Siha: Madiwani waugomea mradi wa Maji, Mbunge aagiza kukamatwa kwa Mkandarasi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Mbunge wa Siha (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Godwin Mollel amemtaka mkandarasi aliyejenga mradi wa maji wa Gararagua kutafutwa popote alipo kwani umejengwa chini ya kiwango.

Amesema hayo leo Alhamisi, Julai 21, 2022 katika Ofisi ya Bodi ya Maji, Magadini Makiwaru iliyopo Karansi wilayani humo, wakati Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), wakikabidhi mradi huo kwenye Bodi hiyo.

Madiwani wa Halmashauri hiyo wamekataa kuupokea kwa madai umejengwa chini ya kiwango.

Dk Mollel amesema kwa gharama yoyete ile ni lazima mkandarasi huyo atafutwe alipo ili ajieleza kwa nini amejenga chini ya kiwango na kusababisha mabomba kupasuka hovyo.

Dk Mollel ambaye pia ni naibu waziri wa afya amesema mradi huo umesababisha kufanyika ukarabati wa mara kwa mara hata kabla ya kukabidhiwa kwenye bodi na wananchi kukosa maji.

"Tutakaa na madiwani wa halmashauri hii, pamoja na mhandisi wa mkoa na naomba mkurungenzi wa idara ya maji wa wizara, tukae tupitie ili tumalize jambo hili na kama itathibitika hatua za kisheria zichukuliwe haraka,” amesema

"Mradi huu umejengwa chini ya kiwango, kitakachotutoa hapa ni wapime Bomba wakishapima turudi sasa tujue nini kimetokea, maana mradi huu umetekelezwa kwa zaidi ya Sh1.7 billion, hizi ni fedha nyingi za Serikali, haiwezekani tunyamaze," amesema Diwani wa Gararagua (CCM), Zakaria Lukumay.

Jonathan Nathari wa Kata ya Orkolili, amesema kwenye kata yake asilimia kubwa ya wananchi hawana maji kutokana na mradi huo kutokamilika na kwamba walishatoa maelezo kwa muda mrefu kuchunguzwa mradi huo lakini ombi hilo limekuwa likipuuzwa.

"Kwa hiyo mimi sintakuwa tayari wala sintoridhika kupokea mradi kabla haujakamilika, inatuweka eneo baya, kama mradi ungekamilika maji yangeenda hadi kule yanakotakiwa kufika," amesema Nasar

Makamu Mwenyekiti wa Halmashari hiyo Noel Mollel, amesema "tulishakaa kwenye kikao maalumu kuhusu mradi huu na kumtaka Meneja wa Ruwasa Wilayani hapa Emmy George kuuchunguza na kutupa ripoti.”

“Leo nashangaa kuitwa ili mradi ukabidhiwe kwenye Bodi wakati ripoti yetu tuliyoomba ya uchunguzi hatujaletewa," amesema

Kwa upande wake, Meneja wa Ruwasa Wilayani humo, Emmy George amesema hakuna tatizo lolote katika mradi huo na kwamba yaliyopo ni ya kawaida.

Chanzo: Mwananchi
 
Ni kawaida mradi kuwa na matatizo madogo madogo wakati unakabidhiwa. Ndio maana kuna muda wa matazamio ambapo mkandarasi atatakiwa kurekebisha dosari zote zitakazojitokeza wakati wa matumizi. Mshitiri anakuwa ameshika kiasi fulani cha malipo ya mkandarasi hadi mwisho wa matazamio utakapoisha na mshauri kuthibitisha kuwa dosari zote zimerekebishwa.

Hao madiwani kukataa kupokea mradi kunazuia dosari nyingine kuweza kugundulika. Na muda wa matazamio unaanza pale mkandarasi anapomkabidhi mradi muajiri wake baada ya msimamizi kuthibitisha kuwa unaweza kutumika na kwa kiasi kikubwa umekidhi viwango na maelekezo ya mkataba.

Amandla...
 
Mbunge wa Siha (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Godwin Mollel amemtaka mkandarasi aliyejenga mradi wa maji wa Gararagua kutafutwa popote alipo kwani umejengwa chini ya kiwango.

Amesema hayo leo Alhamisi, Julai 21, 2022 katika Ofisi ya Bodi ya Maji, Magadini Makiwaru iliyopo Karansi wilayani humo, wakati Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), wakikabidhi mradi huo kwenye Bodi hiyo.

Madiwani wa Halmashauri hiyo wamekataa kuupokea kwa madai umejengwa chini ya kiwango.

Dk Mollel amesema kwa gharama yoyete ile ni lazima mkandarasi huyo atafutwe alipo ili ajieleza kwa nini amejenga chini ya kiwango na kusababisha mabomba kupasuka hovyo.

Dk Mollel ambaye pia ni naibu waziri wa afya amesema mradi huo umesababisha kufanyika ukarabati wa mara kwa mara hata kabla ya kukabidhiwa kwenye bodi na wananchi kukosa maji.

"Tutakaa na madiwani wa halmashauri hii, pamoja na mhandisi wa mkoa na naomba mkurungenzi wa idara ya maji wa wizara, tukae tupitie ili tumalize jambo hili na kama itathibitika hatua za kisheria zichukuliwe haraka,” amesema

"Mradi huu umejengwa chini ya kiwango, kitakachotutoa hapa ni wapime Bomba wakishapima turudi sasa tujue nini kimetokea, maana mradi huu umetekelezwa kwa zaidi ya Sh1.7 billion, hizi ni fedha nyingi za Serikali, haiwezekani tunyamaze," amesema Diwani wa Gararagua (CCM), Zakaria Lukumay.

Jonathan Nathari wa Kata ya Orkolili, amesema kwenye kata yake asilimia kubwa ya wananchi hawana maji kutokana na mradi huo kutokamilika na kwamba walishatoa maelezo kwa muda mrefu kuchunguzwa mradi huo lakini ombi hilo limekuwa likipuuzwa.

"Kwa hiyo mimi sintakuwa tayari wala sintoridhika kupokea mradi kabla haujakamilika, inatuweka eneo baya, kama mradi ungekamilika maji yangeenda hadi kule yanakotakiwa kufika," amesema Nasar

Makamu Mwenyekiti wa Halmashari hiyo Noel Mollel, amesema "tulishakaa kwenye kikao maalumu kuhusu mradi huu na kumtaka Meneja wa Ruwasa Wilayani hapa Emmy George kuuchunguza na kutupa ripoti.”

“Leo nashangaa kuitwa ili mradi ukabidhiwe kwenye Bodi wakati ripoti yetu tuliyoomba ya uchunguzi hatujaletewa," amesema

Kwa upande wake, Meneja wa Ruwasa Wilayani humo, Emmy George amesema hakuna tatizo lolote katika mradi huo na kwamba yaliyopo ni ya kawaida.

Chanzo: Mwananchi
Wapinzani wametucherewasha sana sasa TUSONGE mberee......
In mwendazake voice
 
Back
Top Bottom