Sierra Leone yatanganza hali ya dharura kwenye maswala ya Ubakaji

Display Name

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
410
500
Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Sierra Leone(Julius Maada Bio) amesema "Ni lazima tisimame na kishughulia kwa haraka tatizo hili"

Rais huyo wa Sierra Leone amesema kikosi cha maaluma cha polisi kimeundwa ili kufuatilia/kuchunguza tuhuma hizo kwa haraka na pia kitengo maalimu katika mahakama kimeumdwa ili kushughulikia kesi hizo kwa haraka zaidi.

Ameahidi pia kwa waathirika wote wa vitendo vya ubakaji watapata matibabu bure hadi watakapopona lakini pia yeyote atakayepatikana na hatia ya kubaka watoto wadogo atafungwa kifungo cha maisha.

Uamuzi huu umefikiwa baada ya matukio mengi ya ubakaji na unyanyasaji wa kimapenzi kuripotiwa. Rais Bio amesema "Kila mwezi mamia ya kesi za ubakaji na unyanyasaji wa kimapenzi umekuwa ukiripotiwa hapa nchini. Ukatili huu umekuwa ukifanywa kwa wanawake wetu na watoto wetu"

Katika kesi ambazo zimeripotiwa za Unabakaji na unyanyasaji wa kimapenzi asilimia 75(75%) zimehusisha watoto wenye umri chini ya miaka 15.

Source: Aljazeera:
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom