Sifa ya kuwa board chairman au board member wa mashirika ya umma ni ipi?

Ndumule

Member
Sep 20, 2010
6
1
Mtakubalina nami kwamba bodi ya wakurugenzi ina mchango mkubwa sana kwenye uendeshaji wa shirika lolote lile pamoja na mashirika yetu ya umma. Ukiangalia mashirika yote yanayofanya vizuri yana bodi zenye ujuzi.

Mtu mmoja aliniambia Air Rwanda board chairman wake alikuwa Mwendeshaji mkuu wa Shirika la ndege la Ethiopia na unaweza ukaona jinsi kuwa na ujuzi kama huu kwenye board unavyobadilisha mambo. Air Rwanda inafanya vizuri kuliko sisi. Kagame ameshasema he will find skills anywhere to develop Rwanda, je haijafika wakati wa Tanzania kuwa na bodi zetu za mashirika ya umma zenye watu wenye ujuzi hata kama wanatoka nje?

Naomba mtu mwenye taarifa atupe vigezo vinavyotumika kuchagua wenyeviti wa bodi na wajumbe wa bodi za mashirika ya umma hapa Tanzania kwa sasa. Na ikiwezekana tuyaangalie mashirika yetu makuu kama Bandari, ATC, Tanesco, NSSF, PPF na mengineyo kama yana bodi zenye uwezo yaani uaminifu na weledi (professionalism and integrity). Naamini competence comprises of skills, knowledge and attitude (integrity etc)
 
uwe mtaalam wa kuiba kwa kutumia kalamu na 40%ya pesa utakazoibia shirika uzipeleke ccm makao makuu
 
Back
Top Bottom