Sifa ya Division 4 na 0 kujiunga na Jeshi: Je, ni mkakati wa kuwabeba ndugu/watoto wa vigogo waliofeli?

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,381
73,976
Naiweka kama "Hypothesis" kuwa: Akina Simbachawene and Co. Ltd, (VIGOGO) wana ngudu zao kibao ni failure wa form 4 na 6 ambao Ni Div ZERO NA 4.

Sasa kuwapa ajira, sifa ni div 0 na 4. Sifa hizo zitawakumba ndugu zake, watoto wa marafiki na marafiki wao wote.
 
Miaka yote ambayo failures walikuwa wanachukuliwa huko, alikuwa anabebwa mtoto wa nani ?
All the "cream" were absorbed into High school and therefore failure leftovers were the only choice to join such non-academic professions such as police, jeshi magereza and the like!!
 
Nia kuu ya kujaza failures kwenye jeshi la polisi ni kuwa na mapolisi wasiojua kuifata PGO ili watumike kwa maslahi ya serikali katili ya CCM.
We unadhani PGO ina kipengere hata kimoja cha kuifavour Chadema.

Ile ni kwa ajiri yao wenyewe na CCM yao.
 
Naiweka kama "Hypothesis" kuwa: Akina Simbachawene and Co. Ltd, (VIGOGO) wana ngudu zao kibao ni failure wa form 4 na 6 AMBAO NI dIV ZERO NA 4. Sasa kuwapa ajira , sifa ni div 0 na 4. Sifa hizo zitawakumba ndugu zake, watoto wa marafiki na marafiki wao wote
Hakuna division zero aliyeruhusiwa kujiunga na jeshi.
 
Kama ulipata Div One, two, three tafsiri yake ulikwenda kidato cha sita hivyo huna sifa za kuajiriwa kama form four, hivyo kuna wa kidato cha sita pia wanaajiriwa na kama ulikwenda kidato cha sita ukapata Div 1,2,3 bila shaka ulikwenda chuo kikuu hivyo huna sifa ya kuajiriwa kama form six maana unayo degree.

Sasa matangazo ya ajira yao inaajiri kidato cha nne,kidato cha sita na wenye elimu ya chuo kikuu hivyo omba kulingana na Elimu yako shindana na wa elimu yako usiwazibie riziki wenzako na Uache Majungu. Wewe unadegree halafu unataka uombe kama form four halafu ukifika kazini ujitambulishe unayo degree unataka kazi za watu wa form four afanye nani?

Wanaajiri watu kulingana na mahitaji yao siyo upendavyo wewe.

Majeshini wanazo Elimu zao hata kama hujui kusoma wanakufundisha kile kitu wanachoamini utakiweza wala Elimu ile siyo kama yetu ndiyo maana wao siyo kama sisi.
 
Unajua mtu yoyote ambaye Brain haifanyi kazi vizuri huwa anakuwa na nguvu nyingi za misuli
 
Ni kupata wale watu ambao wataambiwa wavunje watu miguu na kuwapiga risasi watafanya bila hata ya kufikiri
 
Kumbuka tu kuna helcopter kule sijui zinaendeshwa na nani? kumbuka hawa watu wanazo hospitali sijui madaktari ni nani ? kumbuka wanavikosi vya cyber crime sijui kwenye computer huwa anakaa nani?

Kumbuka wanayo magari hawa siju wahandisi wao ni nani? Kumbuka wanavyo viwanda vya nguo siju mafundi wao ni nani? Kumbuka wanaendesha mashtaka mahakamani sijui hao wanasheria ni wakina nani?

Nakukumbusha tena kila Elimu kule majeshini inahitajika kwa sababu maalumu nenda kaombe kazi kwa kushindanishwa na watu wa Elimu yako siyo wewe unayo masters unataka ufanye Usaili na form four. wakati mtakwenda kupishana majukumu.
 
Hoja zote hizi zimekuja kutokana na kukosa ajira ,miaka ya nyuma watu kujiunga na majeshi ilikuwa shida hawataki kabisa leo hii watu wanaona ni ajira
 
Naiweka kama "Hypothesis" kuwa: Akina Simbachawene and Co. Ltd, (VIGOGO) wana ngudu zao kibao ni failure wa form 4 na 6 AMBAO NI dIV ZERO NA 4. Sasa kuwapa ajira , sifa ni div 0 na 4. Sifa hizo zitawakumba ndugu zake, watoto wa marafiki na marafiki wao wote
Angalia wasomi wote hawa wa elimu ya vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi .https://youtu.be/9OX8QeO3284
 
Wakichukuliwa division 1 mnalalamika ni watoto wa vigogo...

Wakichukuliwa division zero bado mnalalamika ni watoto wa vigogo...

Am kweli tenda wema uende zako...
 
Wakichukuliwa division 1 mnalalamika ni watoto wa vigogo...

Wakichukuliwa division zero bado mnalalamika ni watoto wa vigogo...

Am kweli tenda wema uende zako...
Sasa tujiulize hawa ni zero

Angalia wasomi wote hawa wa elimu ya vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi .https://youtu.be/9OX8QeO3284
 
Back
Top Bottom