Sihitaji kura za wafanyakazi (T-shirt Ziko Mitaaani)

Mtu66

Senior Member
Jun 26, 2007
165
3
Naona hizi T-shirt za Sihitaji kura za wafanyakazi ziko mitaani
Wapi zinapatikana? Mwenye Taarifa Jamani...

2dwatk2.jpg


Picha na Saidi
 
Itakuwa poa sana kama zitavaliwa kwa wingi siku ya kupiga kura ili kukumbushana kwamba hahitaji kura za walala hoi.
 
Hakuna Kauli mbaya Kisiasa aliyowahi kuitoa Muungwana inayoizidi hiyo (Sihitaji kura za wafanyakazi).Muungwana si mtu wa majivuno na ujeuri....Lakini miaka yake mitano ya Uongozi wa Nchi kajifunza tabia mbaya....sikuwa najua kwamba mtu anaweza kubadilika tabia ukubwani!
 
hakuna kauli mbaya kisiasa aliyowahi kuitoa muungwana inayoizidi hiyo (sihitaji kura za wafanyakazi).muungwana si mtu wa majivuno na ujeuri....lakini miaka yake mitano ya uongozi wa nchi kajifunza tabia mbaya....sikuwa najua kwamba mtu anaweza kubadilika tabia ukubwani!

watu huwa hawabadiliki tabia wanapopata pesa au madaraka
kinachotokea ni kuwa tabia zao halisi ndio zinajitokeza....
Sasa wasiojua husema amebadilika but ukweli
hizo ndo tabia halisi za mtu...
 
Hakuna Kauli mbaya Kisiasa aliyowahi kuitoa Muungwana inayoizidi hiyo (Sihitaji kura za wafanyakazi).Muungwana si mtu wa majivuno na ujeuri....Lakini miaka yake mitano ya Uongozi wa Nchi kajifunza tabia mbaya....sikuwa najua kwamba mtu anaweza kubadilika tabia ukubwani!

Bal Mwawado! Madaraka hulevya sana
 
ni t-shirt nzuri sana...mwenye taarifa ya wapi zinapatikana atujulishe mapema tunazihitaji mno hasa kwenye hiki kipindi maalum
 
Inapaswa kutengenezwa nyingine inayosema "Watanzania ni Wafuata Upepo" pia!
 
Itakuwa poa sana kama zitavaliwa kwa wingi siku ya kupiga kura ili kukumbushana kwamba hahitaji kura za walala hoi.

Labda na hayo maandishi na mchoro/picha yangeandikwa kwa ubunifu zaidi...I mean bila picha yake maana kwa asiyejua kusoma anaweza kufikiri anasifiwa kwa kazi nzuri aliyoifanya. My imagination - picha ya mbayuwayu (ndege) na maandishi hayo!
 
Hii kauli imeandika historia mpya ya muungwana. Ile siku jamaa 'alitapika' hovyo kabisa kama alikuwa amekunywa mataputapu. Ila alionesha wazi tabia yake ya ndani ambayo amekuwa akiificha kwenye mwavuli wa uungwana. Hii harakati ya kutengeneza tshirt ni nzuri sana, nadhani wanaweza kutengeneza na kanga kabisa...ikawekwa mbayuwayu kama The Boss anavyoshauri, basi zitanoga sana. Itawakumbusha hawa tuliowapa dhamana kuwa 'wakitutapikia' historia itawahukumu
 
Kikwete kama mwanasiasa ambaye cheo chake hutokana na kura, alisahahu kuwa "every vote counts." Huenda anajua kuwa hata asipopigiwa kura na wafanayakazi (pamoja na familia na marafiki zao) bado zitatengenezwa nyingine zaidi ya hizo kumhakikishia ushindi wa kimtindo.
 
Maandishi na picha ni nzuri lakini rangi ya fulana ni mbaya. Mtu akiwa mbali atadhani jamaa anapenda chama chao, kumbe siyo. Rangi nyeupe au bluu safi.
 
Bal Mwawado! Madaraka hulevya sana

Umeniwahi Mkuu, tena hulevya sana na mtu kujiona kama ni Mungu mtu na kujisahau hata kwenye kauli zake na kutoa kauli zilizojaa ufedhuli wa hali ya juu.
 
Rangi yake isiwe hiyo ya chama cha mafisadi .
Mimi nadhani inatakiwa ku quote hayo maneno pamoja na siku /tarehe,Tshirt let be white picha sio lazima kufanya iwe cheap.

Sihitaji/sitaki kura za wafanyakazi
Kikwete xxApril,2010
 
Itakuwa poa sana kama zitavaliwa kwa wingi siku ya kupiga kura ili kukumbushana kwamba hahitaji kura za walala hoi.
BAK

Siku ya kupiga kura huruhusiwi kuvaa kitu chochote chenye kutambulisha itikadi au chama chako.

Na mimi naungana na wanaosema rangi ya tshet iwe nyeupe au bluu na maandishi yawe makubwa kwa sababu lengo ni ujumbe wa maneno kufika. Move hii inaonyesha kumbe mawazo yetu tunayotoa humu JF sometimes yanafanya kazi nakumbuka wazo hili lilianza humuhumu, JF idumu.
 
Back
Top Bottom