Sifa ya kuwa Mbunge Tanzania ni kujua kusoma na kuandika, are we serious?

Unashangaa nini wakati sifa ya kuwa mwenyekiti wa chadema ni UDJ ni elimu ya hapa na pale?
Alafu sifa ya kuwa mwenyekiti wa ccm ni kupiga ngoma za kienyeji na kuogopa kiingereza huku tuna aminishwa ana PHD kumbe ni ya kupiga vigodoro??
 
Kiongozi msomi na ambae hajasoma elimu ya juu wapo tofauti katika maamuzi na kukabili changamoto za wananchi. Hawawezi kuwa sawa kati ya waliosoma na wasio soma
 
Unashangaa nini wakati sifa ya kuwa mwenyekiti wa chadema ni UDJ ni elimu ya hapa na pale?

can't you think outside the box?? Kwa akili yako umeshanipa uchadema,right? Hivi hizi akili kama zako Ni Mungu huyuhuyu ndo alikupa au umezitoa wapi? Wapi umeona nimeandika kuhusu CCM au CHADEMA? Naongelea wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,sio wabunge wa CCM wala Chadema,Idiot!
 
Atleast awe na diploma ya ufundi. Lakin hivyo vigezo ni vya kizaman na havina faida kwa sasa
 
Ccm haitaki wasomi wenye kujitambua kama Lissu, Zitto, Mdee, Mnyika, n.k, inapenda wasomi njaa kama Lipumba, Ndalichako, Mbarawa, Mahiga, na Dr Tulia, na wasio na ufahamu wowote kama Jah pipo, Lusinde, Musukuma n.k
 
Kwa hali ilivyo mbunge walau awe na digrii moja,kuwapeleka watu wasio na elimu bungeni inapofika muda wa mijadala anasubiria tu kipengele cha kupiga makofi.

Elimu inakusaidia pia kufanya maamuzi, wabunge wasio wasomi wamekuwa waoga pia kuwasemea wasomi. vijana wasomi tangazeni nia.
 
Ninaunga mkono hoja.

Matokeo ya kuwa na wabunge ambao hawana elimu yanapelekea hata elimu kuporomoka siku hadi siku .

Chanzo cha mikataba ya hovyo.

Chanzo cha huduma mbovu za kijamii.

Chanzo cha umasikini na vifo vinavyotokana na uzembe.
 
Nakuunga mkono, kuna kamati mbalimbali bungeni mf. Uchumi -asiye na elimu atachangia nini?? Kushiriki mjadala na wabunge wa nje! Asiyesoma anaona kama anaonewa, nataka kiwango cha chini kiwe degree na awe na "vision "
 
mkuu asante kwa kuniwakilishia hili hapa.

mambo mengi kiserikali yanaenda/yanapita kimaandishi kuongozwa na mtu ambaye hata kusoma kitabu cha page50 hajawai
alafu mtu huyu unategemea apitie mikataba ,bajeti,vifungu vya sheria mbali mbali ili aweze kujenga hoja ni ngumu

ndo maana mambo mengi ni bora liende

kama si elimu kupewa kipaumbele basi hii kazi ya ubunge iwe ya KUJITOLEA .
Ili tupate wazalendo na si wachumia tumbo
 
Mkuu hao wenye ma degree kibao si ndio wapiga makofi wazuri sana siku hizi? Kupiga makofi na kuunga mkono hoja mia kwa mia hakutokani na kiwango cha elimu ya mtu wengine huongozwa na kiwango cha njaa aliyonayo. Hatahivyo nakubaliana nawe elimu angalau ya diploma inafanya mtu awe na uelewa wa mambo mengi
 
Kwa hali ilivyo mbunge walau awe na digrii moja,kuwapeleka watu wasio na elimu bungeni inapofika muda wa mijadara anasubiria tu kipengere cha kupiga makofi,Elimu inakusaidia pia kufanya maamuzi,wabunge wasio wasomi wamekuwa waoga pia kuwasemea wasomi.vijana wasomi tangazeni nia
Katiba Mpya!
 
Back
Top Bottom