Sifa za mwanamke wa kweli mwenye 'moyo wa umama'

Halafu kwenye siri napo huwa napata utata.

Kuna watu vyumbani mwao utadhani wanaficha madawa ya kulevya, chumba cha wazazi ni siri, siri siri saaaaaaana.

Utaskia, weee, dada atachunguliaje chumbani kwako, hebu leo nijuzeni, kuna shida gani dada kuingia chumbani kwako???

hivi unapata utata gani? kwani wewe huna usiri? binafsi napenda sana usiri hasa kwenye mambo ya maendeleo ya nyumbani kwangu. sipend mtu ambaye mumewe akisafiri tu kesho unalikuta mtaani baba nanii kasafiri ama wamepanga kujenga unaskia kesho yake mtaani.

chumba kutokuzoewa ni heshima na usalama wa nyumba yako. mfano chumbani umeweka hati zako za nyumba magari vito na hata pesa kama mnamiliki silaha basi hata silaha ipo hapo. sasa je waweza kupaacha pawe ni mahali ambapo watu wanaingia hovyo kweli?

nina mfano wa rafiki yangu alikuwa anaacha chumba chake wazi huwez amini alikuta siku mdogo wake wa kiume amelala kwenye kitanda chake na binti wa kazi wanafanya ngono. it was shame aisee.
 
Wanawake wa DOT com, tunahitaji sana Mungu. Sijui ni kazi zinazotufanya kuto-deliver hata sehemu ambazo ni wajibu wetu. Dah! wanaume zetu spare us please. Mtuvumilie sana hali yenyewe ndo hiyo! lol
 
Sounds like mjakazi bora to me!

Yote uliyoyataja yanajadilika, especially lazima kiwango kiwepo. Uvumilivu kwa kiwango gani? Utiifu, heshima etc! What if mwanaume wako ni jambazi, abuser, womanizer etc. Utamtii tu hata akikuambia ficha mali hii ya wizi? Au muhudumie huyu dada nilimbaka?

Kaunga, loooooh!
 
Last edited by a moderator:
Blaine nafurah kuona unaelewa sasa, ila ngoja nikupe angalizo tusemapo awe na siri hatumaanish kwenye tatizo akae kimya la hasha ingawa haipendezi sana kusema matatizo ya ndani mwako mtaa kwa mtaa. Hapa tunamaanisha zile siri a nyumbani kwake hasa za mipango yao ya maendeleo furaha ya ndoa yao nayakufanana na hayo viwe siri ya ndani kwao.

kuna mwanamke mwigine akinunuliwa upi tu na mumewe kesho kapita hadi kwa shogaake kumweleza, ama wakipanga kujenga tu hata ajajua kiwanja atakipata wapi tayari liko mtaani siku hizi mwenzenu najenga unaona sasa mwanamke wa aina hii huwez kukaribisha roho za kauzibe kwenye familia manake anayatoa ya ndani nje kisha wapambe wanayadaka na kuyavalia nguo hadi kwenye gazet unayakuta.

Hivi kuna mtu hakuelewa concept ya siri katika familia??

Naomba jina lake ili nimwandikishe kwenye darasa langu la tuition/remedial!!

Babu DC!!
 
21. awe anapendwa kwenda viwanja na kumywa angalau bia 1 hadi 3 kla cku
22. awe mweupe kidogo na figure namba8
 
BADILI TABIA na gfsonwin

Pamoja na maelezo yenu mazuri ya siri za chumbani bado napata utata.

Off course kuna sittting room, so sitegemei watu kuja kupigia story chumbani kwangu, wakati huo huo nitaishije na watu wanaoweza niibia vitu vyangu valuable??? Kufikia kuishi na watu wanaoweza niibia hadi nifunge mlango, i consider myself a failure. Siwezi funga chumba kwa ajili hii, sababu sioni inawezaje kutokea kwa watu naoishi nao. Ataondoka mwizi na kuiacha nyumba.

Pia mdogo wangu kuingia na mwanamke kitandani kwangu?? tumetoka familia ya aina gani nii?? Kwanza mie ndugu anayeishi kwangu ataleta gf/bf ambaye wamefikia stage ya kwenda kujitambukisha home, hawea wa guest bubu hawawezi kanyaga kwangu. Siwezi kubali mdogo wangu leo analeta Hadija, kesho Ashura kesho Ana, tumetokea familia gani hiyo?? Sihitaji funga chumba kwa ajili hii.

Ndio, chumba panafanyika tendo takatifu, hata mie sitawaruhusu hawa kuingia chumbani wakati niko ndani na baba mwenye nyumba. Lakini ina maana by any means hawatakaa kuingia chumbani kwangu, sidhani wataingia ila watabisha hodi wakiwa wanataka kuingia. Kama sipo najua wanaingia huko wakiwa na shida maalaumu, sioni why waamue kwenda kuweka kijiwe chumbani kwangu.

Kuhusu kutoa taarifa za mambo ya nyumbani kwa majirani hizi ni tabia za familia, hazijengwi kwa kufunga chumba cha wazazi rather kwa kufundisha familia "ufamilia kwanza" kama ilivyo utaifa kwanza kwa mtanzania
Lazima ufunze familia yako kulinda interest za familia kwanza, sioni hii inahusu vipi kufunga chumba.

Kuna familia zingine mambo yao nje nje, lakini sehemu nuliyokulia mie huwezi kuta jambo la familia linapelekwa kwa jirani, hizi ni taratibu tu.

Mfano mama anafunga chumba lakini kutwa kucha vibarazani kwa majirani, anaongea nini kila siku? Ndio mwanzo wa kutapanya ya nyumbani kwake na watoto wanajifunza hapo hapo.

Anyway, huu ni mtazamo wangu wa 'siri' za familia, hiki kinajengwa kwenye vichwa vya wanafamilia.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin, inaelekea umeamua kuwa submissive so that the marriage could last. There are two sides of that decision....it depends on what is happening at a particular time
 
mie na wewe hatutofautiani kwa kweli.... Kanuni hizi naziacha jf, naishi niwezavyo....... Najitahidi kutimiza wajibu wangu ipasavyo................................ Though naona kadri uzee unavyokaribia uvumilivu nao unaongezeka loh.....(ingawa sijui kama ni uvumilivu au ni ili hali ya kutake things easy)

Hhahaahahahahahahahah,

Wengi wetu tunaamini kuwa ukiona rangi inaanza kubadilika ujue kuwa chakula kinaribia kuiva!! Kwa mtaji huo, na wewe unaukarimia umama bora...

Babu DC!!
 
asante madame....soon tutaiona imebebwa na kuwekwa facebook.........

Wanawake mna kazi eeeeh loh.....
Nadhani co vibaya wanajifunza na kama great thinkers utamwonyesha nai kama sio jamii na fb ikiwemo? tuache ubinafsi
hata wanaume ppia wanapeleka kule
 
Kongosho
dada kutoingia chumbani kwako sio siri ni heshima tu, wadogo zako wanaingia chumbani kwako?

Kiafrika afrika ndoa ni tendo takatifu, chumbani mnapofanyia tendo la ndoa pana heshima yake (ingawa mnaweza fanya hilo tendo hata jikoni) hivyo si busara wala heshima kuingia ingia hivyo...

Pili ni ulinzi tu wa mali zako, vyumbani humu wengine fedha huweka tu popote au valuables zao hivyo kuepuka kuibiwa (si unajua wasichana wa siku hizi ukimpata mzuri unashukuru)

tatu mabinti wa kileo hawa usipowafunza hivyo watataka hata vyupi wafuliwe na msichana, hivyo bora kuwafundisha kuwa chumbani hakupaswi kuingiwa hovyo, chumbani mke fanya usafi mwenyewe

Unaona sasa BADILI TABIA,

Haya mambo hayana kanuni na nadhani mleta mada katoa tu mawazo yake kutokana na uzoefu.....

Kwetu sie na Bibi, chumba chetu kinakuwa out of bound pale tu tunapokuwa nyumbani...Muda mwingine wowote wasichana wa kazi wanakifanyia usafi na kuingia kama sehemu nyingine ya nyumba!!

Na bado Bibi DC ni mwanamke wa kweli!!

Babu DC!!
 
mwanamke wa kweli mwenye moyo wa umama ametofautiana kwa kiasi kikubwa na mwanamke mwingine yeyote. mwanamke huyu awe amebarikiwa kupata watoto ama la lakin atakuwa na sifa zifuatazo.

