Sihitaji kuwa Mkazi wa Mwanza tena la sivyo nitakufa na makachero

SITEGEMEI KUWA MKAZI WA MWANZA, NITAKUFA NIKIWA MASKINI KUISHI MKOA HUU.

Wananchi ni vibaraka wa kuharibu maisha ya Wazalendo, watumishi wa Umma vibaraka wa kupotoshea vyombo vya Usalama, wafanyakazi mashirika binafsi wapokeaji wataarifa za kurubuniwa.

Yaani Mwanza nzima imemfanya DON NALIMISON Kama Msukule wao wakufanikiwa. Nitawaachia limkoa lenu muda wowote msije mkaniua kwa Vipaji alivyonipa Mungu.

Mimi sio fala. Kila napokuwa nashangaa nazingirwa na MAKACHERO, mnataka Nini kwangu. Nikifika ofisi moja wameshaingia na kupotosha.....Duuuuuu, tukutane KAHAMA na DAR ES SALAAM nilikozoea. Mimi siwezi kushindana na Mishosha ng'ombeeeeeee.

DON NALIMISON.
View attachment 1525471
Karibu daslam ule chips na mayai... Halafu jion tunashushia na alkasusu
 
Namkumbuka rafiki yangu mmoja aliyevurugwa tukiwa kazini alikuwa ananiambia mtaa mzima unamsema yeye tu, anafuatwa kila anakokwenda, anatafutwa na wanajeshi wengi. Anawindwa na wahuni wa mtaani kwao. Wamama wa mtaani kwao humsema yeye tu.
Siku moja tuko nje ya ofisi wamama kama wawili hivi walikuwa wanapita nje ya ofisi yetu yaani barabarani huku wakipiga story zao akaniambia unasikia hao wamama wanavyonisema?
Yaani wamama wamemfuata kutoka Kigogo, kariakoo mpaka kazini!!!!!
Nikajua ashavurugwa.
Don hizo ni feelings tu na dalili mbaya.
Umenikumbusha John Nash.
 
Brother, kwa kukaa muda mwingi korokoroni, ni dhahiri kisaikolojia umeathirika sana. Jipe muda wa kutosha ili upumzishe vyema mwili na akili zako, kabla ya kuanza tena shughuli zako za uanaharakati

Kwa kushindwa kufanya hivyo, kila mtu utamshuku anafutilia nyendo zako. Na pengine miongoni mwao utahisi ni watu wabaya kwako, ingawaje kiuhalisia inakuwa ni kinyume chake.

Jipe muda wa kupumzika bro, zingatia kufanya ibada na kuomba kwa bidii mbele ya Mola wako, tafuta mtandao bora wa rafiki zako wa karibu ili upate kujichanganya nao, kula na kunywa kwa kuzingatia viwango bora vya afya, fanya mazoezi ya mwili, jipe muda wa kusoma vitabu, magazeti na vijarida mbalimbali. Hakika ndani ya miezi sita msongo wote wa mawazo utakuwa umeutua kutoka ktk kichwa chako.
Ameathirika baada ya kukaa korokoroni muda mrefu? We unamjua Kisandu kabla ya kufungwa? Mbona saa hizi ana nafuu hapo kisaikolojia

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom