Sielewi kama kweli napendwa

Feb 15, 2010
5
0
habari wana jamii,
mimi ni binti wa miaka 21 nimekua katika mahusiano ndani ya miaka miwili ila jambo ambalo sielewi kwa huyu mwenzangu ni tabia yake.
kabla nimewahi kumfumania zaidi ya mara moja kama hiyo haitoshi kanilaza kitanda kimoja na mwanamke,lakini anadai ananipenda mara tu niamuapo kutengana nae tena bila kumwambi kama naachia ngazi kwan nisitishapo mawasiliano yeye huja kwa spidi ya ajabu.NAOMBENI USHAURI WENU
 
pole sana,
hapo kama una uhakika ana kuchezea ni vyema uamue moja. hiyo mara nje mara ndani itaku-cost! amua kama ni kuachana nae au ukubali tabia yake hiyo.
 
miaka 21!!!!!!!!

shule umemaliza, labda anakuona bado mtoto ndo maana anakuchezea akili.

nakushjauri urudi shule, we bado mdogo sana usijione una vichuchu ukadhanai umekuwa mkubwa, zingatia masomo kwanza. achana na mapenzi ...................
 
Inaelekea huyu ni jamaa wa kwanza kwako ama huna uzoefu kabisa na anautumia uchanga wako kukuletea maafa!

Kimbia haraka na usihirikiane naye TENA!
 
Napoamua anadai nitamtia aibu kwa ndugu zake kwani tayari wananiofahamu


Hiyo ni danganya toto hamna cha ndugu wala nini hapo; kwanza wewe nayeye mna miadi ya kuwa pamoja maisha yenu yote I mean ndoa n.k?

Huyo anakumega tu hana mpango wowote na hapo kwako kageuza mapoozeo akikosa hukooo anajua akirudi utampa tu!:mad:
 
eeeh binti sijui hata niseme nini hapa ...
21 yrs old umelazwa kitanda kimoja na mke mwenza
 
Miaka 21,umekua na mtu kwenye mahusiano sasa kwa miaka miwili,it means ulianza mahusiano na umri wa miaka 19, we mdada unakimbila nini? mbona hayo mambo yapo tu utayakuta unaharakia nini? Kwa taarifa yako sasa huyo jamaa anakupotezea muda na inavyoonekana una weakness ambazo ndio anazitumia,unasema kwamba amesema kwamba itakuwaje mkiachana na ndugu zake wanakufahamu hivi ukifikiri hiyo ni point ya maana? anakuzuga,anakutumia,na mwisho wa siku rafiki utujutia huo muda unaopoteza,kama unasoma soma kwanza acha kuchanganya mambo mawili kwa wakati mmoja,kumbuka wahenga walisema mshika mbili................................................
 
pole sana dada ,
mm nakushauri achananae huyo hakupendi kabisa ,
kama kweli anakupenda asingekulaza kitanda kimoja na mwanamke mwenzako
 
nadhani jamaa yako atakuwa anakucheka sana kimoyo moyo, hata kijiweni kwa washkaji zake atakuwa anakuponda sana tu. unaonekana mdhaifu sana ktk haya mambo kama umri wako ulivyo mdogo. jamaa anakupotezea muda tu, anakufanya kibrudisho, ZINDUKA achana naye, jali shule kwanza ukimaliza shule utawapanga tu na WEWE maana siku hizi kuna wanaume wanapenda sana kulelewa/kuolewa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom