Sielewi fukuza fukuza anayofanya JK CCM

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,445
Hii fukuza fukuza ya watu waliokisaliti Chama wakati wa Uchaguzi imekengwa kweli kukiimarisha Chama au ni kukidhuru Chama kwa Uchaguzi wa 2020?
 
Alianza Manyara siku si nyingi ofisi za chama zikashika moto ,Kigoma kawatimua kina Christopher Chiza na hivi Zanzibar wamekalia kuti kavu ngoja tuone
 
Alianza Manyara siku si nyingi ofisi za chama zikashika moto ,Kigoma kawatimua kina Christopher Chiza na hivi Zanzibar wamekalia kuti kavu ngoja tuone
Waliokuwa viongozi waandamizi wa CCM na wakafukuzwa na mwenyekiti,watakuja kuwa MWIBA MKALI SANA kwa serikali ya Magufuli na CCM kwaujumla, tena keshokutwa tu. Kwanza tusubiri ya Christopher Chiza.
Yaani watu wanapenda kubebana hata kwenye usaliti??
Usaliti haufai hata kidogo.

Ili kuacha unafiki mada hii ilitakiwa ianzie kwa kuwaambia Chadema wamrudishe Zzk na CUF wamsamehe Hamad Rashid....
Hapo mtakuwa mmebalansi kidogo.
 
Itakuwa wale waliomwangusha alipopeleka jina la mgombea wake. Huyu anakuwa driven sana na kisasi. Does he care what happens to CCM? I doubt it!
 
Alianza Manyara siku si nyingi ofisi za chama zikashika moto ,Kigoma kawatimua kina Christopher Chiza na hivi Zanzibar wamekalia kuti kavu ngoja tuone
Zanzibar amfukuze karume......yeye huyu hapendi uoevu na ndie alieleta umoja kwa Wazanzibari hivyo anahatarisha nguvu za ccm ambazo zimekita kuwagawa ili tuwatawale.
Bora afukuzee tu
 
Ni lini Andrew Nyerere umekuwa na mapenzi na CCM? Rais wetu Magufuli alimuomba Mwenyekiti wa CCM asafiche chama kabla hajakabidhiwa. Ni utekelezaji wa agizo la Rais. Wasaliti hawavumiliwi kotekote. Mbowe jana amesema kuwa hatakuwa na hata chembe ya uvumilivu kwa wasaliti wa chama. Sasa unataka CCM ndo iwalee then waje watusumbue?
 
Itakuwa wale waliomwangusha alipopeleka jina la mgombea wake. Huyu anakuwa driven sana na kisasi. Does he care what happens to CCM? I doubt it!
Poleni sana. Hao wanaoshuguulikiwa wanajua makosa yao. CCM ina hazina kubwa ya Uongozi
 
Hii fukuza fukuza ya watu waliokisaliti Chama wakati wa Uchaguzi imekengwa kweli kukiimarisha Chama au ni kukidhuru Chama kwa Uchaguzi wa 2020?
Anachoshindwa kuelewa huyo JK, ni kuwa Yeye ndo sababu ya wananchi wengi kuichukia ccm na wala si hao anaowaita wasaliti...iko hivi

Ni kwa sababu ya utawala wake mbovu na dhaifu ambao haukuzingatia matakwa na ustawi wa raia wa chini ndipo hapo watu wakaichoka ccm...na hakika miezi minne kabla ya uchaguzi wa mwaka jana, kila mtu hata asiye na elimu wala uelewa wa mambo ya siasa..alikuwa hatari kabisa kuisikia ccm na hii ilipeleka chama kupoteza wafuasi na wapenzi kwa wingi...

Lakini pia nguvu ya Lowassa, inajulikana wazi ni miongoni mwa mambo yaliyochangia chama kupata wakati mgumu mbele ya wananchi..sasa unapoanzisha harakati za fukuzafukuza ndani ya chama kwa kisingizio kwamba ni wasaliti...ni muhimu pia kuitazama nafasi na mchango wa mwenyekiti wa chama - taifa umekifikisha wapi chama chenyewe.

Kikwete anajua fika ya kwamba kama si kutumia ubabe, dola na ile tume yao ya uchaguzi, ni wazi Leo ccm ingekuwa chama kikuu cha upinzani....(wanaccm mnaweza kubisha, lakini huo ndo ukweli)..

Kwa mtazamo wangu, kabla hamjawafukuza hao mliopanga kuwafukuza, anza na mwenyekiti kwanza.
 
Yaani watu wanapenda kubebana hata kwenye usaliti??
Usaliti haufai hata kidogo.

Ili kuacha unafiki mada hii ilitakiwa ianzie kwa kuwaambia Chadema wamrudishe Zzk na CUF wamsamehe Hamad Rashid....
Hapo mtakuwa mmebalansi kidogo.
Hapa kinachojadiliwa ni ccm
 
Back
Top Bottom