Sifa ya kiongozi ni Maono(vision) na sio elimu, hongera RC Makonda

emmanuel mhecha

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
933
541
Wandugu za weekend,

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Jamaa kaweka Planning yake iko poa yaani ana focus sana. Ndio sifa ya kiongozi kuangalia ya mbele kabla ya watu wako.

Kwa plan ya kuweka system katika vituo vya police ili kufuatilia wahalifu tangu wanavyoingia jela na wanafungwa wapi nampa Big up ili tujue hawa mafisadi ni kweli wanafungwa au ni kiini macho tu halafu Majizi ya Mali za umma yanaendelea kuserebuka na wife ndani na hukumu imetolewa.
 
Mkuu, ni kipi kingine cha maana alichokiongelea kwenye focus yake hiyo ya kuwasaidia wana Darisalama? Maana siamini kama wakazi wa Tandale, Manzese na uswazi kwingine priority yao ni kujua kama kuna system inefungwa police ili kutrace mafisadi wamefungwa gereza lipi
 
hivi huyu jamaa nini aliwahi anzisha kikafanikiwa?

Machangudoa
Usafi
Walimu bure
Kupaka rangi ukuta
etc
 
Naona kila.la kaahidiwa ulaji,kwamba hata MOAT ikimfungia,kesho yake anapata wadhfa serikalini.

#VYEO_VYA_KUPEANA
 
Huu si muda wa plan. Yuko kwenye ofisi zaidi ya mwaka anatuletea plan za police ambazo si zake zilikuwepo na sasa wanafanya pilot study hapo dar.
Hayo police walieleza tangu zama zile kabwe anatumbuliwa.

Hii nchi mbona vurugu vurugu. Hawa viongozi wanatuona sisi maboya sana.

Kazi kubwa kutafuta activity za kuja kuongea kwenye media.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, ni kipi kingine cha maana alichokiongelea kwenye focus yake hiyo ya kuwasaidia wana Darisalama? Maana siamini kama wakazi wa Tandale, Manzese na uswazi kwingine priority yao ni kujua kama kuna system inefungwa police ili kutrace mafisadi wamefungwa gereza lipi
Hospital zetu kutakuwa kitengo maalumu kwa wagonwa ambao wako serious sana kama malaria Kali mgonjqa hatakiwi asubiri folen
 
Wandugu za wikend, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,jamaa kaweka Planning yake iko poa yaani anafocus sana,ndio sifa ya kiongozi kuangalia ya mbele kabla ya watu wako,kwa plan ya kuweka system katika vituo vya police ili kufuatilia waharifu tangu wanavyoingia jera na wanafungwa wapi nampa Big up ili tujue hawa mafisadi ni kweli wanafungwa au ni kiini macho tu halafu Majizi ya Mali za umma yanaendelea kuserebuka na wife ndani na hukumu imetolewa,najua wale wa mlengwa wa kushoto mtasema (aaaaa lakini Mkala)
Correction: Vision not Focus
 
Tatizo sio maono wala elimu maana hata JPM aliwahi kusema pale bandarini kuwa hakuna sheria inayosema STD-VII asiajiliwe serikalini. Tatizo hapa ni vyeti feki ambapo anayevimiliki uhesabiwa jinai!
 
hivi huyu jamaa nini aliwahi anzisha kikafanikiwa?

Machangudoa
Usafi
Walimu bure
Kupaka rangi ukuta
etc
Kiongozi ni kuanzisha,kama wananchi hamtoi ushirikiano mnaendelea kununua k,Makonda afanyaje?
Halafu umesahau kutaja wauza unga wote wamekimbilia bondeni
 
Kama ni maono na sio vyeti basi warudi viongozi waliotumbuliwa kisa vyeti japo walifanya kazi nzuri

Do a little thing with the great love ~ Mother Theresa
 
Huwezi kuwa na maono bila elimuuuuuu
Huyo hadi anayoyaongea mengine anaandikiwa anakariri kariri.....
Mtu mpuuzi asiyekuwa na elimu na heshima huwa haihitaji nguvu sana sana kumgundua, huwa anajidhihirisha mwenyewe kwa upumbavu wake....
 
Huyo jamaa hawezi kuwa kwenye mdahalo hata kwa dakika tano kwa sababu upeo wake ni below average ya mtanzania(wengi wetu upeo mdogo)
Hayo maigizo wanayomtayarisha mwezi mzima labla kumkaririsha aonekane anafaa hata mtoto wa darasa la kwanza anaweza kukaririshwa vitu vya kuongea
 
Back
Top Bottom