Sifa za mwanamke wa kweli mwenye 'moyo wa umama'

BT usipolala wa mwisho na kuamka wa kwanza wewe ni kakiwanda tu kakufyatua watoto na so mama bora!

maana yake si kwamba atakuwa siyo mama bora bali atakua amepunguza sifa za mama bora, kwani wafikiri kwanini anaamka wa kwanza na kulala wa mwisho? huamka ili kuhakikisha kwamba ata uji anaopika dada umefuata taratibu zake, na hulala wa mwisho ili ahakikishe mambo yotekabla ya kulala yamekwenda sawa hata kama kuna mtu anayeyafanya ila usimamizi na uhakiki wake ni lazima.

unless uwe ni mtu usinayependa kufanyiwa kazi ila kama wapenda kuwajiabika basi lazima kabla ya kulala na kabla ya kuamka kuyaangalia haya.
 
Ofcourse kama akina mama wangefuata haya na akina baba wakafuata ya kule kwenye sifa za mume bora neno talaka lisingefahamika. Maisha haya bora liende tu.
 
Sasa gfsonwin, kama mume anatongoza wadada JF au anaangalia Chelsea nimsubiri ili iwe mtu wa mwisho kulala???

Bwana hakuna ABCD kihivyo, cha msingi ni kuweka maslahi ya watoto lkn usisahau nawe kuishi. Tena wewe umekuwa muhubiri mzuri wa kujipa raha mwenyewe, lkn kama hivyo ulivyo outline vinakupa raha ni safi pia!
 
Last edited by a moderator:
Kaunga kwa kabdri ya maelezo yake hapo juu...Nahisi atakuwa ni msichana..

Mtoa thread hii ameelezea sifa za mwanamke mwema na bora.

Ahsante Mwl gf.

My son, asema hata apewe bank hawezi change mama hata kwa 24 hrs tu! Na opinion ya mwanangu incount kwangu kuliko the whole world leave alone you!
 
Sasa gfsonwin, kama mume anatongoza wadada JF au anaangalia Chelsea nimsubiri ili iwe mtu wa mwisho kulala???

Bwana hakuna ABCD kihivyo, cha msingi ni kuweka maslahi ya watoto lkn usisahau nawe kuishi. Tena wewe umekuwa muhubiri mzuri wa kujipa raha mwenyewe, lkn kama hivyo ulivyo outline vinakupa raha ni safi pia!

yaani Kaunga kuna kitu ambacho nafikir hatuelewani mimi haya niliyoyasema ni kwamba kwa ujumla ndizzo sifa za mama bora ila sasa inapokuja swala la mtu binafsi panakuwepo na tofauti.

labda niseme mume anangalia mechi definately hataka utalala but akirud utaamka kumfungulia mlango na kumpa menu na ni ukweli akishakula yeye lazima atatangulia kitandani kabla yako manake lazima ufute meza urudishe vyombo jikon so mpaka hapo umeshakuwa wa mwisho tu.
 
Last edited by a moderator:
Ofcourse kama akina mama wangefuata haya na akina baba wakafuata ya kule kwenye sifa za mume bora neno talaka lisingefahamika. Maisha haya bora liende tu.

unajua hapa ndio maana tunafundishana ili mwisho wa siku kila mtu ajue nini wajibu wake. tukiacha ujuaji na kujizidishia haki kisha kila mtu akatimiza ampasayo hakika dunian pangekuwa pazuri sana hasa kwa habari ya maisha ya ndoa.
 
Hongera sana gfsonwin kwa kutimiza ahadi yetu!

Kusema kweli huu uzi ni mzuri sana. Ngoja nitafute muda na nijipange kutoa maoni yangu!!

Babu DC!!
 
Mitazamo itofauti, naomba tukubali kutofautiana!
Na wanaume wako tofauti pia, nakumbuka nilishatoa ushuhuda wa mzazi mwenzangu ambaye yeye hapendi kufanyiwa kila kitu na mwanamke kwa kuwa 'si kilema' hayo ni maneno yake.

