Sifa za mwanamke wa kweli mwenye 'moyo wa umama' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sifa za mwanamke wa kweli mwenye 'moyo wa umama'

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by gfsonwin, Aug 27, 2012.

 1. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  mwanamke wa kweli mwenye moyo wa umama ametofautiana kwa kiasi kikubwa na mwanamke mwingine yeyote. mwanamke huyu awe amebarikiwa kupata watoto ama la lakin atakuwa na sifa zifuatazo.

  1) ana upendo wa kweli kwa watu wa nyumbania mwake. yaani si mbaguzi hata kidogo. na daima huifanya familia yake kuwa priority. na kwamwe htumika kama daraja la kuunganisha familia zote mbili alikotoka yeye na aliakotoka mumewe.

  2) ana hekima katika kuyakabili mambo ya nyumbani mwake. hata siku moja haamui mambo kwa ujinga na daima busara yake ndio silaha yake.

  3) ana uvumilivu sana katika jambo lolote lile gumu na daima huona gumu lolote limpatalo kama changa moto tu na si kama kosa.

  4) ana siri sana juu ya maisha ya nyumbani kwake daima hukuti mambo ya nyumbani nje watu wakiyajadili.

  5) ni mchapa kazi hodari, tena ambaye hawez kuruhusu familia yake ikalala njaa kisa baba hajaleta chakula. ama watoto wasisome shule kisa baba hajalipa ada.

  6) daima ni muaminifu na anaaminika sana kwa matendo yake.

  7) siku zote huamka wa kwanza nyumban, na hulala wa mwisho. huakikisha mambo yote ya ndani yako sawa kabla ya yote.

  8) huwa hadekezi watoto wala haengi watoto katika kazi. huakikisha nyumbani kwake kila mtoto ni mchapa kazi na nidham ya ndani ya nyumba ipo.

  9) si mbishi wala hawez kubishana na mumewe mbele za watu. kwani ni msikivu sana kwa mumewe na daima humfanya mume kuwa kiongozi na kamwe huwa habadili cheo cha baba.

  10) ni mwepesi wa kukiri makosa yake kwa mumewe na kuomba samahani lakin pia ni mzuri sana kwenye kuremedy makosa yake.

  13) siku zote ni msafi wa mazingira na mwili daima nyumba yake husifika kwa usafi.

  14) mume na watoto wake hujulikana hata wanapoonekana njian manake huakikisha amewavesha vizuri, kinadhifu na watoto wanaheshima sana.

  15) ni mcha Mungu, kwa imani yake. hata kama baba si mtu wa sala lakin yeye huongoza watoto katika ibada kila iitwapo leo.

  16) hupendelea zaid maendeleo hasa ya kiuchumi na daima hupenda vitu vizuri na hujitahd sana vipatikane.

  17) si mpayukaji wala mtu wa kisirani nyumbani mwake. maneno yake huwa yaliyopangiliwa kwa sauti yenye kunyesha mamlaka lakini yenye upole.

  18) hupendelea kupika na hujiskia furaha sana akipika kwa ajili ya familia yake. na siku akipika basi hata watoto husema leo tunakula chakula kitamu manake ni desturi yake kupika chakula kitamu.

  19) humuheshimu sana mumewe, na daima hupenda kuisikia kauli ya mumewe katika maamuzi. siku zote humfanya baba kuwa msemaji wa familia yake na huakikisha kauli ya baba inatekelezwa.

  20) kamwe huwa hana dharau, wala majivuno, wala kiburi, wala uchoyo wala unafiki kwa mtu yeyote yule.

  nawasilisha
  mwl gf.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  hapo namba 7 na 18, pamenifanya niwe mume bora lol

  ni nzuri.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  asante madame....soon tutaiona imebebwa na kuwekwa facebook.........

  Wanawake mna kazi eeeeh loh.....
   
 4. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  mmh! mwanamke bora huyawah mapambazuko my dear, jitahd utaweza kuamka mapema na kulala wa mwisho. pia mama hulisha wanawe ngano alokanda yeye. lakin naona kama unaongopa.
   
 5. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  vizuri sana mwalimu gfsonwin. ntakuja kutoa comments nkifika ofisini hasa hapo 3 & 4.

  wewe ni mwanamama, sasa iweje useme hivi? naomba maelezo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  mbona wewe unajitoa kundini sio mwanamke kwani? hivi kumbe huwa wanaiba ma post kutoka huku kwa GTs?
   
 7. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  karibu tena Blaine. Kongosho ni mwanamama ila kasema ivyo kwasababu anafikiri yuko weak kwenye vipengele hivyo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Sounds like mjakazi bora to me!

  Yote uliyoyataja yanajadilika, especially lazima kiwango kiwepo. Uvumilivu kwa kiwango gani? Utiifu, heshima etc! What if mwanaume wako ni jambazi, abuser, womanizer etc. Utamtii tu hata akikuambia ficha mali hii ya wizi? Au muhudumie huyu dada nilimbaka?
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  kama ulikuwepo lol


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  ndio hivyo, sio mmama, bora niendeleze ubaba tu

   
 11. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Kaunga umesahau kwamba mwanamke yeyote kwanza mwenye busara hata maamuzi ya nani awe mume wangu hakurupuki kwa vigezo vya nje. huwa anamsoma mtu na kujua kazi yake nk pia inapotokea kama kaolewa na mtu korofi like abuser or womanizer bado anaweza kuvumilia while praying hadi apate njia ya kutokea.

  ukweli ni kwamba na hili tusilipinge mwanamke mwenye roho ama moyo wa umama hata kwenye vitabu vya dini bado anaonekana kuwa subordinated tu. and this is the nature we cant deny it.

  sikatai utatakiwa kumshinda mumeo kwa hoja na si kwa kubishana nae mbele za watu ama kumfanyia jeuri.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,292
  Likes Received: 22,062
  Trophy Points: 280
  Sifa zote hizi anazo mke wangu mpenzi @da mie
   
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  hongera sana mkuu.
   
 14. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Ninaweza kuhighlight hekima na busara; hivyo vyote vinaweza kimlead mwanamke ktk kuwa mama bora, mke bora na bado assijikatalie nafsi yake (kwa kuwa mtumwa au less human).

  Mambo mengine ni usafi, upendo na uwezo wa kuomgoza familia sina shida nayo!

  Nikirudi kuhusu point yangu ya awali, juu ya busara (which is also contextual au inategemea na mtizamo wa huyo muhusika), sidhani (according to me) kama ni busara kuvumilia mwanaume kitombi while unajua risk ya magonjwa ilivyo (na usiniambie walioathirika kwa style hii walikuwa hawasali). So busara yangu mimi ambayo ni tofauti na yako ni kupack my things na kuondoka na watoto wangu!
   
 15. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  kaunga wewe upo ndani ya ndoa..............................?
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  ndio huwa wanaiba......

  Ila namba 7 mmmh na namba 18 nikichoka sipiki mie aiiiii........

  Sijui ndo sina sifa loh
   
 17. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Nimeamua nisijibu hilo swali; kama kuna point unataka kumake just air it!
   
 18. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  BT usipolala wa mwisho na kuamka wa kwanza wewe ni kakiwanda tu kakufyatua watoto na so mama bora!
   
 19. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  hizo points zilinihitaji nijue umesimama upande upi,

  yumkini ningekuwa katika nafasi kubwa ya kupeana uzoefu na wewe...........

  usijali lakini............................
   
 20. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  sasa umeona Kaunga kwamba wewe uko tayari kuitetea familia yako kwa gharama yeyote ile? kwamba utaondoka na wanao je wajua kwamba iyo ndo moja ya sifa ya umama? manake siku zote mama ndio mtetez wa wanae na ndo maana hata acha watoto wasisome eti kisa baba hayuko responsible. huwa anahangaika awe yuko ndani ama ametoka na wanawe na kwamwe hawaahi wanawe nyuma.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...