Sigara hupunguza nguvu za kiume

drgeorge

Member
Jun 22, 2009
99
23
Sigara na marijuana ni miongoni mwa sababu zinazochangia kupungua kwa nguvu za kiume.

Saababu zingine ni msongo wa mawazo, hofu au mashaka. Wanaume wengi wanaupungufu wa nguvu za kiume lakini si kwa sababu ya ugonjwa yaani pathology, ila ni kiakili yaani psychology.

Kula vizuri, suluhusisha matatizo yako, ondoa wasiwasi na mashaka, uwe unacheki afya yako, mwamini mungu.

Mambo yataenda sawa kabisa, ila kama kuna dalili zozote zisizo za kawaida kuhusu uzazi onana na wataalamu wa afya, daktari mapema, acha kujitibu kienyeji.
 
Mambo yanayochangia upungufu wa nguvu za kiume.

Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu. Mzunguko wa damu mwilini una maana sana kwani kama damu haizunguki vizuri itachangia uume kutosimama vizuri kwa sababu usimamaji hutegemea kiasi na kasi ya damu inayoingia kwenye mishipa ya sehemu hiyo. Dawa zinazotumika kutibu shinikizo la damu huchangia pia kupungua kwa nguvu za kiume.

1. Unywaji pombe kupita kiasi: Pombe inaweza kuathiri mishipa ya damu na mishipa ya fahamu kwa wakati mmoja. Wakati mwingine mtu akilewa sana huathiri ubongo na kukata mawasiliano kisaikologia na hivyo kushindwa kuwa katika hali ya kuwa na hamu ya ngono na hivyo kutosimamisha.

2. Unene. Unene huwa unaambatana na mafuta mengi mwilini. Mafuta hayo wakati mwengine huzidi kwenye kuta za ndani za mishipa ya damu na hivyo kupunguza ukubwa wa mrija kiasi kwamba damu inipita kidogo na kwa shida. Hii huchangia kupungua kwa nguvu za kiume kwa sababu kiasi cha damu kinachotakiwa kisimamisha uume kitakuwa kidogo sana. Wakati mwingi uume unaweza kusimama kidogo na kulala kabla shughuli haijakamilika.

3. Kutokufanya mazoezi: Tusipofanya mazoiezi pia mzonguko wa damu kutokuwa mzuri na hivyo kutoparuhusu damu ya kutosha kusimamisha uume. Kwa watu wanaotembelea magari na shughuli za kukuaa maofisini mda mrefu na hasa kama hawafanyi mazoezi asubuhi au jioni wako kwenye hatari zaidi kuliko watu wanotembea kwa miguu mwendo mrefu na kufanya kazi ngumu za kuuchosha mwili.

5. Matatizo ya kisukari: Kisukari ni ugonjwa unaoathiri mishipa ya fahamu na kufanya mishipa ya damu kutofanya kazi yake viuri ili kuruhusu damu kujaa kwenye uume. Hii himfanya mgonjwa wa kisukari kushindwa kusimamisha hata kama ana hamu ya kufaya tendo hilo.

5. Umri: Inaelezwa kuwa kadri umri unavyopanda ndio uwezo wa nguvu za kiume utaendelea kupungua. Baadhi ya watu huanza kuona tatizo hili wanapofikia umri wa miaka 40 na kuendelea na hasa kama maisha yao hayakuwa na mazoezi ya mwili. Sababu

nyingine ni kama utumiaji madawa ya kulevya, kuumia katika uti wa mgogongo, uvutaji sigara nk. Sababu nyingi zinachangia kupungua kwa nguvu za kiume zinaepukika kwa hiyo tunashauriwa kuwasiliana na wataalamu ili kujifunza jinsi ya kujikinga au kutibu matatizo
 
Tunashukuru kwa maada nzuri ambayo wanaume tunatakiwa kuzingatia ili tuendelee kuwa ngangari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom