SIHA KILIMANJARO: Viboko 15 na faini ya 50,000 kwa atakayekutwa baa usiku na mtoto

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Serikali ya Kijiji cha Sanya Hoye, Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro imetangaza adhabu ya kuchapwa viboko 15 na kulipa faini ya Sh.50,000 kwa mkazi yeyote atayekutwa baa nyakati za usiku, akiwa ameambatana na mtoto mwenye umri chini ya miaka 18.

Chanzo: Radio One
 
So mwenye miaka kuanzia 15 anaruhusiwa kuingia bar?
 
Ifike na Dar maana ni too much
Unaona birthday parties Za watoto zinafanyika bar tena usiku
 
Bar nyingi sana wanapika chakula na hawajatenga sehemu maalum kwa wale wanaokwenda kula chakula tu. Chili nalo liangaliwe.
 
Siha naona wanajitahidi kurudisha heshima katika jamii. Juzi Kati tu Kijiji cha Karansi kiliazimia kuchapwa viboko sabini kwa watoto wa kiume wanaovaa mitepesho. Leo tena Kijiji kingine cha Sanya Hoye kimeazimia kucharazwa bakora na faini juu! Wanahitaji kuigwa na jamii.
 
Suala la fani hilo ni la kwao na nadhani wana kanuni zinazowaruhusu.. Ila kumtandika mtu bakora ipo nje ya uwezo wao.. Maana hiyo inahusisha na kuwepo kwa madaktari kwa ajili ya kuwapima afya watandikwaji kabla ili kuangalia kama afya inaruhusu.. Halafu viboko 15 ni vingi sana kulingana na kosa lenyewe..

Pia swali la msingi, watahakikishaje kama wapo under 18 hao watakaokutwa..? kwa kuangaliwa..?
 
Back
Top Bottom