Sifa za kugombea ubunge zibadilishwe walau mgombea awe na elimu ya shahada

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
1,506
2,000
Habari za leo ndugu zangu,
Uzi wangu leo utakua mfupi sana.

Ni ushauri tu sifa za kugombea ubunge zibadirishwe walau mgombea awe na Shahada.

Na wanaogombea udiwani walau wawe na diploma.

Wanaogombea uenyekiti wa vijiji walau wawe na cheti cha form four.

Ndugu zangu ni ushauri tu.

Ninyi mnaonaje wakuu.
 
Raynavero

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
38,481
2,000
Hao wasomi wana tija gani ktk nchi?!!zaidi ya kuwa mafisadi na kujikomba ngazi za juu tubaki hvyo hvyo ili kila mtu awe na haki sawa
 
engida

Member
Apr 22, 2021
8
45
Hao wasomi wana tija gani ktk nchi?!!zaidi ya kuwa mafisadi na kujikomba ngazi za juu tubaki hvyo hvyo ili kila mtu awe na haki sawa
Tuseme ukweli, jamani dunia nzima inaongozwa na ELIMU. Namnukuu Mahatma Ghandi (Mwanaphilosophia nguli ktk Menejimenti) 'Ili uwe kua kiongozi bora, ni lazima kiongozi uwe muelewa kuliko wale unaowaongoza'. Hapa Tanzania ni kinyume chake. Kwa kweli haya ya kukataa elimu (Sayansi), ni mawazo yanayotawaliwa na hao ambao kwa bahati mbaya hawajapata nafasi ya kuingia madarasani kama mkakati wa ushindi katika siasa. Bado haingii akilini tunapomchagua darasa la saba kwenda kututungia sheria za biashara za kimataifa, huku unamkataa Daktari mbobezi katika biashara za kimataifa. TUAMKENI, TUBADILIKE!!!!
 
Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
8,120
2,000
Habari za leo ndugu zangu,
Uzi wangu leo utakua mfupi sana.

Ni ushauri tu sifa za kugombea ubunge zibadirishwe walau mgombea awe na Shahada.

Na wanaogombea udiwani walau wawe na diploma.

Wanaogombea uenyekiti wa vijiji walau wawe na cheti cha form four.

Ndugu zangu ni ushauri tu.

Ninyi mnaonaje wakuu.
Kwani Musukuma, Lusinde, Jah People na Kinanasi wao wanasemaje?
 
simon2016

JF-Expert Member
Oct 19, 2020
299
1,000
Ujinga tuu umekujaaa kwani hilo bunge ni la wasomi hilo ni la kila mtu unaweza ukawa na elimu halafu huna akili kikubwa hakuna limitation yeyote anaweza kutetea wenzake azame mule .

Hivi ungekua hujasoma hlf unasikia kuingia bungeni mpaka uwe umesoma unajisikiaje ? Mbona ambao hawasoma ndio wanalipa kodi na kufanya kazi ngumu na halali hlf mnataka mkae muwasemee bila kukatwa kodi ?

Wewe n fwala bht yko ktiba intaka kila mtu atoe maoni yke la svyo nngkuweka kundi la MATAGA.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,332
2,000
Habari za leo ndugu zangu,
Uzi wangu leo utakua mfupi sana.

Ni ushauri tu sifa za kugombea ubunge zibadirishwe walau mgombea awe na Shahada.

Na wanaogombea udiwani walau wawe na diploma.

Wanaogombea uenyekiti wa vijiji walau wawe na cheti cha form four.

Ndugu zangu ni ushauri tu.

Ninyi mnaonaje wakuu.
Na asiwe na umri wa zaidi ya miaka 60.
 
kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,203
2,000
Habari za leo ndugu zangu,
Uzi wangu leo utakua mfupi sana.

Ni ushauri tu sifa za kugombea ubunge zibadirishwe walau mgombea awe na Shahada.

Na wanaogombea udiwani walau wawe na diploma.

Wanaogombea uenyekiti wa vijiji walau wawe na cheti cha form four.

Ndugu zangu ni ushauri tu.

Ninyi mnaonaje wakuu.
Uongozi ni kipaji na sio vyeti.Tumeona awamu pendwa wenye phd lkn reasoning zao zipo chini kuliko kuku
 
Mwamba 777

JF-Expert Member
Nov 23, 2020
669
1,000
Habari za leo ndugu zangu,
Uzi wangu leo utakua mfupi sana.

Ni ushauri tu sifa za kugombea ubunge zibadirishwe walau mgombea awe na Shahada.

Na wanaogombea udiwani walau wawe na diploma.

Wanaogombea uenyekiti wa vijiji walau wawe na cheti cha form four.

Ndugu zangu ni ushauri tu.

Ninyi mnaonaje wakuu.
ndo maana skuzote tunasemaga hii katiba haifai imesha expire.

inatakiwa wote kuwa na shahada kuanzia mbunge mpaka mwenye kiti wa mtaa.

Haiwezekani taifa kubwa kama Tz kuongozwa na mbumbumbu.
 
luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
3,691
2,000
Kiukweli ipo hiyo haja yaan ukifuatilia elimu za baadhi ya wabunge wetu ni kichekesho huwezi kumtuma apeleke ujumbe wa nchi ata kwa raisi Ndayishiyme wa Burundi...yaan mbunge ni standard seven graduate tena mwenyewe ana tamba kwelii wakat hukunmtaan kuna majitu yana L.L.M, MSc, M.A hawana kazi .

Na ukizingatia nchi sasa ivi ina wasomi lundoooo wanaohitimu kila mwaka hawa ndio wana jua changamoto ya mfumo wa elimu yetu, hivyo tukipeleka hawa wana liberal minded wataleta mawazo mapya
 
Kong Chi

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
249
500
As long mtu ana akili timamu kugombea ni haki yake kikatiba na ilindwe kwa nguvu zote, huyu ujinga wa kiwango cha elimu or sijui umri ndio adui wa demokrasia, Rais wa Mbeya Mr Proud alikuwa anaongea point bungeni kuliko hao Drs na Profs
 
Kong Chi

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
249
500
Kiukweli ipo hiyo haja yaan ukifuatilia elimu za baadhi ya wabunge wetu ni kichekesho huwezi kumtuma apeleke ujumbe wa nchi ata kwa raisi Ndayishiyme wa Burundi...yaan mbunge ni standard seven graduate tena mwenyewe ana tamba kwelii wakat hukunmtaan kuna majitu yana L.L.M, MSc, M.A hawana kazi .

Na ukizingatia nchi sasa ivi ina wasomi lundoooo wanaohitimu kila mwaka hawa ndio wana jua changamoto ya mfumo wa elimu yetu, hivyo tukipeleka hawa wana liberal minded wataleta mawazo mapya
Kagombee na wewe na LLM yako uwashinde hao darasa la saba sio kulalamika tuu na kufikiri LLM yako ni ya maana wakati hata kuandika barua ya kuomba kazi kwa kiingereza kizuri huwezi
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
8,666
2,000
Habari za leo ndugu zangu,
Uzi wangu leo utakua mfupi sana.

Ni ushauri tu sifa za kugombea ubunge zibadirishwe walau mgombea awe na Shahada.

Na wanaogombea udiwani walau wawe na diploma.

Wanaogombea uenyekiti wa vijiji walau wawe na cheti cha form four.

Ndugu zangu ni ushauri tu.

Ninyi mnaonaje wakuu.
Kweli kabisa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom