'Sigara Zimeniua'

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,079

4176050.jpg

Jeneza la Mzee Albert likiingizwa kaburini huku bango la maandishi 'Sigara Imeniua' likiwa pembeni Wednesday, March 03, 2010 11:16 PM
Mvuta sigara aliyeteseka miaka mingi kutokana na magonjwa yaliyotokana na uvutaji sigara ametimiziwa matakwa yake kuwa atakapofariki jeneza lake na kaburi lake liweke maneno yanayosema 'Sigara Zimeniua'. Jeneza la mzee Albert Whittamore lilizungushwa katika mitaa ya mji wake nchini Uingereza huku likiwa limewekewa maneno 'Sigara Zimeniua'.

Mzee Albert aliyefariki mwishoni mwa mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 85, aliacha wosia kuwa atakapofariki kaburi na jeneza lake liwekewe maneno hayo ili kuwaonya vijana wasije wakapoteza maisha yao kama alivyopoteza ya kwake kutokana na magonjwa yaliyotokana na uvutaji sigara.

Mzee Albert aliteseka miaka mingi sana kutokana na matatizo ya mapafu, ugonjwa uliotokana na uvutaji wake uliokithiri wa sigara enzi za ujana wake.

Bango lilitengenezwa na kuwekewa maandishi ya 'Sigara Zimeniua' kabla ya jeneza lake kuzungushwa kwenye mitaa kadhaa ya mji wa Dover uliopo kilomita 160 toka jijini London.

Kwenye kaburi lake nako kuliwekewa bango kama hilo ambalo inasemekana litakaa hapo kwa muda wa wiki moja.

Mzee Albert kabla ya kufariki alikuwa akiwausia vijana kuhusiana na madhara yanayotokana na uvutaji wa sigara.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4176050&&Cat=7
 
Siku zake zilikuwa zimefika hata kama asingevuta sigara, 85 years old kusumbuliwa na magonjwa ni jambo la kawaida hata kama haukuvuta sigara!
Asiwaharibie watu biashara zao!
Na Sigara si zina onyo, yeye hakuliona?!
 
so sad, guys stop smoking!

ni kweli pape ila hiyo ni roho aitoki kirahisi inaitaji ujitoe
kweli kweli kwa mungu uamue umtolee dhabihu mungu maana
ukiangalia kwenye life za wengine hiyo no laana ya ukoo
kama kisukari,uzinzi,pressure haya mambo ni kukataa kwa jina la yesu
we unafikia kufia guest wakati una mke si laana hiyo pape
ndiyo haya mpaka unakufa unavuta sigara
 
Siku zake zilikuwa zimefika hata kama asingevuta sigara, 85 years old kusumbuliwa na magonjwa ni jambo la kawaida hata kama haukuvuta sigara!
Asiwaharibie watu biashara zao!
Na Sigara si zina onyo, yeye hakuliona?!

maisha ya kuishi mwanadamu ni 70 kwanza ashukuru mungu kumuongezea na kuwaomba radhi waliokuwa wakimtunza kwa kuharibu na kufuja pesa zao kwa miaka 15 iliozidi ambayo unatunza kajukuu kakubwa kabisa
 
Kuna wanaovuta paketi nzima na zaidi kwa siku.
Chakula walacho sio mlo kamili.
Kisa cha yote hayo ni kutafuta tu ujiko, ili waitwe chain smoker.
Nimehubiri wee hawajasikia, sasa kazi kwao.
 
Nilikuwa najiuliza ingekuwa vp kama marehemu aliyekufa kwa ugonjwa wa ukimwi
alafu kwenye jeneza lake pangeandikwa 'AIDS KILLED ME'
 
Mkuu Kabengwe! Huyu Marehemu amesema ameteseka siku nyingi na magonjwa ya MAPAFU sababu ya sigara.. Ndio maana akatuusia.

Siku zake zilikuwa zimefika hata kama asingevuta sigara, 85 years old kusumbuliwa na magonjwa ni jambo la kawaida hata kama haukuvuta sigara!
Asiwaharibie watu biashara zao!
Na Sigara si zina onyo, yeye hakuliona?!
 
alikuwa anavuta tumbaku sio sigara wazee wengi huwaga wanavuta tumbaku au alikuwa ajui kama sigara ni sumu ukizingatia na umri wake je hicho kifua kilijaa mimoshi
conquest
 
maisha ya kuishi mwanadamu ni 70 kwanza ashukuru mungu kumuongezea na kuwaomba radhi waliokuwa wakimtunza kwa kuharibu na kufuja pesa zao kwa miaka 15 iliozidi ambayo unatunza kajukuu kakubwa kabisa
mama mia kama kawaida yako unamwaga mapointi huku ukitoa referensi. big up

Hawa wajamaa wanatakiwa kushitakiwa kwa kuwashawishi vijana wadogo kuvuta sigara.....unaweza kuuwawa na sigara at 85? angekuwa bellow 45 hapo tungeeweza kuongea mambo mengine.
Hapo ni sawa na kuwaambia vijana vuteni masigara na mabange kwa wingi, you wont die any time soon.
 
Siku zake zilikuwa zimefika hata kama asingevuta sigara, 85 years old kusumbuliwa na magonjwa ni jambo la kawaida hata kama haukuvuta sigara!
Asiwaharibie watu biashara zao!
Na Sigara si zina onyo, yeye hakuliona?!

Sikio la kufa halisikii dawa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom