Sifa za maafisa ubalozi wetu ni zipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sifa za maafisa ubalozi wetu ni zipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Annina, Jan 25, 2010.

 1. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa wale waliobahatika kufika katika ofisi za balozi zetu katika nchi mbalimbali watakubaliana nami kwamba hali inasikitisha. Pamoja na uchache wa maafisa, uwezo wao kitaaluma pia ni wa kutilia shaka. Nchi karibu zote sasa zimeachana na political diplomat na kujiunga na economic diplomat, hii ina maana maafisa ubalozi wanatakiwa kuwa na uelewa wa hali ya juu katika masuala ya biashara na uchumi katika ngazi ya kimataifa. Kweli Tanzania haina watu makini katika fani hii wanaoweza kutumika huko? Hatuhitaji timu kubwa ubalozini ili kufanikisha agenda (kama tuna agenda), tunahitaji watu wenye sifa za kuwa huko. Nchi nyingine nafasi za ubalozi wanapewa watu wenye uwezo wa hali ya juu, mfano Korea huwezi kuwa diplomat mpaka ufikie viwango vilivyowekwa ikiwa ni pamoja na kufanya mitihani na kuandika mada mbalimbali za kiuchumi, mwisho wa siku wanapeleka watu wenye sifa ili kutetea agenda yao. Naomba anaejua sifa za diplomats wa Tanzania (hata kama hazifuatwi) anijulishe. Asante sana,Annina
   
 2. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Sifa kubwa uwe mtoto wa Mafisadi na mwanachama wa Chama Cha Majambazi, baba yako au ankal awe kwenye nafasi kwenye Chama cha Majambazi. Uwalambe miguu watawala. Uwe na undugu hata wa mbali kwa viongozi wa Chama Cha Majambazi.

  Ukibahatika upate ukiwa nje ya hiyo criteria hutakaa zaidi ya miongo miwili.

  Sasa kama unabisha tutaanza kuwaweka majina hapa kuanzia kwenye balozi zetu zote halafu uone. Yaani who is who in our foreign missions.
   
 3. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Asante sana Wacha1, najua kuna uwezekano huo hasa kama hakuna sifa zilizoainishwa kwa nafasi hizo, ndio maana nauliza kama kuna anaejua vigezo atujulishe ili tusihukumu maana mtu anaweza kuwa mtoto wa mkubwa lakini ana sifa zinazostahili.


  Asante sana,


  Annina
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Wengi wao planted wa usalama hata videzo vinakuwa siri.....kujuana tu kunatawala....ila wengi wanajitahidi kujisomesha somesha zaidi wakiwa nje!!
   
 5. M

  Mende dume Member

  #5
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  we never had an agenda for years!

  kila kitu is either MDG, EFA, MKUKUTA ambazo ni za UN, UNESCO na WB respectively.

  Kweli we are either way fucked!
   
 6. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Kama vile kusipokuwepo na sifa za mtu kuwa usalama wa taifa wala ajira kutangazwa, vivyo hivyo na hawa mabalozi hawana sifa maalumu inayotambulikana kisheria. Hata house girl wa mkubwa unaweza zawadiwa ubalozi katika nchi fulani.
   
 7. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Natamani watu wangejua yanayoendelea huko, labda hatua za makususdi zingechukuliwa! Kuna usiri gani katika vigezo? Mbona FBI na CIA wameweka vigezo wazi na nafasi zinatangazwa kwa web zao?

  Annina
   
Loading...