Sifa muhimu za binti wa kuoa kuanzia 2021 na kuendelea

Sasa kwa kumiliki nia thabiti, upendo furaha na amani ndio umeweka mzigo wote huo wa vigezo kwa binti wa watu?

Wewe mwenyewe hapo mileage inasoma ngapi kwanza, na Je, unatoka familia bora?

Nnachomaanisha lazima wewe uwe kwanza na hivyo vigezo unavyovihitaji kutoka kwa mwenza unaemtarajia.
Ndio mkuu vigezo hivyo ni navyo , na vijana wengi wanavo lakini nashindwa kuelewa inakuwaje inapofikia wao suala la kuoa wanakosea kufanya maamuzi sahihi na inakuja kuwa cost?

Wengi wanoa kutimiza wajibu tu katika jamii, na tamaa za kimwili!

Wewe unafikiri wanawake hawaset vigezo vyao wanapotafuta mwenza wa kuwa nae?
 
Tumetofautiana vigezo na mitazamo mkuu, usitake dunia yote iamini katika jambo unaloliamini wewe. Wengi sana wamekua na bikra na tumezitoa wakiwa na umri wa zaidi ya 26 na bado hatujawaoa, na mengine mengi.
Wewe unachokitafuta ni nini kama sio uzinzi oa wanawake wazuri hao tulia na mmoja
 
Ndio mkuu vigezo hivyo ni nanvyo , na vijana wengi wanavo lakini nashindwa kuelewa inakuwaje inapofikia wao suala la kuoa wanakosea kufanya maamuzi sahihi na inakuja kuwa cost??
Wengo wanoa kutimiza wajibu tu katika jamii, na tamaa za kimwili!

We unafikiri wanawake hawaset vigezo vyao wanapotafuta mwenza wa kuwa nae?

Kuwa na vigezo sio tatizo, vigezo vya aina gani? Kumbuka haviwezi kufanana kati ya mtu na mtu. Inategemea na mhusika anahitaji kitu gani.
 
kila mtu na maisha yake, tusipangiane...nafahamu watu wameoa kwenye familia zenye hali ya chini...na mwanamme/mume ndio anapata usingizi anapoona amewawezesha upande wa mkewe...

hakuna sheria itakufunga usiposaidia upande wa mke...ni wewe na mkeo na namna mlivyojipangia maisha yenu...
 
  • Ukasomeshe watoto wa shemeji zako kuanzia primary hadi varsity.
  • Ukamjengee Baba mkwe nyumba inayoeleweka maana ya sasa haifai kabisa kufikia.
  • Usipompà bwashe 50k utatangazwa kuwa bwashe hana kitu yule na ukienda ukweni hutaheshimika.
  • Hakikisha unajenga nyumba ya rooms 4+ coz mabwashe watahamia hapo ili kupunguza machungu ya bush(wanakuja kupumzika).

Mkuu, wengine tunakuelewa. Swala la bikra siwezi elezea sana. Ila kama umeamua kuoa asiye bikra, basi mambo ya kutoa mahari kubwa hayapo, utalipaje mahari kubwa kwa unsealed pussy? Yani unaambiwa 4m wakati wakulungwa walishajichapia wakachoka huko?

Nashukuru sana mkuu kwa kutoogopa kuwa mwanaume na kulezea hali halisi cha kushangaza wanaume wa siku hizi hawafikirii kabisa ... wanaacha hisia ziwaendeshe na kuhofia zaidi jamii itawachukuliaje?
 
Hakuna shule iliyowahi kufanikiwa kufundisha mapenzi haipo, kila mtu aliumbwa na perfect match yake umri hauwezi kuwa limiting factor kama mmeunganishwa na upendo, kiufupi watu wanapitia mambo mengi katika maisha na hubarika for good.
Katika suala la ndoa lazima kuwe na limit ya age hasa kwa wanawake! Huyo 45yrs wako mnaweza kuishi tu sio lazima uoe
 
"atoke familia tajiri" wewe hapo ulipo ni tajiri??

Au ndio atoke familia tajiri ili na wewe upate mserereko.
Yes atoke familia wanaojiweza wenyewe wasiwe tegemezi (ndugu lawama) mimi si3ndi kuoa katika ukoo wao kutoka kwenye umasikini, hilo ni jukumu lao kupambana na adui ambaye ni umasikini!
 
Kuwa na vigezo sio tatizo, vigezo vya aina gani? Kumbuka haviwezi kufanana kati ya mtu na mtu. Inategemea na mhusika anahitaji kitu gani.
Ukishajitambuwa unahitaji niji hauwezi kupata tabu wala kuendeshwa na hisia
 
kila mtu na maisha yake, tusipangiane...nafahamu watu wameoa kwenye familia zenye hali ya chini...na mwanamme/mume ndio anapata usingizi anapoona amewawezesha upande wa mkewe...

hakuna sheria itakufunga usiposaidia upande wa mke...ni wewe na mkeo na namna mlivyojipangia maisha yenu...
Siwezi kukushangaa ukiamnini kwenye kubeba misalaba ya watu wengine .. tunatoka kwenye jamii inayoamini kwenye ujamaa zaidi.. na ina hasara zake
 
Kwa mtazamo wangu naona, kila kitu kinaanzia kwa mwanaume, au kama ni mwanamke ndio anatafuta wa kuolewa nae basi, itaanzia kwake,

1. Tuanze swala la bikra, Naamini mwanamke kutokuwa na bikra sio sababu ya msingi mkashindwa kuishi maish ya amani, maana maisha ya amani katika ndoa hayaletwi na ngono pekee yake, kuna tabia ya mtu, dini, malezi, tv anazoangalia, na mambo mengi tuu, pia hapo ikumbukwe bikra hutoka kwa njia tofauti tofaut sio ngono pekee yake, na mtu kuwa bikra haimaanishi hajawai kuwa kwenye mahusiano na wanaume pia

Basi tuje kwenye swala la msingi kuhusu bikra, kwanin nasema inaanzia kwako wewe mwanaume, ni kuwa wakati wewe unataka mwanamke mwenye bikra wewe unayo hiyo bikra? kwanin nasema hivyo, wakati wewe ukioa bikra na wewe sio bikra, pia itakua ni matatizo vile vile ndani ya nyumba, kwani tunajua mwanamke bikra hajazoea kufanya ngono muda mrefu na mara kwa mara, vipi wewe sasa na experience yako ya miaka 10 ya kufanya ngono Gia ishatumika mpaka inahitaji busta kuzunguka, ukiwa unahitaji mara kwa mara na akasema akasema hajazoea, utaenda nje ya ndoa kutafuta bikra mwingine ama utarudi kwa hao mnaowaita malaya, (kwanini usioe haohao mnaotoshelezana sasa ili upewe unavotaka) na ukitoka nje ya ndoa hujatatua tatizo pia kumbuka.

2. Tukija kwa upande wa umasikini ni vile vile wakati unataka kuoa kwenye familia za kitajiri au mwanamke tajiri, unasemaje wew kwa upande wako, ni tajiri? familia yako ni ya kitajiri (hawakumbatii umasikini?) mimi na nyinyi wote tumeshashuhudia mwanaume akiteswa na kunyanyaswa kisa mwanamke ana kipato kuzidi huyo mwanaume, humajawai kusikia msemo unaosema mwanaume anaweza kuishi na mwanamke asie na kazi kwa miaka 5 ila mwanamke awezi kuishi na mwanaume asie na kazi kwa siku 5? kama unatak kuishi na familia ya kitajiri basi hakikisha na wew ni tajiri wa kuzidi, na ukiwazidi tunarudi pale pale, kuwa lazima majukumu yatakuepo kwa upande wa wakwe, sasa usitake nikuelezee majukumu yana ghalama kiasi gani kwa hao matajiri, pia nakubaliana na kuoa familia za kimasikini unaweza ukaonekana kama ndio mkombozi wao wa kuwatoa kwenye janga lao la umasikini, lakini sio wote, sio familia zote zipo hivyo, na hata kama kuna hela unatakiwa kuwapa hiyo familia usichukulie kama wanakumola ila chukulia kama ni moja ya familia na unawasaidia kama mmoja wa wana familia, em jichukulie wew ndio mkwe sasa na binti yako kaolewa usingependa usaidiwe kwa namna moja au nyingine? kwani wew pamoja na hela zako zilizo wazidi unahisi hamna siku utataka msaada kutoka kwao? maisha ni kusaidiana jamani, pia wanaume msichulie kila siku kuwa mnatumika kwenye hela zenu, maisha ya sasa yamebadilika, mahitaji ni mengi sana, kwa kila mtu, hivyo ni vyema kusaidiana kwa hapa na pale inapobidi, ila msaada usizidi uwezo wako, hivyo basi weka bayana kwa mwenza wako kiasi unachopata ili kusiwe na chuki pale unashindwa kumpa mtu hela

MWISHO.
Ndoa bora na imara huja kwa kupitia wanandoa wanaohusika na sio Baba mkwe, mama mkwe, shemeji wala wifi, Biblia inasema atatoka mtu mmoja kwenda kuungana na mwenzake nao watakua mwili mmoja, aisemi atatoka na shemeji wala wifi wala mkwe, na ndoa hudumishwa Upendo, uvumilivu, kutokua na husuda, pasipo masengenyo, furaha ya wawili. Ndoa haidumishwi na Mali (mnahitaji Mali ila sio mali pekee itafanya mdumu), uchoyo haufai katika ndoa, Ndoa haidumishwi na bikra, kama mkeo ni malaya ni malaya tuu haijarishi ulimvunja bikra ama la. (maana hata malaya alizaliwa na bikra), kama mkeo ni malaya hata ukimvunja hiyo bikra ataendelea kuwa malaya, kwani nyinyi hamjasikia malaya wenye bikra?

Hapa muhimu Tunatakiwa tumuombe sana Mungu ili tunapochagua mwenza wetu awe ni yule ambae tumepewa na Bwana na sio hawa tunawaangalia kwa macho tuu na kuwatani kwa shepu walizonazo, sura au wanavojipamba, vifua, pesa, magari na mengine mengi.
Bikra au pesa havitakupa ndoa bora, bali inaanzia kwako kama utaendana na hiyo bikra au huo utajiri
mtazamo wako ni mzuri ,ila ifkie kipindi muelewe ya kuwa watoto wenu wanapoamuwa kufunga ndoa -- muwaache wakajitegemee musiwaingilie . waacheni na wao wakaanzishe familia zao aisee ..
hamuwadai chochote wazazi wengi wanawasumbuwa na kuwatwesha watoto wao mizigo mizito na kuwafanya waone ndoa ngumu! na ndio tunafikia hapa kwenye mtazamo wa kutokuoa masikini.
 
Akili za kidangaji hizi siku hizi zime hamia mpaka kwa wanaume.

Wasiokuwa na mawe sijui waende wapi,kweli haki sawa imeharibu baadhi ya waunaume. Ila kijana mwanaume kaumbiwa kubeba majukumu na kukabiliana na changamoto.

Mtafute mwanamke mwenye hofu ya Mungu na atakaye kupenda kwenye kila hali na kumbuka hamna kitu KICHUNGU duniani kama hela ya mwanamke, hela yamwanamke si yako, japokuwa wanalilia 50/50 ila sio kwenye hela yao
kamwe hela ya mwanamke hainihusu mimi mkuu , sijali anaizingiza kiasi gani wala kipato chake, ila sihitai kuwa na mwanamek anayetoka kundi la wanyonge wale wanotoka familia zinazo amini kwenye kumtegema binadamu mwenzao awakomboe badala ya Mungu !
 
Kila uzi watu wanasema tafuta pesa, tafuta pesa ...ni kama wao wanazo nyingi au ni ushamba tu wa watu wa jf
vijana wa sasa hivi ili kuw ana self confidence inawabidi wajiweze kiuchumi na kifedha , wasilolijuwa ni kuwa maamuzi, misimao busara na akili hazitokani na pesa pekee..
mwisho wa siku pesa haziwasaidii katika mahusiano yao ya kimapenzi wala ndoa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom