Sifurahishwi kabisa na utaratibu huu wa Ubungo Bus Terminal | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sifurahishwi kabisa na utaratibu huu wa Ubungo Bus Terminal

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kinyoba, Jun 8, 2011.

 1. kinyoba

  kinyoba JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 1,238
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Habari za leo wadau, kuna hili swala la kulipa sh 200/ au kuonyesha tiketi wakati wa kutoka ndani ya stand. Wanapokuuliza tiketi wao wanadhani uliingilia wapi? Ni lazima uwe umekuja na bus toka mkoani au ulilipa sh 200 getini.

  Ni kero sana kuanza kutafuta tiketi ulipoiweka na mara nyingi ni vigumu kuiona sababu ya urefu wa safari may be from mbeya, au ile tiketi ya sh 200 mtu anaweza kuipoteza pia.

  Ninavyoona pale hawapaswi kuwadai chochote watu wanaotoka stand, zaidi ni wizi tu wa waziwazi na usumbufu usio na lazima. Wao wajishuhulishe na watu wanaotaka kuingia stand.

  Hilo ni wazo langu wadau sijui ninyi mnaonaje.
   
 2. 1

  19don JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  kweli ni usumbufu tu unapo ingia terminal unaonyesha tiketi na wakati wa kutoka uonyeshe pia wakati hakuna njia ya mkato unayoweza kuingia terminal bila kupitia kwenye gates zao hii ni kero na usumbufu kwa abiria tu.
   
 3. j

  jmhangate Member

  #3
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hawajui wanapotezea watu muda; nchi hii inahitaji vitu wiwili ili iendelee
  1. Kujali muda
  2. Kuwajibika

  Muda unaotumika kutafuta tiketi mfukoni unaweza kusababisha baadhi ya watu waendelee kusubiri; huu ni upotezaji wa muda usio na sababu
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,000
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  jifunze kuitunza tiketi yako, pia kaa nayo karibu maana bila kufanya hivyo walinzi watshindwa kujua kama ulikuwa nayo au la. kumbuka ubungo kuna watu wengi sana wanaoingia, kwani anaetoka mkoani ana sura tofauti na wa pale pale ubungo?
   
 5. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #5
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,000
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  aisee nyie vilaza kweli, kwanini ukikaribia usiwe umeiandaa kabisa? huoni hata huo upuuzi uliouandika hapo ni kupoteza muda?
   
 6. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #6
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,000
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  sasa bila kuonyesha unataka uaminike kwa lipi?
   
 7. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #7
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,000
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mod hamisheni hii post, nadhani imepotea njia kidogo.
   
 8. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #8
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanaojua umuhimu wa kujali muda ni wachache sana.
  Huyo inaetaka ajali muda wako...anahisi akikupotezea muda huenda akapata chochote kutoka kwako.
  Hapo unafikiri lini la muda litakua wanalijali?
  Kuna siku nlikuepo pale kidogo nishikane nao mashati...ati! Natoka mkoani nimechoka wanaitaka tiketi ya safari/kuingia...nikawajibu sina!
  Wakasema hupiti hapa hadi uoneshe ....nikawaona majinga tu! Hayafikirii kabisa...yanaudhi kabisa.
   
 9. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #9
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni hivyo...kuna maana gani wakuzuie wakati unaingia ndani?
  Wakuache uingie ili ukiwa unatoka wakuombe hiyo tiketi waitakayo.
  Yaan ukiwa unaongea nao...watazame sura zao!
  Hawana uelewa kabisa.
  Nahisi wapo kama migambo ya jiji-dar.
   
 10. kinyoba

  kinyoba JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 1,238
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  wewe ni mvivu wa mawazo, na hufai kuwa great thinker, pia yaelekea hujaelewa kilichoandikwa, unadhani kuna njia ya mkato ya kuingia pale ubungo? au wewe huwa unaruka ukuta? au pia yawezekana wewe ni mmoja wa wezi wa pale mlangoni. ni upuuzi kuwa na mawazo mgando.
   
 11. kinyoba

  kinyoba JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 1,238
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  wewe ni mvivu wa mawazo, na hufai kuwa great thinker, pia yaelekea hujaelewa kilichoandikwa, unadhani kuna njia ya mkato ya kuingia pale ubungo? au wewe huwa unaruka ukuta? au pia yawezekana wewe ni mmoja wa wezi wa pale mlangoni. ni upuuzi kuwa na mawazo mgando.
   
Loading...