Sifa inayopata Rwanda Msumbiji ilibidi tuwe tunapewa Tanzania kama Jeshi letu lingeenda na kasi ya Mwl. Nyerere?

jiwekuu770

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
2,247
1,633
Miaka 1960-1980 jeshi la Tanzania lilikua ni tishio Africa.

Kwa East Africa ndyo lilikua kinara kwa ubora na kuogopeka kijeshi?

Vita ya tz na Ug ililipa headline nyingine achilia mbali kushiri ukombozi katka nchi zingine.

Lakin sasa zama zimebadilika
Uganda ya sasa si ile
Kenya nayo imepiga hatua

Kuibuka kwa Ugaidi nchi ya Msumbiji nilitegemea Budget ya jeshi iongezeke mara dufu ikifuatiwa na ulinzi wa kisasa ikiwa ni pamoja na kununuliwa kwa vifaa vya kisasa kutoka Israel, US na Russia.

Cha ajabu nchi kama Rwanda ndyo ina trendi kwene kudhibiti hao magaidi ambao hawako hata karibu nayo.

Rwanda imekua kinara wa Ukanda wa maziwa makuu, kanchi kadogo Rwanda kamekua n tishio kwa intelligensia na Kijeshi.

Kamechukua Title ya Tanzania ya nyerere miaka ile

Je, sisi tunaenda taaratibu kuwa NEXT DRC?

Mimi
Jiwekuu770
 
Mura mbuya tata!!! wamepungua sana jeshini! wamebaki kuuza mayai tu mjini, huko jeshini mmebana sana!!! sababu ya kuendekeza ulaji!! si hkn vita mura!! sasa kila mtu anataka jeshi akale officers Mess!!

warembo wa kiume, waosha kucha siku hizi weeengi sana huko!! na ikitokea vita tutachakazwa mpaka mlie poo!

wanacho mind kutovaa sare za jeshi tu baaasi!
 
Yaani tutenge bajeti kubwa ili kupigana na magaidi waliopo msumbuji na ambao hawana effects kubwa kwetu??!!

Una akili sawasawa kweli??

Mkuu!

Nadhani unaelewa kua hilo kundi ndo lilitaka kuweka ngome Kibiti enzi za utawala wa kikwete na likaja kusambaratishwa JPM!!

Aidha unajua ni idadi kiasi gan ya wahanga waliokufa mtwara na kibit kwa ajili ya ugaidi?

Nadhani kuna namna

Unaona ubahili wa hela n bora kuliko maisha ya watu ikiwemo ww mwenyewe
 
Kuruhusu wanasiasa wa ccm ku infilitrate kwenye utumishi wa umma!

Leo hii DED ni kada wa ccm, mtendaji wa kata au kijiji ni makada wa ccm..polisi ni kada wa ccm!

Huko jeshini na TISS wenda wamejazana makada ndio maana ufanisi unashuka!

lakini si sababu ya kufanya vibaya !! China every aspect of life is governed by ccp n ndyo hiyo inampeleka kuwa world power
 
Rwanda imefadhiliwa na mfaransa kulinda masla yake kule msumbiji kumbukq kuna TOTAL kampuni ya mafuta pale Cabo de Gado

Ni kweli ,,,…
lakini mikakati ya kiulinzi haiko bayana hata bajet ya ulinzi kuongezeka
 
Miaka 1960-1980 jeshi la Tanzania lilikua ni tishio Africa.

Kwa East Africa ndyo lilikua kinara kwa ubora na kuogopeka kijeshi?

Vita ya tz na Ug ililipa headline nyingine achilia mbali kushiri ukombozi katka nchi zingine.

Lakin sasa zama zimebadilika
Uganda ya sasa si ile
Kenya nayo imepiga hatua

Kuibuka kwa Ugaidi nchi ya Msumbiji nilitegemea Budget ya jeshi iongezeke mara dufu ikifuatiwa na ulinzi wa kisasa ikiwa ni pamoja na kununuliwa kwa vifaa vya kisasa kutoka Israel, US na Russia.

Cha ajabu nchi kama Rwanda ndyo ina trendi kwene kudhibiti hao magaidi ambao hawako hata karibu nayo.

Rwanda imekua kinara wa Ukanda wa maziwa makuu, kanchi kadogo Rwanda kamekua n tishio kwa intelligensia na Kijeshi.

Kamechukua Title ya Tanzania ya nyerere miaka ile

Je, sisi tunaenda taaratibu kuwa NEXT DRC?

Mimi
Jiwekuu770
Uko tayari kiasi gani kukatwa ziada kwenye tozo na kodi ili kugharamia hiyo vita? Uko tayari kiasi gani kuona tishio la hao wana Mgambo kuja mji kama Dar kulipua majengo kama mbinu yao ya kulipa kisasi, kama yakutayo wakenya? Tusiropoke tu
 
Mko tayari kiasi gani kupitia yale nchi ilipitia baada ya vita vya Kagera, yale ya umaskini wa kutupa maana mambo ya maana na msingi yote yalisimama kisa vita.

Mko tayari kiasi gani kuhimili shida hizo zote? Ili tupate misifa tu, sifa tu, yani sifa hizi hizi sifa

Si bora tubaki na sifa za royal tour
 
Kuna rika mtu ukifikia unapaswa kujua kuwa huwezi beba sifa zoooooote duniani,

Na kwamba muhimu zaidi ni kuangalia mambo yako ya msingi
 
Kumbuka Msumbiji na Rwanda hazijapakana, ni ngumu kwa wanamgambo hao kuvuka mipaka kushambulia huko, sisi tumepakana na Msumbiji, lazima hiyo vita tuingie kiakili.

Na si kweli kuwa hakuna makubwa jeshi letu inafanya huko, naamini ina makubwa inafanya ila halisemi kama tu ambavyo lilimalizana na kibiti kimyakimya,

Kufanya mambo hadharani sana ni kuvuta attention ya hao wavamizi kwa nchi yetu, kitu ambacho hatutaki

Binafsi sitaki niwashe aljazeera ama BBC halafu vichwa vya habari viwe ni wavamizi wa Msumbiji wavamia kulipa kisasi tz,

Hivyo serikali na jeshi wanajua wanachofanya
 
Kwa hiyo tunaogopa magaidi?
 
Uliyeandika uzi utakuta unaishi kwa mume wa dada yako umeshakula na kutazama tamthilia ITV ukaamua uandike huu ushuzi. Uwe na adabu kwa jeshi linalohakikisha unakuwa salama hapo kwa shemeji yako.
 
Back
Top Bottom