Sifurahiii wala sitaki kuona mwanamke anatoa mimba, ila kwa hali hii hebu tuseme tu ule ukweli "afanyeje"??

..... naona wengi mnakomaa kutoa mimba sio solution, hivi unaweza kuzaa huyo mtoto halafu uwe tayari kuishi na kovu kwenye akili yako miaka yako yote ya uhai hapa duniani kila ukimuona huyo mtoto?!

..... mnataka kusema mtu kubakwa ulikuwa ni mpango wa Mungu?, if yes, Mungu ni mbaya! kwanini Mungu asingempitisha njia nyingine ili asibakwe?

..... hilo janga likitokea kwa mtu wangu wa karibu namwambia ATOE serious, halafu amwambie Mungu nisamehe kwa kilichotokea.
Mwanamke akibakwa ana haki 200% za kutoa hiyo mimba,
 
Pamoja na hayo yote lakini;

Zoezi la utoaji mimba (Abortion) linapaswa kufanyika pale ambapo kiumbe kilichopo katika mfuko wa uzazi kitaleta madhara kiasi cha kuhatarisha maisha ya mjamzito husika.

Na hiyo ni baada ya kufanyika kwa vipimo vya kitabibu na Daktari/Madaktari kujiridhisha kuwa kuna ulazima huo, si kwa hisia tu za mjamzito mwenyewe bali vipimo.

Kwahiyo, ushauri bora zaidi nadhani ni wa kutunza huo ujauzito na huyo mtoto atakayezaliwa na pia mama wa mtoto huyo kupatiwa huduma maalumu ya kuituliza akili yake, namaanisha kuwa, apatiwe tiba ya kisaikolojia.
unadhani akipatiwa Tiba kisaikolojia na mwana saikoloji bora dunia nzima

kitendo cha kumuona yule mtoto mbele yake,hakitomkumbusha wapi alipomtoa?

kitendo cha mtoto kumuuliza baba ake anafananaje,je hatokumbuka?

labda yawezekana kuna jinsi ya kusahaulisha mtu wa namna hiyo,siwezi kujua maana sio mwana saikoloji.
 
matatizo ya kisaikolojia ni mabaya sana, wakati mwingine inakupasa kufanya maamuzi magumu. naamini hata Mungu ataelewa tu aise.
hata mimi huwa naamini hivyo,kuna mambo Mungu itabidi atuelewe tu kuwa ni magumu kwetu

akubaliane na matokeo tutakayoyachukua.
 
Kutoa mimba siyo solushen, kila kiumbe kina haki ya kuishi no matter what. Kwani watoto wangapi wanalelewa na wababa wasio wakwao? Kuna masingomaza wangapi wanalea watoto wao wakati wanaume waliosababisha wapo na wanajulikana kabisa, tena bora kwa kesi hii mwanaume hajulikani. Kutoa mimba ni dhambi, sawa na kuua, tusihalalishe dhambi juu ya dhambi. Lakini pia kwanini ubake? Ni upungufu wa akili na maarifa
unadhani mama atampenda yule mtoto kwa asilimia 100?

hebu fikiria upande huo? maana kuna swala la mtoto kupata haki ya kuja duniani

pili kuna swala la mtoto kupata huduma stahiki ikiwamo UPENDO wa dhati toka kwa mama na baba.
 
Nitalea mimba yangu na kuleta kiumbe duniani..dhambi yangu kubwa itakua pale tu mwanangu atakaponiuliza hilo swali la Baba yake yu wapi.
utamjibu nini? Dhambi yako itakua ipi hapo?
 
..... naona wengi mnakomaa kutoa mimba sio solution, hivi unaweza kuzaa huyo mtoto halafu uwe tayari kuishi na kovu kwenye akili yako miaka yako yote ya uhai hapa duniani kila ukimuona huyo mtoto?!

..... mnataka kusema mtu kubakwa ulikuwa ni mpango wa Mungu?, if yes, Mungu ni mbaya! kwanini Mungu asingempitisha njia nyingine ili asibakwe?

..... hilo janga likitokea kwa mtu wangu wa karibu namwambia ATOE serious, halafu amwambie Mungu nisamehe kwa kilichotokea.
ulichokiandika mpk atokee mtu wa kuniaminisha tofauti na mawazo yako

itam bidi afanye kazi ya ziada sana ili kunifanya nipingane na wewe...
 
FRANC THE GREAT Nani aliweka huo uamuzi? Serikali au Mungu?

Mimba kama mwanamke kabakwa ni haki yake 100% kuitoa, mwili ni wa kwake sio wa serikali, kuumia ataumia yeye na sio serikali

Huyo Mungu kama yupo na ana uwezo kweli basi angezuia huo ubakaji au hiyo mimba kutungwa
Asante sana
 
Ubakaji ni kosa kisheria na adhabu zipo!

Ila, mtu anapoongozwa na HISIA au MIHEMKO katika maisha yake siku zote ataishi maisha ya tabu sana hususani kiakili.

Wapo waliotoa mimba na maisha yakazidi kuwa magumu zaidi, na wengine wakashindwa kupata tena ujauzito katika maisha yao.

Kuna msemo unasema; You Should Not Make Decisions When You're Emotional!

Ninachosema ni kuwa, katika maisha hupaswi kuongozwa na hisia ama mihemko katika kufanya maamuzi maana kuna uwezekano mkubwa wa kuyajutia maamuzi yale hapo baadaye.

Ndiyo maana kuna Wataalamu wa Saikolojia ambao kazi yao ni kutoa tiba ya Kisaikolojia kwa watu walioathirika kwa namna hiyo ili wasije kufanya maamuzi mengine yatakayohatarisha zaidi maisha yao ya baadaye.
 
unadhani akipatiwa Tiba kisaikolojia na mwana saikoloji bora dunia nzima

kitendo cha kumuona yule mtoto mbele yake,hakitomkumbusha wapi alipomtoa?

kitendo cha mtoto kumuuliza baba ake anafananaje,je hatokumbuka?

labda yawezekana kuna jinsi ya kusahaulisha mtu wa namna hiyo,siwezi kujua maana sio mwana saikoloji.
Ndiyo maana kuna Professions kama Psychotherapists na Psychologists kwa ajili ya Cases kama hizo.

Akipatiwa matibabu ya namna hiyo kwa usahihi kabisa, hicho kitu hakitasumbua akili yake.

Maana tatizo si huyo mtoto anayemtazama kila siku. La hasha, tatizo lipo akilini ambapo akipatiwa matibabu sahihi hilo halitomsumbua.
 
labda tuangalie upande wa sheria. Lakini kiimani kutoa mimba changa sio tatizo, maana pale hujaua. Ni sawa na mtua naye masturbate au ku-ejaculate kwenye condom.

Huyo kama ni ndugu yangu au mtoto wangu, namwambia achague mwenyewe cha kufanya, ila akiomba ushauri kwangu nitamuambia akaitoe tena mapema.

Kwa nini ateseke na mimba asiyojua mhusika, mtoto asiyejua baba, kisu cha kutonesha jeraha na kumkumbusha machungu yaliyopita!
Na akiamua kuilea ni yeye na support nitampa hata kununua diapers za mtoto
 
Kutoa mimba ni uhalifu mkubwa pia kwa wanaoamini katika MUNGU hiyo ni dhambi ya mauaji kabisa,ushauri ni bora akavumilia akazaa maisha yaendelee na huwezi jua kuwa huyo mtoto akawa ndo mkombozi wako au wa jamii maana Kuna mifano mingi ya waliopatikana kwa mama zao kubakwa ambao kwa Sasa ni watu mhimu Sana miongoni mwao ni wachungaji,waimbaji na watu kibao maarufu(listi ninayo ukitaka).
 
kutoa siyo busara kwani huyo mtoto akizaliwa naye atambaka au? amlee tu mtoto atakuwa wake peke yake

Kama ni mwanaume anaweza kuja kubaka baadae na kama ni mwanamke anaweza kubakwa pia so ni lazima muhusika afanye maombi makali kuondoa laana
 
Ya sirini ni mengi ubakaji neno lililo kuzwa kiharakati na kisiasa kwa manufaa ya matumbo ya waharibu fikra za wanajamii kwa kukuza mambo.
 
Kwa hili la kubakwa,
mimi sijui wanaume wanao fanya hivyo wanachukuliaje? Hivi dada yake akifanyiwa hivyo atajisikiaje??
Napendekeza tuelimishe dada zetu kuwa, mtu akibakwa kuna mambo makuu mawili ya kufanya kwa haraka
1. Kwenda hospitali haraka ili kupata ushauri wa daktari, pamoja na kupatiwa dawa za Kuzuia UKIMWI, hii hutakiwa ifanyike mapema ndani ya masaa 48 (siku mbili)
2. Kule Hospitali pia muathirika ataweza kupatiwa dawa za kukinga mimba isishike kama Daktari akiona zinahitajika; Hii ni kama muathirika atawahi hosipitali ndani ya masaa 48 (siku mbili)

Mungu hapendi kabisa utoaji mimba hivyo naomba nisichangie hapo
Wabeja kolumba
 
Ubakaji ni kosa kisheria na adhabu zipo!

Ila, mtu anapoongozwa na HISIA au MIHEMKO katika maisha yake siku zote ataishi maisha ya tabu sana hususani kiakili.

Wapo waliotoa mimba na maisha yakazidi kuwa magumu zaidi, na wengine wakashindwa kupata tena ujauzito katika maisha yao.

Kuna msemo unasema; You Should Not Make Decisions When You're Emotional!

Ninachosema ni kuwa, katika maisha hupaswi kuongozwa na hisia ama mihemko katika kufanya maamuzi maana kuna uwezekano mkubwa wa kuyajutia maamuzi yale hapo baadaye.

Ndiyo maana kuna Wataalamu wa Saikolojia ambao kazi yao ni kutoa tiba ya Kisaikolojia kwa watu walioathirika kwa namna hiyo ili wasije kufanya maamuzi mengine yatakayohatarisha zaidi maisha yao ya baadaye.
Wapo pia waliotoa mimba na wakaishi vizuri tu na wanalea watoto, ni kitafuta njia salama tu ya kuitoa.
sijaona maamuzi ya muhemko wowote hapo, mtu kutoa mimba ambayo haikupangwa tena ya kubakwa ni reasonable, mtu yeyote ambaye hana hizi imani za kufikirika eti sijui mpango wa Mungu ataliunga mkono hili
 
Hamna kitu kibaya kama kumbukumbu hasa hiyo kumbukumbu inapokua mbaya katika maisha yako unaweza thubutu hata Kujitoa uhai hivi hivi

Hebu tuangalie huyu mdada mzuri sana alikua akitokea zake katika safari zake,ghafla njiani anavamiwa na kundi la wanaume walioshiba "wanam'baka wote, Kwa kupokezana kwa idadi ni kama wanaume 6 hivi, wanapomaliza ushetani wao wanaondoka wanamuacha yule dada pale, baada ya Muda yule dada anapata nguvu

Anainuka na kurudi zake nyumbani, kukaa baada ya mwezi anajigundua ni MJAMZITO na bila kufikiria mara mbili huu ujauzito ni wa mmoja ya wale wanaume waliom'baka

Mwanamke anaweza akaamua asiutoe huo ujauzito akautunza mpaka anajifungua, mtoto akakua kisha yule mtoto kila siku amuulize mama ake

"hivi mama baba yangu yuko wapi"? hivi hapa si ndio mwanamke atakumbuka alipopita huko? au mtu anatokea anamwambia yule mwanamke "mtoto wako atakua kafanana na baba yake huyoooo" hivi kwa maisha ya namna hii huyu mwanamke ataweza kweli kuishi kwa amani ktk maisha yake hapa duniani kweli angali kuna uwepo wa yule mtoto wake????

Kesi za namna hii zikinijiaga huwa nawambiaga tu "watoe hizo mimba aseeee" sijui nyie wenzangu kesi ya namna hii ikikufikia ukaambiwa mshauri yule mwanamke

Cha kufanya Kati ya kutunza Ujauzito au autoe ujauzito?
Nimesoma clip hii nikaiacha eti nisichangie chochote, lakini nikaona nafsi inanisuta tena sana. Hakuna thamani kubwa ya sisi binadamu mbele ya MUNGU kama HATUKUSAMEHE HAPA DUNIANI . Kwa sisi Wakristo Sala Kuu ya BABA YETU inajieleza wazi kwamba Mwenyezi Mungu atusamehe sisi ikiwa sisi tuliwasamehe wale walioteuliwa hapa duniani.
Niende kidogo kwenye mada. Kwanza niseme pole kwa huyu Dada kwa kubakwa kisha kupata ujauzito. Wabakaji wanadhambi yao na watahudumiwa kwayo. Dada huna dhambi katika kubakwa huko. Mtoto huyu ambaye yupo tumboni kwa Dada ni kiumbe kilichokubalika kuzaliwa na Mungu mwenyewe, kama sivyo hakika Mungu angekutwaa mbinguni ili kiumbe hicho kisizaliwe. Mungu amekuwa nguvu ikaibuka na kurudi nyumbani kisha baada ya mwezi ukajikuta umjamzito wa mmoja kati ya wabakaji. Kuna ujumbe Mungu anakupatia kwamba amethamini uhai wako wewe na mtoto wako. Hakika Mungu ni wa ajabu sana. Mtoto huyu atazaliwa na Mungu atampa Karama zake na kukuta anawapigania akina mama dhidi ya kubakwa, je hutastaajabu kuona hilo? Msamaha wako kwa wabakaji wako itakuwa ni faraja kwa mtoto wako na hakika utampenda. Kumsamehe kwako kwa dhati yule mbakaji aliyekuwa mtoto kutakupatia faraja ya kudumu na matumaini kwa Mungu kuwa hakika ATAKUSAMEHE kwa kuwa UMESAMEHE. Kamwe usitarajie kusamehewa na Mungu ikiwa hutasamehe iwe ni Mkristo au Muislamu.

Wito wangu kwa Dada nakuomba Dada yangu Mpendwa sana UHAI NI MALI YA MUNGU na ni YEYE PEKEE awezaye kuutoa ikawa ni halali LAKINI SI BINADAMU. Mpendwa mtoto wako mtarajiwa usimuue. Amri ya 5 ya Mungu inasema USIUE.
Ikiwa utasamehe kwa dhati tambua kuwa nawe UTASAMEHEWA dhambi zako na Mungu. Pope JOHN Paul II alipopigwa risasi na yule Mlebanon Mungu alimuokoa hakufa na alipopima aliiomba serikali ya Lebanon imwachie huru wakakataa., Pope alienda kumtembelea mfungwa yule gerezani huko nadhani alimtamkia rasmi kuwa alishamsamehe, ni furaha iliyoje yule mfungwa alijisikia. Leo hii tunavyoongea Pope John Paul II no Mtakatifu ( Kwa sisi Wakatoliki tunajua mchakato huu unamaana gani) Mungu akupe nguvu ya KUSAMEHE KWANI KUSAMEHE NI MATUMAINI YA UHAI MPYA NA MUNGU.
 
Back
Top Bottom