Sifurahii kifo,lakini kwa hili channel ten ni funzo kwenu,kaeni chini mtafakali

Ruhazwe JR

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
3,403
920
Tukiwa kwenye majonzi juu ya mwenzetu aliyetolewa uhai na waporaji wa pumzi, ambao sisiti kuwaita watekaji wa demokrasia watumiwao na kundi la watu wachache wenye kujiharalishia madaraka kwa nguvu ya mtutu, mtutu ambao umenunuliwa kwa kodi ya sisi walala hoi,naona ni vema nirudi kwa upande wa Channel Ten.

Nimekua nikifatilia taarifa zao za hivi karibuni wanaonekana hawako kiuhalisia hasa pale linapokuja swala la uozo wa serikali.Mfano ni ile habari juu ya kifo cha Ally kilichosababishwa na Polisi mjini Morogoro.Walionekana kutoa taarifa kwa kuipendelea polisi na kuikandamiza CHADEMA,lakn siku si nyingi polisi wamepiga hodi kwao tena hodi ya kishindo.

Mimi sisiti kuwaambia na kuwashauri,wakae chini watafakari,kama kuna hongo walipokea kutoka CCM ili wawe wanapotosha kweli na kua ongo basi ni wakati wao hata hili la Iringa wapotoshe.Kama wamekua wakifanya vile kwa sababu ya woga basi wanapaswa waamke sasa nakuchukua hatua kwa vitendo.

Binafsi simjui mmiliki wa channel 10 lakin kama ni kigogo wa CCM nawashauri ndugu zetu wanaofanya kazi huko kuwa maisha ni popote,wakati wao umefika wakimbie mapema.

Narudia tena sifurahii kifo,ila kwa hili mnapaswa kukaa upya na kutafakari.
 
Madabhali Jnr kumbe Mkurya, rrrr kwenye llll. Hata hivyo hakuwa mwandishi huyo ni day waka mpiga picha wa mtaani. Nachukia mauaji.
 
huo ujumbe unatakiwa umfikie mtangazaji wa magic fm anayeitwa sebo.
 
huo ujumbe unatakiwa umfikie mtangazaji wa magic fm anayeitwa sebo.

iko siku na yeye chungu yetu tuliyonayo leo itahamia kwake ndipo atalia nakusaga meno,ingawaje nawaombea maisha marefu washuhudie watu wanavyochukua dora
 
Hakuna Chombo huru mpaka sasa Tz hata kimoja, Chombo huwa huru pale kinapoandika habari uipendayo! Cha msingi ni kulaani mauaji na wauaji, Muulize Jk atakwambia enzi zile za Mtandao Vyombo vyote vya Habari vilitongozeka kwake mpaka Msema kweli na Nyakati na kama vingekuwa demu ningesema kavipiga kwa condom moja bila kubadili,
 
sawa sawa tu naona sasa ukombozi unaelekea kutamu kwa hii style naamini sasa hawa policcm watakua hawana pakufichia uozo na hakuna wa kuwatetea tena hatua ya mwisho waue kiongozi mmoja wa juu kama dr slaa au mbowe au mnyika au lema au zito ndio mapambano yaanze rasmi. Hawawezi kutusumbua vichwa hawa polisi kwanza idadi yao ni kiduchu sana.tutaanza kuwapangia mikakati ya kuwapunguza idadi huku mitaani
 
Songoro umetumia maneno mazito,lakin niseme tu kwamba binafsi si kwamba ntakuwa na imani na chombo cha habari ambacho kitaandika habari niipendayo,hapana.Hoja yangu ni kuwa siku zote ni kazi kuibadili Ongo kuwa Kweli,watanzania sasa si kama wa enzi ile Tukidanganywa tunajua kwakua penye ukweli siku zote uongo unajitenga.haingi akili watu wasiokua na hata jiwe mkononi ukawatawanya kwa risasi ya moto,wengine hatuna elimu ya kutisha lakini tunajua taratibu za majesh kutawanya makundi,mpaka kuja kufikia hatua ya risas ya moto.Tatizo ni pale mwandishi,TV ama chombo chochote cha habar kujalibu kutuhadaa kuwa ukweli ni huu na si huu.JAMANI HATA TUSIPOSOMA PICHA INAONEKANA,mbona ITV wanajitahidi?
 
Last edited by a moderator:
huo ujumbe unatakiwa umfikie mtangazaji wa magic fm anayeitwa sebo.

Nimeshangaa kumsikia Kibonde kule kwenye Jahazi, jinsi alivyoudhiwa na mauaji ya Mwandishi mwenzake. Amesema kama yeye ndiye angekuwa Rais, RPC Kamuhanda angewekwa benchi kupisha uchunguzi na kama ikithibitika anahusika na tukio hilo, sheria ingechukua mkondo wake.
 
na yeye imeanza kumuingia eeh!...simtakii mabaya lakini matamani ile chungu yetu naye imkute
 
Last edited by a moderator:
Nimeshangaa kumsikia Kibonde kule kwenye Jahazi, jinsi alivyoudhiwa na mauaji ya Mwandishi mwenzake. Amesema kama yeye ndiye angekuwa Rais, RPC Kamuhanda angewekwa benchi kupisha uchunguzi na kama ikithibitika anahusika na tukio hilo, sheria ingechukua mkondo wake.

Mkuu, umenikumbusha huyo jamaa nilisahau kumtaja.
 
huo ujumbe unatakiwa umfikie mtangazaji wa magic fm anayeitwa sebo.

Umenikumbusha ndugu yangu kuhusu huyo mtu,mbona ana kiranga hivyo? Sebo ni kama limbukeni fulani hivi yeye anawaiga wafu FM,kimbelembele na anaboa. wewe sebo kama unanisikia au mfikishieni ujumbe kazi ya utangazaji haikufai
 
Hakuna Chombo huru mpaka sasa Tz hata kimoja, Chombo huwa huru pale kinapoandika habari uipendayo! Cha msingi ni kulaani mauaji na wauaji, Muulize Jk atakwambia enzi zile za Mtandao Vyombo vyote vya Habari vilitongozeka kwake mpaka Msema kweli na Nyakati na kama vingekuwa demu ningesema kavipiga kwa condom moja bila kubadili,

Wandishi wanahabari na nyie muache kimbelembele mkiona tukio tu tayari umbea ndio yanawakuta
 
Back
Top Bottom