Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,832
- 18,827
Mwanamke akibakwa ana haki 200% za kutoa hiyo mimba,..... naona wengi mnakomaa kutoa mimba sio solution, hivi unaweza kuzaa huyo mtoto halafu uwe tayari kuishi na kovu kwenye akili yako miaka yako yote ya uhai hapa duniani kila ukimuona huyo mtoto?!
..... mnataka kusema mtu kubakwa ulikuwa ni mpango wa Mungu?, if yes, Mungu ni mbaya! kwanini Mungu asingempitisha njia nyingine ili asibakwe?
..... hilo janga likitokea kwa mtu wangu wa karibu namwambia ATOE serious, halafu amwambie Mungu nisamehe kwa kilichotokea.
unadhani akipatiwa Tiba kisaikolojia na mwana saikoloji bora dunia nzimaPamoja na hayo yote lakini;
Zoezi la utoaji mimba (Abortion) linapaswa kufanyika pale ambapo kiumbe kilichopo katika mfuko wa uzazi kitaleta madhara kiasi cha kuhatarisha maisha ya mjamzito husika.
Na hiyo ni baada ya kufanyika kwa vipimo vya kitabibu na Daktari/Madaktari kujiridhisha kuwa kuna ulazima huo, si kwa hisia tu za mjamzito mwenyewe bali vipimo.
Kwahiyo, ushauri bora zaidi nadhani ni wa kutunza huo ujauzito na huyo mtoto atakayezaliwa na pia mama wa mtoto huyo kupatiwa huduma maalumu ya kuituliza akili yake, namaanisha kuwa, apatiwe tiba ya kisaikolojia.
hata mimi huwa naamini hivyo,kuna mambo Mungu itabidi atuelewe tu kuwa ni magumu kwetumatatizo ya kisaikolojia ni mabaya sana, wakati mwingine inakupasa kufanya maamuzi magumu. naamini hata Mungu ataelewa tu aise.
unadhani mama atampenda yule mtoto kwa asilimia 100?Kutoa mimba siyo solushen, kila kiumbe kina haki ya kuishi no matter what. Kwani watoto wangapi wanalelewa na wababa wasio wakwao? Kuna masingomaza wangapi wanalea watoto wao wakati wanaume waliosababisha wapo na wanajulikana kabisa, tena bora kwa kesi hii mwanaume hajulikani. Kutoa mimba ni dhambi, sawa na kuua, tusihalalishe dhambi juu ya dhambi. Lakini pia kwanini ubake? Ni upungufu wa akili na maarifa
ulichokiandika mpk atokee mtu wa kuniaminisha tofauti na mawazo yako..... naona wengi mnakomaa kutoa mimba sio solution, hivi unaweza kuzaa huyo mtoto halafu uwe tayari kuishi na kovu kwenye akili yako miaka yako yote ya uhai hapa duniani kila ukimuona huyo mtoto?!
..... mnataka kusema mtu kubakwa ulikuwa ni mpango wa Mungu?, if yes, Mungu ni mbaya! kwanini Mungu asingempitisha njia nyingine ili asibakwe?
..... hilo janga likitokea kwa mtu wangu wa karibu namwambia ATOE serious, halafu amwambie Mungu nisamehe kwa kilichotokea.
Asante sanaFRANC THE GREAT Nani aliweka huo uamuzi? Serikali au Mungu?
Mimba kama mwanamke kabakwa ni haki yake 100% kuitoa, mwili ni wa kwake sio wa serikali, kuumia ataumia yeye na sio serikali
Huyo Mungu kama yupo na ana uwezo kweli basi angezuia huo ubakaji au hiyo mimba kutungwa
Ubakaji ni kosa kisheria na adhabu zipo!FRANC THE GREAT Nani aliweka huo uamuzi? Serikali au Mungu?
Mimba kama mwanamke kabakwa ni haki yake 100% kuitoa, mwili ni wa kwake sio wa serikali, kuumia ataumia yeye na sio serikali
Huyo Mungu kama yupo na ana uwezo kweli basi angezuia huo ubakaji au hiyo mimba kutungwa
Ndiyo maana kuna Professions kama Psychotherapists na Psychologists kwa ajili ya Cases kama hizo.unadhani akipatiwa Tiba kisaikolojia na mwana saikoloji bora dunia nzima
kitendo cha kumuona yule mtoto mbele yake,hakitomkumbusha wapi alipomtoa?
kitendo cha mtoto kumuuliza baba ake anafananaje,je hatokumbuka?
labda yawezekana kuna jinsi ya kusahaulisha mtu wa namna hiyo,siwezi kujua maana sio mwana saikoloji.
Hapana ukiliweka wazi hata wanasaikolojia watasaidia kuweka sawa kuliko kukiua kiumbe kisichokuwa na makosa.Mmmh Mungu atusamehe kuliko mateso ya maisha yote kila utapokuwa unamtazama yule mtoto ni heri ku*** tu
kutoa siyo busara kwani huyo mtoto akizaliwa naye atambaka au? amlee tu mtoto atakuwa wake peke yake
Wabeja kolumbaKwa hili la kubakwa,
mimi sijui wanaume wanao fanya hivyo wanachukuliaje? Hivi dada yake akifanyiwa hivyo atajisikiaje??
Napendekeza tuelimishe dada zetu kuwa, mtu akibakwa kuna mambo makuu mawili ya kufanya kwa haraka
1. Kwenda hospitali haraka ili kupata ushauri wa daktari, pamoja na kupatiwa dawa za Kuzuia UKIMWI, hii hutakiwa ifanyike mapema ndani ya masaa 48 (siku mbili)
2. Kule Hospitali pia muathirika ataweza kupatiwa dawa za kukinga mimba isishike kama Daktari akiona zinahitajika; Hii ni kama muathirika atawahi hosipitali ndani ya masaa 48 (siku mbili)
Mungu hapendi kabisa utoaji mimba hivyo naomba nisichangie hapo
Wapo pia waliotoa mimba na wakaishi vizuri tu na wanalea watoto, ni kitafuta njia salama tu ya kuitoa.Ubakaji ni kosa kisheria na adhabu zipo!
Ila, mtu anapoongozwa na HISIA au MIHEMKO katika maisha yake siku zote ataishi maisha ya tabu sana hususani kiakili.
Wapo waliotoa mimba na maisha yakazidi kuwa magumu zaidi, na wengine wakashindwa kupata tena ujauzito katika maisha yao.
Kuna msemo unasema; You Should Not Make Decisions When You're Emotional!
Ninachosema ni kuwa, katika maisha hupaswi kuongozwa na hisia ama mihemko katika kufanya maamuzi maana kuna uwezekano mkubwa wa kuyajutia maamuzi yale hapo baadaye.
Ndiyo maana kuna Wataalamu wa Saikolojia ambao kazi yao ni kutoa tiba ya Kisaikolojia kwa watu walioathirika kwa namna hiyo ili wasije kufanya maamuzi mengine yatakayohatarisha zaidi maisha yao ya baadaye.
Nimesoma clip hii nikaiacha eti nisichangie chochote, lakini nikaona nafsi inanisuta tena sana. Hakuna thamani kubwa ya sisi binadamu mbele ya MUNGU kama HATUKUSAMEHE HAPA DUNIANI . Kwa sisi Wakristo Sala Kuu ya BABA YETU inajieleza wazi kwamba Mwenyezi Mungu atusamehe sisi ikiwa sisi tuliwasamehe wale walioteuliwa hapa duniani.Hamna kitu kibaya kama kumbukumbu hasa hiyo kumbukumbu inapokua mbaya katika maisha yako unaweza thubutu hata Kujitoa uhai hivi hivi
Hebu tuangalie huyu mdada mzuri sana alikua akitokea zake katika safari zake,ghafla njiani anavamiwa na kundi la wanaume walioshiba "wanam'baka wote, Kwa kupokezana kwa idadi ni kama wanaume 6 hivi, wanapomaliza ushetani wao wanaondoka wanamuacha yule dada pale, baada ya Muda yule dada anapata nguvu
Anainuka na kurudi zake nyumbani, kukaa baada ya mwezi anajigundua ni MJAMZITO na bila kufikiria mara mbili huu ujauzito ni wa mmoja ya wale wanaume waliom'baka
Mwanamke anaweza akaamua asiutoe huo ujauzito akautunza mpaka anajifungua, mtoto akakua kisha yule mtoto kila siku amuulize mama ake
"hivi mama baba yangu yuko wapi"? hivi hapa si ndio mwanamke atakumbuka alipopita huko? au mtu anatokea anamwambia yule mwanamke "mtoto wako atakua kafanana na baba yake huyoooo" hivi kwa maisha ya namna hii huyu mwanamke ataweza kweli kuishi kwa amani ktk maisha yake hapa duniani kweli angali kuna uwepo wa yule mtoto wake????
Kesi za namna hii zikinijiaga huwa nawambiaga tu "watoe hizo mimba aseeee" sijui nyie wenzangu kesi ya namna hii ikikufikia ukaambiwa mshauri yule mwanamke
Cha kufanya Kati ya kutunza Ujauzito au autoe ujauzito?