Sifa za Waziri Mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sifa za Waziri Mkuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by We can, Nov 14, 2010.

 1. W

  We can JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mawaziri wote na ndiye Kiraanja Mkuu wa Kazi za kila siku za serikali, hivyo anapaswa awe:

  1. Mkali, asiyeonea na ambaye haonei mtu, watu, taasisi, nk,
  2. Asiwe fisadi, wala mtu aliyewahi kuwa fisadi ili kutoa dira/ mwongozo kwa mawaziri wake na kwa bosi wake,
  3. Hapaswi kuwa kimbelembele, kiherehere na mzandiki,
  4. Hapaswi kuwa mdini, mkabila, wala mbaguzi wa aina yeyote,
  5. Haswi kujali QUANTITY bali QUALITY ktk kazi; na aweke vigezo vya QUALITY. Sharti azingatie maelekezo ya wataalam (wasomi na tafiti zao). Ahakikishe ELIMU inapewa fungu kubwa kuwezesha wa Tanzania wafanye tafiti na siyo ku IMPORT wataalamu au KU IMPORT vifaa vya kitaalam, this should never be a long-term plan...
  6. Ajue kuwa Tanzania siyo nchi ya kuombaomba misaada,
  7. Atafakari upya na mara kwa mara kauli na sera za serikali; mfano is KILIMO kwanza a PRIME dira for Tanzania? au KILIMO BORA kwanza?
  8. Hapaswi kuwa na nyumba ndogo au yeye kuwa sehemu ya nyumba ndogo,
  9. Hapaswi kujali nani anamsifia au anamlaumu, alimradi anatenda kwa maslahi ya waliowengi,
  10. Anapaswa awe tayari kushirikiana na bosi wake kutimiza ahadi zooote wakati wa Kampeni.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Nov 14, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Awe mtu mwenye maamuzi kulingana na cheo alichonacho, bila kuathiri madaraka ya Mkuu wake.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Awe motto wa mkulima na awe na uwezo wa kulia linapokuja suala na mauaji ya albino
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Asiwe na nywele nyeupe.
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  awe ni mtu atakaye sema kwa dhati kuwa zanzibar si nchi..na akibanwa sana basi aite wanasheria wakuu wa serikali watafute definition ya zanzibar ni nchi au sio nchi
   
 6. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  awe anatoka katika familia ya Mkulima, anayeweza kujibu maswali ya pao kwa hapo, na anayemwogopa mkuu wake wa nchi
   
 7. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Asiwe ni mtu mwenye vijisenti, mwenye house girl wa kichina na mroho wa madaraka
   
 8. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Awe ni mtu ambaye alishauweka umaskini wake hadharani.
   
 9. c

  chelenje JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asiwe mwenye hasira ila busara...
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Nov 14, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Awe mwenye kufuga ng'ombe ikulu
   
 11. m

  matawi JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hivi ndivyo tunavyotaka lakini hachaguliwi kwakura za wananchi anachaguliwa na mafisadi ambao lazima wamwelekeze wanataka nini? so hapo nothing we can do mpaka tupate raisi wa kweli
   
 12. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  aweke maslahi ya nchi mbele ya chama baadae!
   
 13. Nyodo1

  Nyodo1 Member

  #13
  Nov 14, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Atambue kwamba Kilimo hakitoi umasikini, Nchi kwa kilimo ulimwenguni ni China na Marekani.. na ni nchi za viwanda... Kilimo hakitutoi, ajaribu kutambua Viwanda ndiyo njia pekee, Kwa kuanzia vidogo vidogo. Tunahitaji kuweza kujilisha tu, ila siyo uti wa mgongo wa maendeleo yetu.
   
 14. M

  Mtemakuni JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  awe anatambua kuna mungu ili aweze kumake fair and proper decisions otherwise moto utamhusu...!
   
 15. m

  mchakachuaji1 Senior Member

  #15
  Nov 14, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Utapata wapi viwanda bila kilimo. Punguza porojo mkuu.
   
 16. W

  We can JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimeona jina lako mkuu...tena No.1 kabisa!
   
Loading...