mambo ya kifahari katika jimbo lake bali anaitaji kuwepo na mikakati mbalimbali ambayo itaweza kuwasaidia wananchi wake katika harakati mbalimbali za maendeleo.

  Kauli ya Bw Nassari aliitoa mapema wiki hii katika eneo la Sakila ndani ya kituo cha watoto yatima cha African Orphanage wakati wa hafla kwa watoto hao na mmiliki wake.

  Bw Nassari alisema kuwa ni aibu kubwa sana endapo kama ataendekeza zaidi ufahari wakati wananchi wake wakiwa wanateseka na changamoto mbalimbali za kijamii huku muda nao ukiwa unadhidi kunyongonyea.

  Alisema kuwa kwa muda wake mwingi sana atahakikisha kuwa anajikita na matatizo ya kijamii ambayo yamekuwa ni kilio kikubwa sana kwa wananchi wa Jimbo la Arumeru Mashariki ambapo changamoto hizo zinaweza kuepukika endapo kama watakuwa na umoja.


  “Mimi sihitaji ubishooo au ufahari ndani ya jimbo hili kwa kuwa wapo baadhi ya viongozi ambao wanaendekeza zaidi ubishoo na ufahari huku majimbo yao yakiwa na shida sasa sasa mimi natangaza hadharani hapa kwangu hamna kitu kama hicho”aliongeza Bw Nassari.

  Pia alisema kuwa kwa upande wa Magari ambayo nayo hutumika mara nyingi na viongozi hasa pale wanapopata ubunge kwa upande wake yeye atatumia usafiri wa Kawaida sana ambapo baadhi ya fedha atazielekeza jimboni.

  “jamani leo mnaona gari ambao mimi ninalo ni lakawaida sana si gari la kifahari na hata mara nyingine mimi kama mimi huwa natumia hata usafiri wa pikipiki(TOYO)kwa kuwa siendekezi ubishoo zaidi ila naelekeza nguvu zangu nyingi katika kusaidia jamii”aliongeza Bw Nassari.

  Naye mkurugenzi wa kituo hicho cha watoto yatima bw Nickson alifafanua kuwa viongozi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajijenga zaidi katika mitizamo ambayo itaweza kuwasaidia wananchi na wala sio kulumbana.

  Bw Issangya aliwataka viongozi kuhakikisha kuwa katika nyakati za sasa wanajikita zaidi kwa makundi maalumu kama vile yatima na wajane kwa kuwapa misaada ambayo inalenga kuwasogeza zaidi mbele na wala sio kuwatenga kama ilivyo kwa baadhi ya familia.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  BRAVO!!! Aheri Unasema Ukweli afadhali Unaondoa ULAU-MASHA jimboni kwako Mapema sababu una Miaka Miwili tu Uchaguzi

  Mwingine Unakuja 2015 ni karibu, na jimbo hilo litakuwa na upinzani sababu watajaribu kuweka mtu mkakamavu kuondoa

  Aibu ya kushindwa sababu walipeleka UONGOZI MZIMA na kuanguka kwa AIBU
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Hivi kuendesha gari zuri ni ubishoo?
   
 4. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakuamini sana mwana
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nani kaongelea kuendesha Gari Zuri??
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mkuu thread umeanzisha wewe halafu unataka kupingana nayo ngoja ninukuu maneno ya Nassari, kidogo halafu utatupata maana ya ubishoo.

  "Jamani leo mnaona gari ambao mimi ninalo ni la kawada natumia hata (TOYO) kwa kuwa siendekezi ubishoo"

  Mwisho wa kunukuu...Mbowe anaendesha gari la kifahari ni bishoo?
   
 7. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Big hon nassary kwani hapo wameru hawakukosea kabisa.
   
 8. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mhe ritz, hata kama unalipwa kwa kuitetea chama kinachojifia chenyewe natural death... Je? unaridhika na hali ya maisha ya watanzania wa kawaida yalivyo? unafurahia watoto wetu kukosa elimu bora? unaridhika na huduma za kijamii zinazopaswa kutolewa na serikali iliyoko madarakani? unaridhika na uuzaji wa rasilimali zetu kwa jina la uwekezaji? unaridhika jinsi madini yetu yanavyosafirishwa kwa makontena na kuita mchanga? unaridhika kuendesha VOGUE lako kwenye madimbwi ? UNARIDHIKA? Ni kweli kuwa HUHITAJI MABADILIKO?
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Hivyo vyote mie siridhiki navyo mkuu, mie nilikuwa nauliza tu kutembelea gari zuri ni ubishoo?
   
 10. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  ritz una taabu ktk kuchangia.Sijui huwa unasubiri majina fulani ukiyaona tuu unarukia unachagua kipande cha kutumia the una shambulia.
  Hembu nikuulize.
  Kwa nini watu wanpenda unadhifu wakitoka?Kwa nini watu wanapenda aina fulani ya magari hata km vitu vya msingi ndani vikiwa vinatoa uhuru kama mengine ya bei ya chini au hata brand isiyo na jina kubwa?

  Yote haya ni kupata mtazamo wa kukubalika na kupewa heshima kuliko wale walioshindwa pata vyote hivyo.Ubishoo unahusiana na image projection hasa materaial things na power au kumfanya bishoo kuwa detached from the society ili awe favourity.Nasser bado anaona hakuna cha kumtenganisha na maisha ya kawaida wanayoishi watu wengine ktk jimbo lake.

  unless utapoteza muda kudai kuwa uzuri uanotafsiri sio huo,ila Nassar anousemea ni huu wa kuwa gari ghali lenye naksi za ziada.Sidhani km kuna waziri atayeweza panda toyo,sababu ya kwanza ni personality , ya pili labda security.Ila wanaweza panda tuu kipindi cha chaguzi na usiku pale watakapoenda kwa wagangakule kwetu unapohitaji panda aina zote za usafiri haki kufika.Sijui km ahadi za kuweka madaraja na vivuko litakamilika.
   
 11. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  well kama huridhiki then tumia kipaji chako kuwakomboa watanzania wenzako mafukara wa kunuka lakini wenye utajiri wa kunukia dunia nzima kaka... TAIFA MBELE MKUU... wewe hapo ulipo ikitokea umeugua ghafla bado utapelekwa kwanza kwenye hizi hospital ambazo kuanzia wahudumu mpaka madaktari wako demoralized kupita kiasi achilia mbali ukosefu wa nyenzo muhimu...Mkuu ACHA PROPAGANDA ZA KIPUMBAVU PIGANIA TAIFA LAKO....
   
Loading...