Uchaguzi 2020 Sifa Kuu Tano (5) za Bernard Kamillius Membe Zinazoonesha kwamba hafai kuwa Rais wa Nchi

Kwaiyo Jiwe ndo anafaa kuongoza hii nchi miaka 10.?

Watz wengi hasa Maficcm ni wapuuzi sana! Kuna Jambo liko wazi kabisa....Kati ya JPM na BCM kuwa BCM(Bernad Camilius Membe) ana sifa bora za Uongozi kuliko Magufuli.

  1. BMC ni Mwanadiplomasia wa Kimataifa wakti JPM ni mbumbumbu.
  2. BMC ni kachero mbobezi ilhali JPM hajui lolote kuhusu Hilo.
  3. BMC ana uzoefu katika Mahusiano ya Kimataifa kuliko JPM.
  4. BMC ana uzoefu kazini kuliko JPM.
  5. BMC anatema 'yai" au slang vizuri sana kuliko JPM.
  6. BMC ametembelea nchi za nje nyingi Sana wakti JPM hajakanyaga hata nji moja.
  7. BMC ana exposure kubwa Kimataifa ilhali JPM hana hiyo exposure hata kidogo!
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikimfuatilia ndugu yetu na Mtanzania mwenzetu Bernard Membe katika harakati zake za kuutafuta Urais wa JMT. Kwa sasa nimefanikiwa kung’amua sifa zake tano (5) ambazo binafsi naona kabisa kuwa zinamfanya asiwe mtu sahihi kwa nafasi hiyo kubwa na takatifu. Sifa hizo ni kama ifuatavyo:

Amekosa unyenyekevu: Miezi iliyopita katika mitandao ya kijamii ulisambaa ujumbe wa sauti, Ndugu BM akiwa anamsema vibaya Rais wa nchi na viongozi wengine wa CCM. BM alikubali kuwa sauti katika ujumbe huo kweli ni yake, lakini akabaki na msimamo wake kuwa hawezi kumuomba mtu radhi sababu hajakosea chochote. Ameendelea kutunishiana misuli na viongozi wa Chama hadi walipofikia hatua ya kumvua uanachama. Binafsi naona kuwa alikosa tu sifa ya unyenyekevu na kuomba radhi ili maisha mengine yaendelee kama kawaida.

Mjivuni: Hivi karibuni BM akiongea na baadhi ya watu wa Mkoa wa Lini alisikika akisema uchaguzi huu bila yeye kuwapo utakosa mvuto. Alisema kuwa yeye pekee ndiye “Mnogeshaji”. Logically ni kuwa hakuona mtu mwingine yeyote nchini, mwenye sifa kama zake au kumzidi yeye ambaye anaweza kunogesha uchaguzi wa mwaka huu. Huo ni ujivuni na kujiona yeye ni bora kuliko Watanzania wengine wote.

Mtu wa masharti mengi: BM akiongea na watu hao alitoa sharti kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimsafishe ili aweze kuchukua fomu za kuwania nafasi ya kugombea Urais wa JMT, vinginevyo angefanya maamuzi mengine. Pili, juzi ametoa sharti kwa vyama vya upinzani kuungana ili awe mgombea wao. Binafsi naona kama ni mtu anayependa kutoa masharti mengi ili atekeleze jambo fulani. Wananchi tunakuwa katika wakati mgumu maana tutakiwa kutimiza masharti yake ili tu atuletee maendeleo.

Mvunja sheria: Kwa nafasi yake na uzoefu wake katika siasa alipaswa kujua kuwa muda wa vyama kuungana na kusimamisha mgombea mmoja umepita, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 na kufanyiwa Revision 2019. Sheria inataka vyama kutoa taarifa ya kuungana miezi mitatu kabla ya Uchaguzi, na lazima azma hiyo iridhiwe na Mkutano Mkuu wa Kila Chama kinachoungana. Tafsiri ya Uchaguzi ni kuwa ni mchakato unaoanza pale vyama vinapoanza Kutafuta Wagombea na unahitimishwa pale Mshindi Anapotangazwa. Hivyo vyama vimechelewa kuungana, BM analazimisha kutokea uvunjifu wa sheria kwa faida zake binafsi.

Opportunist: Mfumo wa Tume ya Uchaguzi, hasa namna inavyopatikana na wajumbe wake haujaanza leo, au awamu hii ya uchaguzi. Malalamiko ya vyama vya upinzani kudai kile wanachodai kuwa ni Tume Huru hayajaanza awamu hii. Mwaka 2015 BM alipokuwa akiona kuwa ana nafasi kubwa ya kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM, Tume Huru haikuwa agenda kwake. Hivyo hivyo kwa miaka ya nyuma ambapo yeye alikuwa akitangazwa na Tume hii hii kuwa mshindi wa Ubunge. Swali la kujiuliza, ni kipi ambacho leo kimemfanya aone kuwa Tume ina mapungufu ikiwa miaka yote amekuwa kimya? Binafsi naona kuwa ni mtu anayetafuta fursa kwa manufaa binafsi. Kwake ameona ili aweze kupokoleka Upinzani basi aimbe wimbo wao, ikiwa miaka mingine yoyote amekuwa akiuona huo wimbo kuwa ni kelele.

HITIMISHO
Watanzania tunapaswa kuwa waangalifu sana na aina ya viongozi tunaowachagua. Ni wakati sasa kwetu sisi wanachama wa vyama hivi vya upinzani kupaza sauti kubwa ya Kuwakataa watu kama hao, ambao wanatoka kwenye vyama vyao katika hatua za mwisho za uchaguzi, na baada ya uchaguzi wanatugeuka na kurejea tena huko walikotoka, maana kimsingi ndiko iliko historia yao ya Siasa, na mtu hawezi chafua legacy yake kirahisi hivyo.​

Membe anategeme kuloga...wakati sisi tunamtegemea Mungu! Nani aongozwe na na mlozi tena aliye katwa mkia?
 
Watz wengi hasa Maficcm ni wapuuzi sana! Kuna Jambo liko wazi kabisa....Kati ya JPM na BCM kuwa BCM(Bernad Camilius Membe) ana sifa bora za Uongozi kuliko Magufuli.

  1. BMC ni Mwanadiplomasia wa Kimataifa wakti JPM ni mbumbumbu.
  2. BMC ni kachero mbobezi ilhali JPM hajui lolote kuhusu Hilo.
  3. BMC ana uzoefu katika Mahusiano ya Kimataifa kuliko JPM.
  4. BMC ana uzoefu kazini kuliko JPM.
  5. BMC anatema 'yai" au slang vizuri sana kuliko JPM.
  6. BMC ametembelea nchi za nje nyingi Sana wakti JPM hajakanyaga hata nji moja.
  7. BMC ana exposure kubwa Kimataifa ilhali JPM hana hiyo exposure hata kidogo!
Nimelazimika kukuita we ni mpumbafu kabisa maana unalopoka tu bila mantiki! Tupe faida moja tu kwa taifa ambayo huyo mkatwa mkia wako ameliletea faida ktk nyazifa alizolitumikia n Mimi nikuletee achievement 10 za Magu! Hakuna nchi ya kuuzwa Tz, huyo mkatwa mkia mwambie ajiuze mwenyewe kwa hao waliomfadhiri! Tz kwa Sasa Ina mwenyewe...na halali!
 
Watz wengi hasa Maficcm ni wapuuzi sana! Kuna Jambo liko wazi kabisa....Kati ya JPM na BCM kuwa BCM(Bernad Camilius Membe) ana sifa bora za Uongozi kuliko Magufuli.

  1. BMC ni Mwanadiplomasia wa Kimataifa wakti JPM ni mbumbumbu.
  2. BMC ni kachero mbobezi ilhali JPM hajui lolote kuhusu Hilo.
  3. BMC ana uzoefu katika Mahusiano ya Kimataifa kuliko JPM.
  4. BMC ana uzoefu kazini kuliko JPM.
  5. BMC anatema 'yai" au slang vizuri sana kuliko JPM.
  6. BMC ametembelea nchi za nje nyingi Sana wakti JPM hajakanyaga hata nji moja.
  7. BMC ana exposure kubwa Kimataifa ilhali JPM hana hiyo exposure hata kidogo!
Kuda wakutembeza bakuli na kulitukanisha taifa umepita kitambo Sana...habari ya mjini kwa Sasa ni kujitegemea! N kuwafanya wao ndio waje kututembelea...watufuate wao!
 
Mnamwanzishia uzi mtu ambae hajachukua fomu.....Happ kwene sheria umekosea mkuu maana tume bado haijatangaza siku mwezi Wala tarehe ya uchaguzi
 
Amekosa unyenyekevu: Miezi iliyopita katika mitandao ya kijamii ulisambaa ujumbe wa sauti, Ndugu BM akiwa anamsema vibaya Rais wa nchi na viongozi wengine wa CCM. BM alikubali kuwa sauti katika ujumbe huo kweli ni yake, lakini akabaki na msimamo wake kuwa hawezi kumuomba mtu radhi sababu hajakosea chochote. Ameendelea kutunishiana misuli na viongozi wa Chama hadi walipofikia hatua ya kumvua uanachama. Binafsi naona kuwa alikosa tu sifa ya unyenyekevu na kuomba radhi ili maisha mengine yaendelee kama kawaida.
Mimi hata nikipewa milioni siwezi kumpa kura BM nikaacha kumpa JPM, lakini ukweli lazima usemwe kwamba kimsingi Membe kwenye sauti ile hakufanya kosa lolote la kustahili kuomba radhi.
Ipo wazi kabisa Mzee Kinana, Nape Nnauye na Ngeleja walimkosea sana Mh.Raisi kwenye sauti zile. Tena washukuru sana walitenda vile kwa kiongozi wa Tanzania ya amani. Ingekuwa nchi nyingine sasa tungeongea mengine.
Sijaona kosa la Yusuf Mzee Makamba kwenye kauli zake katika zile sauti.

Alichofanya Membe ni kulalamikia au kuhoji tu, tena bila lugha ya kashifa na dharau.
Memne hafai kabisa kuwa raisi kwa sababu zingine lakini si kwa kipengele hiki nilicho kunukuu.
 
Watz wengi hasa Maficcm ni wapuuzi sana! Kuna Jambo liko wazi kabisa....Kati ya JPM na BCM kuwa BCM(Bernad Camilius Membe) ana sifa bora za Uongozi kuliko Magufuli.

  1. BMC ni Mwanadiplomasia wa Kimataifa wakti JPM ni mbumbumbu.
  2. BMC ni kachero mbobezi ilhali JPM hajui lolote kuhusu Hilo.
  3. BMC ana uzoefu katika Mahusiano ya Kimataifa kuliko JPM.
  4. BMC ana uzoefu kazini kuliko JPM.
  5. BMC anatema 'yai" au slang vizuri sana kuliko JPM.
  6. BMC ametembelea nchi za nje nyingi Sana wakti JPM hajakanyaga hata nji moja.
  7. BMC ana exposure kubwa Kimataifa ilhali JPM hana hiyo exposure hata kidogo!
Ipi Kati ya hizi itabadili maisha ya watanzania na kujenga uchumi?
 
Watz wengi hasa Maficcm ni wapuuzi sana! Kuna Jambo liko wazi kabisa....Kati ya JPM na BCM kuwa BCM(Bernad Camilius Membe) ana sifa bora za Uongozi kuliko Magufuli.

  1. BMC ni Mwanadiplomasia wa Kimataifa wakti JPM ni mbumbumbu.
  2. BMC ni kachero mbobezi ilhali JPM hajui lolote kuhusu Hilo.
  3. BMC ana uzoefu katika Mahusiano ya Kimataifa kuliko JPM.
  4. BMC ana uzoefu kazini kuliko JPM.
  5. BMC anatema 'yai" au slang vizuri sana kuliko JPM.
  6. BMC ametembelea nchi za nje nyingi Sana wakti JPM hajakanyaga hata nji moja.
  7. BMC ana exposure kubwa Kimataifa ilhali JPM hana hiyo exposure hata kidogo!

NIMENOTE TUKISHINDA UCHAGUZI SISI MAFISIM NAKUFUNGULIA THREAD YA KUKUCHAMBA
 
Watz wengi hasa Maficcm ni wapuuzi sana! Kuna Jambo liko wazi kabisa....Kati ya JPM na BCM kuwa BCM(Bernad Camilius Membe) ana sifa bora za Uongozi kuliko Magufuli.

  1. BMC ni Mwanadiplomasia wa Kimataifa wakti JPM ni mbumbumbu.
  2. BMC ni kachero mbobezi ilhali JPM hajui lolote kuhusu Hilo.
  3. BMC ana uzoefu katika Mahusiano ya Kimataifa kuliko JPM.
  4. BMC ana uzoefu kazini kuliko JPM.
  5. BMC anatema 'yai" au slang vizuri sana kuliko JPM.
  6. BMC ametembelea nchi za nje nyingi Sana wakti JPM hajakanyaga hata nji moja.
  7. BMC ana exposure kubwa Kimataifa ilhali JPM hana hiyo exposure hata kidogo!
Una tafuta rais wamataifa au rais wa Tanzania ?
 
Ni kwa nini tunamjadili Membe ambaye hajachukua hata fomu badala ya kuwajadili waliochukua fomu tayari?
 
Kuna mwanasiasa asiye mnafiki? Mhodhi wa Mali? Mpenda sifa? Mwongo? Siku moja Shangazi Fatma Karume aliuliza hivi ni lazima mwanasiasa awe mwongo? Aliuliza hivyo kwa sababu mwanasiasa akiulizwa I say mbona ulipoulizwa ulijibu kama sivyo? Atakujibu “Ni siasa tu hujui” kwa hiyo siasa Tanzania imebadilishwa kuwa uwongo na mambo yote Haya!!!!! Ainu! Ndiyo maana NYU anahama tu chama kwa kuwa tu upande fulani kuna dola itakayomhakikishia Kushinda Kitu fulani !! Shame on them! Sijui watanzania ni kwa nini kwenye kura zetu tusiweke tu 00000 kwa wote tuone watafanya nini!
 
Watz wengi hasa Maficcm ni wapuuzi sana! Kuna Jambo liko wazi kabisa....Kati ya JPM na BCM kuwa BCM(Bernad Camilius Membe) ana sifa bora za Uongozi kuliko Magufuli.

  1. BMC ni Mwanadiplomasia wa Kimataifa wakti JPM ni mbumbumbu.
  2. BMC ni kachero mbobezi ilhali JPM hajui lolote kuhusu Hilo.
  3. BMC ana uzoefu katika Mahusiano ya Kimataifa kuliko JPM.
  4. BMC ana uzoefu kazini kuliko JPM.
  5. BMC anatema 'yai" au slang vizuri sana kuliko JPM.
  6. BMC ametembelea nchi za nje nyingi Sana wakti JPM hajakanyaga hata nji moja.
  7. BMC ana exposure kubwa Kimataifa ilhali JPM hana hiyo exposure hata kidogo!
Kwa hiyo hizo sifa za membe ndo zinatuletea maendeleo nchi ? Mwacheni Baba jeska apge kazi hyo exposure ya kimataifa ya membe wala haitusaidii ktu wa tanzania.
 
Back
Top Bottom