1) ana upendo wa kweli kwa watu wa nyumbania mwake. yaani si mbaguzi hata kidogo. na daima huifanya familia yake kuwa priority. na kwamwe htumika kama daraja la kuunganisha familia zote mbili alikotoka yeye na aliakotoka mumewe.

2) ana hekima katika kuyakabili mambo ya nyumbani mwake. hata siku moja haamui mambo kwa ujinga na daima busara yake ndio silaha yake.

3) ana uvumilivu sana katika jambo lolote lile gumu na daima huona gumu lolote limpatalo kama changa moto tu na si kama kosa.

4) ana siri sana juu ya maisha ya nyumbani kwake daima hukuti mambo ya nyumbani nje watu wakiyajadili.

5) ni mchapa kazi hodari, tena ambaye hawez kuruhusu familia yake ikalala njaa kisa baba hajaleta chakula. ama watoto wasisome shule kisa baba hajalipa ada.

6) daima ni muaminifu na anaaminika sana kwa matendo yake.

7) siku zote huamka wa kwanza nyumban, na hulala wa mwisho. huakikisha mambo yote ya ndani yako sawa kabla ya yote.

8) huwa hadekezi watoto wala haengi watoto katika kazi. huakikisha nyumbani kwake kila mtoto ni mchapa kazi na nidham ya ndani ya nyumba ipo.

9) si mbishi wala hawez kubishana na mumewe mbele za watu. kwani ni msikivu sana kwa mumewe na daima humfanya mume kuwa kiongozi na kamwe huwa habadili cheo cha baba.

10) ni mwepesi wa kukiri makosa yake kwa mumewe na kuomba samahani lakin pia ni mzuri sana kwenye kuremedy makosa yake.

13) siku zote ni msafi wa mazingira na mwili daima nyumba yake husifika kwa usafi.

14) mume na watoto wake hujulikana hata wanapoonekana njian manake huakikisha amewavesha vizuri, kinadhifu na watoto wanaheshima sana.

15) ni mcha Mungu, kwa imani yake. hata kama baba si mtu wa sala lakin yeye huongoza watoto katika ibada kila iitwapo leo.

16) hupendelea zaid maendeleo hasa ya kiuchumi na daima hupenda vitu vizuri na hujitahd sana vipatikane.

17) si mpayukaji wala mtu wa kisirani nyumbani mwake. maneno yake huwa yaliyopangiliwa kwa sauti yenye kunyesha mamlaka lakini yenye upole.

18) hupendelea kupika na hujiskia furaha sana akipika kwa ajili ya familia yake. na siku akipika basi hata watoto husema leo tunakula chakula kitamu manake ni desturi yake kupika chakula kitamu.

19) humuheshimu sana mumewe, na daima hupenda kuisikia kauli ya mumewe katika maamuzi. siku zote humfanya baba kuwa msemaji wa familia yake na huakikisha kauli ya baba inatekelezwa.

20) kamwe huwa hana dharau, wala majivuno, wala kiburi, wala uchoyo wala unafiki kwa mtu yeyote yule.

nawasilisha
mwl gf.

Mithali 31......
 
BADILI TABIA na gfsonwin

Pamoja na maelezo yenu mazuri ya siri za chumbani bado napata utata.

Off course kuna sittting room, so sitegemei watu kuja kupigia story chumbani kwangu, wakati huo huo nitaishije na watu wanaoweza niibia vitu vyangu valuable??? Kufikia kuishi na watu wanaoweza niibia hadi nifunge mlango, i consider myself a failure. Siwezi funga chumba kwa ajili hii, sababu sioni inawezaje kutokea kwa watu naoishi nao. Ataondoka mwizi na kuiacha nyumba.

Pia mdogo wangu kuingia na mwanamke kitandani kwangu?? tumetoka familia ya aina gani nii?? Kwanza mie ndugu anayeishi kwangu ataleta gf/bf ambaye wamefikia stage ya kwenda kujitambukisha home, hawea wa guest bubu hawawezi kanyaga kwangu. Siwezi kubali mdogo wangu leo analeta Hadija, kesho Ashura kesho Ana, tumetokea familia gani hiyo?? Sihitaji funga chumba kwa ajili hii.

Ndio, chumba panafanyika tendo takatifu, hata mie sitawaruhusu hawa kuingia chumbani wakati niko ndani na baba mwenye nyumba. Lakini ina maana by any means hawatakaa kuingia chumbani kwangu, sidhani wataingia ila watabisha hodi wakiwa wanataka kuingia. Kama sipo najua wanaingia huko wakiwa na shida maalaumu, sioni why waamue kwenda kuweka kijiwe chumbani kwangu.

Kuhusu kutoa taarifa za mambo ya nyumbani kwa majirani hizi ni tabia za familia, hazijengwi kwa kufunga chumba cha wazazi rather kwa kufundisha familia "ufamilia kwanza" kama ilivyo utaifa kwanza kwa mtanzania
Lazima ufunze familia yako kulinda interest za familia kwanza, sioni hii inahusu vipi kufunga chumba.

Kuna familia zingine mambo yao nje nje, lakini sehemu nuliyokulia mie huwezi kuta jambo la familia linapelekwa kwa jirani, hizi ni taratibu tu.

Mfano mama anafunga chumba lakini kutwa kucha vibarazani kwa majirani, anaongea nini kila siku? Ndio mwanzo wa kutapanya ya nyumbani kwake na watoto wanajifunza hapo hapo.

Anyway, huu ni mtazamo wangu wa 'siri' za familia, hiki kinajengwa kwenye vichwa vya wanafamilia.

Ndiyo maana wewe ni dada mkuu....Hata kama kwenye hizo sifa za mdogo wangu gfsonwin umepata below....naamini hujapata namba ya kiatu na wewe ni kichwa cha kutisha (a.k.a jembe)!!

Babu DC
 
Last edited by a moderator:
Asante Babu Dark City

I thought kichwa changu kimekuwa 'corrupted' mahali

hata kwangu wanaingia nikiwa sipo, na bado najihisi nina amani tu.

Hata nikiwepo mama yao peke yangu kuna saa wanagonga na kuingia kuuliza wanachotaka na wanatoka.

Unaona sasa BADILI TABIA,

Haya mambo hayana kanuni na nadhani mleta mada katoa tu mawazo yake kutokana na uzoefu.....

Kwetu sie na Bibi, chumba chetu kinakuwa out of bound pale tu tunapokuwa nyumbani...Muda mwingine wowote wasichana wa kazi wanakifanyia usafi na kuingia kama sehemu nyingine ya nyumba!!

Na bado Bibi DC ni mwanamke wa kweli!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Mithali 31......

Sasa wewe Lilian Masilago, si ungecopy hii na kutuwekea hapa ili watu waone wenyewe??

Mithali 31

1 Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake.
2 Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu?
3 Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.
4 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?
5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.
6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.
8 Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu wote walioachwa peke yao;
9 Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; Uwapatie maskini na wahitaji haki yao.
10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
11 Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.
12 Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.
13 Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
14 Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.
16 Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.
18 Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.
19 Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.
20 Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21 Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22 Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23 Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
24 Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.
26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
28 Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,
29 Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.
30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.
31 Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin, inaelekea umeamua kuwa submissive so that the marriage could last. There are two sides of that decision....it depends on what is happening at a particular time
nafikiri kila mwenye ndoa ndivyo anavyowish kwamba ndoa yake idumu, hata hivyo haikupi nafasi ya kuonewa na kudharauliwa ila ninachokiona mm kwa experience yangu ni kwamba mwanaume yeyote yule hata kama ni mbaya sana huwa anaweza kubadilika kutokana na mke anavyomchukulia. na hili hufanya ndoa kudumu na kuish kwa amani.
 
Asante Babu Dark City

I thought kichwa changu kimekuwa 'corrupted' mahali

hata kwangu wanaingia nikiwa sipo, na bado najihisi nina amani tu.

Hata nikiwepo mama yao peke yangu kuna saa wanagonga na kuingia kuuliza wanachotaka na wanatoka.

Hakuna taabu Kongosho,

Kila nyumba ina taratibu zake ila kuna collection ya mambo ambayo yanafanyika katika nyumba nyingi na hayo ndiyo hutegeneza recipe kama hii aliyotuwekea gfsonwin.

Sidhani kama kuna wanawake wengi wanaoweza kufikisha hata 70%, ila ukweli utabaki hapo hapo kwamba kuna sifa ambazo mama bora anatakiwa kuwa nazo kama yule mama yao Juma na Roza wa kwenye vile vitabu vyetu vya zamani!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom