Sielewi kwanini bado Andrew Chenge na Nimrod Mkono hawajashitakiwa suala la IPTL

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,314
24,177
Hawa viongozi waandamizi humu nchi wamehusika sana kwa nyadhifa zao katika suala la umeme wa IPTL na madini.

Tumeona kina Kitilya, Mramba, Mgonja na wengine wakifikishwa kwa Pilato kujibu mashitaka kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Majuzi TANESCO(soma Serikali), wamepigwa faini ya 1Trillion kutokana na mikataba iliyoridhiwa na Nimrod Mkono. https://allafrica.com/stories/201501051846.html

Kwa upande wake, pamoja na machungu yote ya makenikia, Andrew Chenge ana uhusika.

Hata idara ya Serious Crimes ya Uingereza ilibaini Chenge ana $1million huko benki za nje.Andrew Chenge - Wikipedia

Pamoja na juhudi zote za Serikali, hawa mabwana wanapeta tu.
 
Huyo Chenge ndiyo Mwanasheria Wanayemtegemea CCM..na Ndiye aliyefanikisha baadhi ya Sheria mbovu Kuinufaisha CCM na Yeye binafsi..
Hata katika Marekebisho ya Katiba yeye alisaidia kukwamisha Mchakato ili CCM waendelee kufaidika.
Itahitaji Kuitoa CCM kwanza Madarakani halafu tuyashughulikie haya Majizi..
 
Kusubiri Chenge afungwe kwenye Utawala wa CCM ni kuota Unapaa kwenda Juu pasi mabawa! Joka la Makengeze he is Intelligent ever! Sahau Utawala kama wa Jiwe kumfunga, labda kwa Ubabe. Ila Andrea Chenge anajua alichokifanya, ni mueleve kama Nyoka!
 
Back
Top Bottom