Sielewi nimepatwa na nini mwenzenu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sielewi nimepatwa na nini mwenzenu...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sajenti, May 13, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Niko katika mahusiano ya kimapenzi na mdada mmoja kwa takribani mwaka mmoja na nusu sasa. Na kwa kweli tangu niwe na huyu mpenzi wangu hatujawahi kutatizana sana na pia ni mtu tunayependana sana. Ndugu na jamaa kwa pande zote wanaelewa uhusiano wetu. Kutokana na mipangilio yangu nilipanga kumu-engage huyu mpenzi wangu tarehe 24 July mwaka huu tena kwa kum-surprise, nilipanga tarehe hii kwa makusudi kabisa kwani kwangu mimi ni tarehe inayobeba matukio mazito na muhimu katika maisha yangu. Lakini kwa muda wa mwezi mmoja sasa nimekuwa katika dilema kiasi kwamba nahisi kama ahadi ya kumu-engage huyu mpenzi wangu naweza kuifuta muda wowote.

  Sababu kubwa ni kuwa nimekutana na binti mwingine ambaye sina jinsi ya kumuelezea hapa nikaeleweka.Tulikutana katika mkutano wa kikazi Arusha na nikajikuta navutika kwake. Kifupi kwa vigezo vyangu ni mzuri wa sura na umbo, yuko hot kimapenzi nakosa wa kumfananisha naye, ana akili ya maisha ni mshauri wa aina yake. Kifupi katika muda mfupi niliokuwa naye amenifanya nipagawe.

  Kumbuka nina mtoto wa kike wa miaka 9 niliyezaa na mwanamke mwingine yuko shule grade 4 hapa Dar na huyu dada amenishawishi tumtafutie shule moja ya boarding Arusha na hata ada yuko tayari kulipa kwani kwa habari nilizopata hiyo shule hata fee yake ni ndefu pia. Najikuta nayumba sana ingawa mchumba wangu mtarajiwa bado hajagundua kinachoendelea lakini nahisi muda si mrefu yatasanuka tu. Maana kinachonitokea ni kama napoteza hisia kwa huyu mchumba mtarajiwa. Mimi ni mtu wa misimamo sana lakini katika hili najiona nimepigwa bao sielewi ni mapenzi tu au kuna zaidi ndani yake. ameniomba kama niko tayari kuwa naye kwa karibu afanye mpango wa kupata uhamisho wa kikazi ili aje huku Dar...sijampa jibu ingawa ndio hivyo simu kila siku kutwa mara 4, are you ok sweet, umekula nini leo mchana, umeshalala au uko wapi unafanya nini na nani? Ili mradi mambo kedekede..
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  huh! samahani ila kama wewe mtu wa msimamo ilikuwaje ukalala nae hapo mwanzo huyu binti mpya!

  nashindwa kuwaelewa watu wanaojibandika vyeo vya uongo.............na the way unavyoongelea kama kumcheat huyo unaemuita mchumba mtarajiwa umezowea
   
 3. bht

  bht JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  huna msimamo..mpaka hapo
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu thanks for asking

  nasikitika kwamba jukwaa letu la mahusiano, jamii na mapenzi limeingiliwa na watu wanaotaka kuhalalisha kufanya-fanya mapenzi tu.... mwanzo nilikua napenda kutoa ushauri lakini kwa sasa naona kama inakua too much

  sioni mtu akija kuuliza shule nzuri, vyuo au kozi nzuri, namna ya kupenda zaidi, bali sasa ni kila anakuja kusema jinsi alivyotembea nje ya mstari na anaomba tumhalalishie

  its getting worse
   
 5. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  SAJENTIIIIIII................Unataka kufanya kosa kubwa sana katika maisha yako na utalijutia milele! Take my words! Mchumbie mchumba wako haraka iwezekanavyo na usisubiri mambo ya July 24. Hayo ni majaribu tu, na huyo binti mpya ana kasi sana na ndicho kinachotia shaka. Pia wakati wa kufanya maamuzi mazito kama kuoa au kuolewa, watu hukumbwa na vishawishi vingi ambavyo wala huwa hawakuvitegemea na wala hata hujui vimetoka wapi.

  Kama una sikio la kusikia na unisikie sasa.....BETTER THE DEVIL YOU KNOW THAN AN ANGEL YOU DON'T KNOW!
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks sis!
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  May 13, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  Humu siku hizi kuna stori za ajabu ajabu na za kila aina. Kweli kila mtu na maisha yake.
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  De Nevo..............watu wamekubwa na jini la kuporomosha maadili.

  nilifikiri angekuja hapa kutuambia namna anavyojuta jinsi alivyomkosea mchumba wake kwa kulala na mwanamke siku moja ,..............anakuja hapa kutuomba ushauri wa kumcheat mtu! duh ...

  tunakoelekea siko jamani
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  May 13, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sajenti....pole kaka but kumbuka wanawake wazuri wanazaliwa kila siku. Sasa utawaengade wangapi wakati ukiona mwenye uvuto zaidi unapoteza direction?

  nakushauri:
  1. Kwa vile hujamwambia mpenzio wa ukweli unamuengage- kaa chini tafakari tamu na chungu zake
  2. Linganisha tamu na chungu za mwenzio na huyo mgeni
  3. Usichukue maamuzi ya haraka kwani mpenzi mpya hujamjua vema
   
 10. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Kitu kikubwa ni kuridhika, wazuri hawaishi..leo huyo binti wa Arusha utamuona almasi, kesho unaweza kukutana na mzuri zaidi kitabia na umbo sijui utafanyaje...wewe fanya tu uamuzi wako mana ndiye utakayeishi kwenye maisha yako ya ndoa..ila ukijicommit kwa mtu funga milango mingine ya tamaa..
   
 11. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mara yamwisho kwenda angaza ilikuwa ni lini?? maana mtu kwenye mkutano tu umeshajua yuko HOT!!

  yaelekea ww ni walewale sketi isipite mbele yake wataka kuona imepindiwa uzi wa rangi gani halafu unajiita mtu wa msimamo ! kwanza nikuulize una msimao upi wakuangalia sketi gani imekupitia au.....
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  inatia shaka sana hii tabia aisee
   
 13. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #13
  May 13, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Nadhani jama ameshindwa kuwa human! careless heart....

  Man mchumbie huyo GF wako,kwanza huyo dem mpya anajua una mchumba? Yaani ni mrahisi kweli kweli.Na wewe unajiskia comfortable tu?
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mapenzi ya kichina hayo ndugu yangu... nadhani mengine tunahitaji staha tu!
   
 15. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #15
  May 13, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Yeye anajua kabisa matokeo yake halafu anataka tumshauri. Wabongo bana , ukimwwuliza swali naye anajibu kwa swali. FYI we do not deal with "obvious" .
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  May 13, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Pole sana Sajenti -huna msimamo
  umempenda huyo dada kisa ni mzuri ..ana pesa kaahidi kukusomeshea mwanao ..usiache mbachao kwa msala upitao.Umewezaje kuzijua tabia za huyu dada mpya kwa kipindi kifupi hiki?
  atatokea mwingine mzuri zaidi ya huyo itakuwaje??
   
 17. RR

  RR JF-Expert Member

  #17
  May 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Mkuu sitashangaa kesho mtu akkibuka na bandiko la kutaka kuungwa mkono ili aolewe na baba yake au amwoe mamie....
  Ngoja tuone!
   
 18. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #18
  May 13, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Afadhali umesema na umenifungua macho; unajuwa mie nilijiunga na JF wakati kuna wimbi kama hili na mpaka leo uliposema nilidhani hii ndiyo kazi mahususi ya hili jukwaa! Do asante mkuu
   
 19. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #19
  May 13, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Sajent go take a life MSIMAMO WAKO NI KUMEGA kila anayekuvutia; kweli nimeuona hata mimi; na hayo mambo yenu ya kuiga; ivi mtoto wa 9 yrs unamfukuzia boarding ili akajifunze maadili ya nani; wakirudi wasagaji huko mnawabebea mabango; hammuoni serikali imeanzia kidato cha kwanza?
   
 20. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #20
  May 13, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,996
  Trophy Points: 280
  Mke mwema mtu hupewa na Bwana, hapo kujudge ni ngumu sana, wewe sio wakwanza kufanya hayo mambo kuna watu wanafikia mpaka stage ya uchumba na ndoa inashindikana, JARIBU KUWA NEUTRAL, NA KUFANYA ANALYSIS ZISIZOKUWA BIASED KWA UPANDE WOWOTE NA KISHA FATA MOYO WAKO KATIKA HAKI NA UKWELI, UWEZI KUOA KWA SABABU UMEISHI NA MTU MUDA MREFU NA PIA HUWEZI KUOA KWA SABBABU MWANAMKE ANA AKILI YA MAENDELEO NA ATAKUSOMESHEA MTOTO
   
Loading...