Nina uhakika kuna wanaume ambao wana ufunguo kiasi kwamba akija late anaingia ndani na kupasha msosi kwenye microwave na kula kisha humjoin mkewe kitandani. Mke ambaye amelala saa Saba baada ya kuchoka then aamshwe saa nane na nusu kumfungulia baba aliyekuwa anaangalia mechi (@Dark City sijui na hii ni sifa ya mwanaume wa kiafrika).

Anyway silazimishi mtazamo wangu, lkn kuwa mama bora ni pamoja na kuwa binadamu bora; na hii ni very contextual!
 
mwanamke wa kweli mwenye moyo wa umama ametofautiana kwa kiasi kikubwa na mwanamke mwingine yeyote. mwanamke huyu awe amebarikiwa kupata watoto ama la lakin atakuwa na sifa zifuatazo.

1) ana upendo wa kweli kwa watu wa nyumbania mwake. yaani si mbaguzi hata kidogo. na daima huifanya familia yake kuwa priority. na kwamwe htumika kama daraja la kuunganisha familia zote mbili alikotoka yeye na aliakotoka mumewe. 100/100

2) ana hekima katika kuyakabili mambo ya nyumbani mwake. hata siku moja haamui mambo kwa ujinga na daima busara yake ndio silaha yake. 100/100

3) ana uvumilivu sana katika jambo lolote lile gumu na daima huona gumu lolote limpatalo kama changa moto tu na si kama kosa. 80/100 aangalie asije kuwa na upendo wa mshumaa, kumbuka kila mtu ana breaking point na kuna mambo yasiyovumilika (abuse. infidelity etc) siwezi kushauri mdada abaki kwenye ndoa ya mateso kwa kigezo cha uvumilivu. natumaini umewahi ona/soma stori za gender based violence.

4) ana siri sana juu ya maisha ya nyumbani kwake daima hukuti mambo ya nyumbani nje watu wakiyajadili. 80/100 too much secrecy hurts na kuomba external help sio udhaifu. kama una tatizo kubwa kwenye familia kubaki nalo moyoni si solution, omba msaada/ushauri na kupata ushauri mzuri ambao hukuweza kufikiria mwenyewe.

5) ni mchapa kazi hodari, tena ambaye hawez kuruhusu familia yake ikalala njaa kisa baba hajaleta chakula. ama watoto wasisome shule kisa baba hajalipa ada.110/100

6) daima ni muaminifu na anaaminika sana kwa matendo yake. 100/100

7) siku zote huamka wa kwanza nyumban, na hulala wa mwisho. huakikisha mambo yote ya ndani yako sawa kabla ya yote. 80/100 yeye pia ni binadamu sio robot. Dark City alisema mwanaume ndio wa mwisho kulala maana inabidi acheki usalama nyumbani kwake

8) huwa hadekezi watoto wala haengi watoto katika kazi. huakikisha nyumbani kwake kila mtoto ni mchapa kazi na nidham ya ndani ya nyumba ipo. 100/100

9) si mbishi wala hawez kubishana na mumewe mbele za watu. kwani ni msikivu sana kwa mumewe na daima humfanya mume kuwa kiongozi na kamwe huwa habadili cheo cha baba. 90/100, hii ni kweli kama baba atakuwa na sifa husika, mama usikae kimya ukiona mumeo kakosea

10) ni mwepesi wa kukiri makosa yake kwa mumewe na kuomba samahani lakin pia ni mzuri sana kwenye kuremedy makosa yake. 100/100

13) siku zote ni msafi wa mazingira na mwili daima nyumba yake husifika kwa usafi. 110/100

14) mume na watoto wake hujulikana hata wanapoonekana njian manake huakikisha amewavesha vizuri, kinadhifu na watoto wanaheshima sana. 100/100

15) ni mcha Mungu, kwa imani yake. hata kama baba si mtu wa sala lakin yeye huongoza watoto katika ibada kila iitwapo leo. 100/100,

16) hupendelea zaid maendeleo hasa ya kiuchumi na daima hupenda vitu vizuri na hujitahd sana vipatikane. 100/100

17) si mpayukaji wala mtu wa kisirani nyumbani mwake. maneno yake huwa yaliyopangiliwa kwa sauti yenye kunyesha mamlaka lakini yenye upole. 90/100, sometimes a firm hand is needed. imagine mwanao anavuta sigara utatumia sauti ya upole?

18) hupendelea kupika na hujiskia furaha sana akipika kwa ajili ya familia yake. na siku akipika basi hata watoto husema leo tunakula chakula kitamu manake ni desturi yake kupika chakula kitamu. 90/100,

19) humuheshimu sana mumewe, na daima hupenda kuisikia kauli ya mumewe katika maamuzi. siku zote humfanya baba kuwa msemaji wa familia yake na huakikisha kauli ya baba inatekelezwa. 90/100, refer to (9) above

20) kamwe huwa hana dharau, wala majivuno, wala kiburi, wala uchoyo wala unafiki kwa mtu yeyote yule. 100/100

nawasilisha
mwl gf.

comments in blue, based on my experience growing up

EDIT: napendekeza mod aiweke hii thread kwenye sticky

Mtoa mada ameeleza vizuri sana sifa ya mwanamke bora,ukikuta mengi yaliyoandikwa yanakuuma na huyawezi basi ujue wewe si mwanamke bora ambaye anazungumziwa hivyo ukae kimya.Na kama umeolewa lazima ndoa yako ni shida sana wala haina furaha ndio maana unatafuta kila aina ya defending mechanism uonekane unayoyafanya ni sahihi lakini bahati mbaya unaeumia zaidi ni wewe mwenyewe just bcoz huna hekima wala busara hat kuchagua mume ulishindwa.Ila kam hujaolewa bado ujue utakesha sana labda kwa msaada wa waganga.Ninamheshimu sana sana mke wangu maana sifa zake hata ulizoandika juu naona hazitoshi bado.Ndoa yangu ina miaka minne huu wa tano lakini utadhani tupo kwenye fungate maana nimemfanya zaidi ya mke but my only best friend i believe most.Ndoa ina raha bwana poleni mnaolia.
 
BT usipolala wa mwisho na kuamka wa kwanza wewe ni kakiwanda tu kakufyatua watoto na so mama bora!

ndo maana nikasema uanamke kazi sana aisee....
Mie sifanyi zaidi ya uwezo wangu,
kama nimeshindwa naacha, mwenzangu anisaidie si ndo umuhimu wa kuwa wawili?

Iam a human being, natumia damu akhuuuu
 
Mitazamo itofauti, naomba tukubali kutofautiana!
Na wanaume wako tofauti pia, nakumbuka nilishatoa ushuhuda wa mzazi mwenzangu ambaye yeye hapendi kufanyiwa kila kitu na mwanamke kwa kuwa 'si kilema' hayo ni maneno yake.

Nina uhakika kuna wanaume ambao wana ufunguo kiasi kwamba akija late anaingia ndani na kupasha msosi kwenye microwave na kula kisha humjoin mkewe kitandani. Mke ambaye amelala saa Saba baada ya kuchoka then aamshwe saa nane na nusu kumfungulia baba aliyekuwa anaangalia mechi (@Dark City sijui na hii ni sifa ya mwanaume wa kiafrika).

Anyway silazimishi mtazamo wangu, lkn kuwa mama bora ni pamoja na kuwa binadamu bora; na hii ni very contextual!

samahani,
unasema mtu arudi saa nane usiku uamke kumfungulia mlango?
Kwanza kwa nini arudi saa nane.....
Kama ni kwa sababu ya man u na barcelona sijui asahau tu.....

Ila pamoja na yooooooote watu wanasahau kila mtu ana style yake ya maisha, kila couple ina namna yao ya kuishi................

Na vya kuambiwa unachanganya na vya kwako.....
 
unajua hapa ndio maana tunafundishana ili mwisho wa siku kila mtu ajue nini wajibu wake. tukiacha ujuaji na kujizidishia haki kisha kila mtu akatimiza ampasayo hakika dunian pangekuwa pazuri sana hasa kwa habari ya maisha ya ndoa.

Haya maisha haya bora liende tu. Mara nyingine huwa naona huu usemi wa 'wazazi walikuwa zamani, sasa bongo flavour tu'.
Ushawahi sikia novel inayoitwa 'men are from mars, women are from venus'? Hopeful novel ile ina majibu mengi na mazuri. We should learn to enjoy our differences badala ya hizo tofauti kuwa threats. Lazima tukumbuke kuwa men walikuwa mars, wakachukua darubini, wakawaona wanawake venus, then wakaja duniani na kusahau kuwa walikutana all na tofauti kibao.
 
Ni sifa nzuri hizo, kulingana na wakati, mtu(mwanaume/mume) uliye naye, na mazingira mliyonayo kwa wakati huo.
Maisha ya kanuni sanaaaaa, na sheria kama hesabu za quadratic equations mi siyawezi. Nature tu iamue Mambo. Basiiiiii....Niwe mtu wakujua na kutimiza wajibu wangu Basi. Makanuni Makanuni mi naona siyawezi.
 
samahani,
unasema mtu arudi saa nane usiku uamke kumfungulia mlango?
Kwanza kwa nini arudi saa nane.....
Kama ni kwa sababu ya man u na barcelona sijui asahau tu.....

Ila pamoja na yooooooote watu wanasahau kila mtu ana styke yake ya maisha, kila couple ina namna yao ya kuishi................

Na vya kuambiwa unachanganya na vya kwako.....

Kwa kweli BADILI TABIA haya maisha yanatofautiana sana.....kila mtu na hulka yake, style yake na namna yake. Maisha sio PAI wala kanuni ya kutafuta eneo la Duara. Ni vile tu yalivyo kutokana na wakati na mazingira.
 
Last edited by a moderator:
Sasa gfsonwin, kama mume anatongoza wadada JF au anaangalia Chelsea nimsubiri ili iwe mtu wa mwisho kulala???

Bwana hakuna ABCD kihivyo, cha msingi ni kuweka maslahi ya watoto lkn usisahau nawe kuishi. Tena wewe umekuwa muhubiri mzuri wa kujipa raha mwenyewe, lkn kama hivyo ulivyo outline vinakupa raha ni safi pia!

Mdogo wangu Kaunga,

Hakuna mechi za Chelse, Man U au Barca ambazo zinachezwa kila siku....Kama huyo mwanamume anachelewa kurudi kila siku (au mara kwa mara) na kusingizia mechi, basi mke wake anatakiwa kuwa mbayu wayu!!

Kuhusu JF na chit chat, mwanamume wa kweli ninayemfahamu mimi hawezi kufanya upuuzi kama huo mbele ya mke wake...Atachit chat kutwa mzima ila akifika home anageuka angel.....Huyo ndiye mwanamume wa kweli tunayemwongelea hapa kila mara....Lazima aheshimu mke wake na kumpa first priority hata kama anachepuka once in a while (wale wasiotaka kuona hii kitu wasisome hapa)!!

Kwa hiyo, kama baba anaangalia mechi (kama ambavyo mama anaweza kuwa anaangalia movie), sidhani kama mama atazuiliwa kwenda kulala!! Ila, kitendo cha mama kukimbilia chumbani kulala wakati nyumba yake iko out of order, kitaleta mashaka juu ya uwezo wake wa ku-manage nyumba kama mama bora na mke mwema!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom