Sifa 7 za mwanamke mpambanaji

Kilenzi _Jr

JF-Expert Member
Sep 10, 2021
306
1,000
Dunia ingekuwa wapi leo bila mwanamke? Wanawake wana nafasi kubwa katika jamii yetu ya Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla. Mwanamuziki Beyoncé wa marekani aliwahi kuimba akisema wanawake wanakimbiza/wanaongoza dunia (Runs the World (Girls)

Ingawa baadhi ya wanawake wengi hawajapata ujasiri wa kuishi kufuatana na matakwa yao, wapo wengine wanaoishi na kutimiza ndoto zao katika maisha yao kila siku

Mwanamke mpambanaji ni mwanamke imara na anayeijua nguvu iliyo ndani yake ya kupambana na kukabiliana na changamoto katika nyanja mbalimbali za maisha ili kutimiza malengo yake. Hizi ni sifa za mwanamke mpambanaji:

1.Jasiri
jasiri mwanamke mpambanaji

Mwanamke mpambanaji ni jasiri anaona nafasi za kujiendeleza na kuzinyakua haraka. Mwanamke jasiri haogopi kushindwa na changamoto zilizo mbele yake, siku zote huchagua kuzikabili. Wanawake wengi majasiri wamefanikiwa kuinua uchumi wao na kuzisimamia familia zao, wakati mwingine bila hata ya msaada wa mwanaume. Ni wajasiriamali. Ni wanawake wenye nyadhifa za uongozi wakifanya kazi na kuleta maendeleo kwa bidii.

2.Hufanya Maamuzi Sahihi
Mwanamke mpambanaji haogopi kufanya maamuzi sahihi juu ya maisha yake na kufuatilia mipango yake. Hupokea maoni chanya na kuamua pia kupuuzia maoni ya watu wengine yasiyo na tija ama ambayo hayamsaidii kwenda mbele na kutimiza ndoto zake. Kutokana ma mapito yake, mwanamke mpambanaji hufanya mamuzi sahihi juu ya jinsi gani ya kubadili mwenendo wa maisha yake ili kujiboresha siku zote.

3.Ana Ndoto
ana ndoto mwanamke mpambanaji

Mwanamke mpambanaji ana ndoto za kuwa mtu fulani ama kufikia malengo fulani. Haogopi kuwa tofauti na mategemeo ya wengine. Pia anajua ni njia gani za kufuata ili kutimiza ndoto zake. Anajua umuhimu wa kuwa makini na kila nafasi inayopita mbele yake inayoahidi mafanikio. Ndoto zake ni muhimu kwake na huzipa kipaumbele.

4.Mbunifu
Mwanamke mpambanaji ni mbunifu kila wakati. Wanawake wamebarikiwa uwezo wa kufanya mambo mengi katika muda mchache. Hivyo basi, mwanamke mpambanaji anajua jinsi ya kujigawa katika kazi, kuongeza ujuzi na kujaribu mambo mbalimabli ili apate matokeo sahihi katka mambo anayoyafanya.

5.Anajitegemea
Mwanamke mpambanaji anajua kujisimamia katika mambo mbalimbali maishani. Hii haimaanishi mpambanaji hahitaji msaada kwa wengine bali anajua msaada peke yake hautoshi. Anafahamu kuwa lazima ajiongeze maana kuna mambo mengi anayohitaji kutimiza. Hivyo basi, anaelewa nafasi yake katika maendeleo yake na hata ya familia yake.

6.Hujitoa
hujitoa mwanamke mpambanaji

Mwanamke mpambanaji anatambua mchango wake katika jamii inayomzunguka. ujitoa kwasababu ni jambo sahihi na si kwa ajili ya kupata umaarufu ama cheo. Mwanamke mpambanaji pia anajua thamani ya kuwainua wengine na kuwatia moyo wale wanaomwangalia. Siku zote, anajitambua na kutambua mchango wake katika jamii yake.

7.Anatia Hamasa
Mwanamke mpambanaji huhamasisha jamii yake kuwa bora zaidi kupitia juhudi zake na mafinikio yake huhamasisha watu wengine kuongeza jitihada katika shughuli na mambo mbalimbali. Mpambanaji sio mchoyo wa maarifa, na hupenda kuona wengine wakifanikiwa kupitia yeye.
 
Madame B

JF-Expert Member
Apr 9, 2012
28,878
2,000
Pia usisahau jamii inayomzunguka nayo inachangia kufikia malengo yake.
Mwanamke anapaswa aangalie ni aina ipi ya jamii inayomzunguka ambayo anaishi nayo.
Kuna jamii zingine, zinapelekea tunakosa utu na uthubutu.
Asante.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,742
2,000
In short we called this type of a woman a WIFE MATERIAL.
Dunia ingekuwa wapi leo bila mwanamke? Wanawake wana nafasi kubwa katika jamii yetu ya Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla. Mwanamuziki Beyoncé wa marekani aliwahi kuimba akisema wanawake wanakimbiza/wanaongoza dunia (Runs the World (Girls)

Ingawa baadhi ya wanawake wengi hawajapata ujasiri wa kuishi kufuatana na matakwa yao, wapo wengine wanaoishi na kutimiza ndoto zao katika maisha yao kila siku

Mwanamke mpambanaji ni mwanamke imara na anayeijua nguvu iliyo ndani yake ya kupambana na kukabiliana na changamoto katika nyanja mbalimbali za maisha ili kutimiza malengo yake. Hizi ni sifa za mwanamke mpambanaji:

1.Jasiri
jasiri mwanamke mpambanaji

Mwanamke mpambanaji ni jasiri anaona nafasi za kujiendeleza na kuzinyakua haraka. Mwanamke jasiri haogopi kushindwa na changamoto zilizo mbele yake, siku zote huchagua kuzikabili. Wanawake wengi majasiri wamefanikiwa kuinua uchumi wao na kuzisimamia familia zao, wakati mwingine bila hata ya msaada wa mwanaume. Ni wajasiriamali. Ni wanawake wenye nyadhifa za uongozi wakifanya kazi na kuleta maendeleo kwa bidii.

2.Hufanya Maamuzi Sahihi
Mwanamke mpambanaji haogopi kufanya maamuzi sahihi juu ya maisha yake na kufuatilia mipango yake. Hupokea maoni chanya na kuamua pia kupuuzia maoni ya watu wengine yasiyo na tija ama ambayo hayamsaidii kwenda mbele na kutimiza ndoto zake. Kutokana ma mapito yake, mwanamke mpambanaji hufanya mamuzi sahihi juu ya jinsi gani ya kubadili mwenendo wa maisha yake ili kujiboresha siku zote.

3.Ana Ndoto
ana ndoto mwanamke mpambanaji

Mwanamke mpambanaji ana ndoto za kuwa mtu fulani ama kufikia malengo fulani. Haogopi kuwa tofauti na mategemeo ya wengine. Pia anajua ni njia gani za kufuata ili kutimiza ndoto zake. Anajua umuhimu wa kuwa makini na kila nafasi inayopita mbele yake inayoahidi mafanikio. Ndoto zake ni muhimu kwake na huzipa kipaumbele.

4.Mbunifu
Mwanamke mpambanaji ni mbunifu kila wakati. Wanawake wamebarikiwa uwezo wa kufanya mambo mengi katika muda mchache. Hivyo basi, mwanamke mpambanaji anajua jinsi ya kujigawa katika kazi, kuongeza ujuzi na kujaribu mambo mbalimabli ili apate matokeo sahihi katka mambo anayoyafanya.

5.Anajitegemea
Mwanamke mpambanaji anajua kujisimamia katika mambo mbalimbali maishani. Hii haimaanishi mpambanaji hahitaji msaada kwa wengine bali anajua msaada peke yake hautoshi. Anafahamu kuwa lazima ajiongeze maana kuna mambo mengi anayohitaji kutimiza. Hivyo basi, anaelewa nafasi yake katika maendeleo yake na hata ya familia yake.

6.Hujitoa
hujitoa mwanamke mpambanaji

Mwanamke mpambanaji anatambua mchango wake katika jamii inayomzunguka. ujitoa kwasababu ni jambo sahihi na si kwa ajili ya kupata umaarufu ama cheo. Mwanamke mpambanaji pia anajua thamani ya kuwainua wengine na kuwatia moyo wale wanaomwangalia. Siku zote, anajitambua na kutambua mchango wake katika jamii yake.

7.Anatia Hamasa
Mwanamke mpambanaji huhamasisha jamii yake kuwa bora zaidi kupitia juhudi zake na mafinikio yake huhamasisha watu wengine kuongeza jitihada katika shughuli na mambo mbalimbali. Mpambanaji sio mchoyo wa maarifa, na hupenda kuona wengine wakifanikiwa kupitia yeye.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom