sidhani kama tulihitaji vyama vingi kwa sasa

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,277
1,121
binafsi nadhani tuliwahi sana kufanya maamuzi ua kuwa na vyama vingi kwani sioni faida zake zaidi ya hasara zifuatazo

(1) nchi imekuwa ikiingia hasara kuwadhibiti wapinzani pale wanapoamua kusimamia kitu wanachodhani ni sahihi, kuandaa chaguzi, pia hela hizi zingeweza kufanya shughuli nyingine za maendeleo

(2) wapinzani wana taarifa nyingi dhidi ya serikali ambazo zikiwekwa wazi zinapandikiza sumu ya chuki kwa vizazi na hii inaweza kuvurugu "amani" ambayo tumejuvunia kwa muda mrefu

(3) hebu jazia zingine
 
Hoja yako ya pili haina mashiko kwani wananchi wakiambiwa wizi unaofanywa Na watu waliopo serikalini in kupandikiza chuki? Kwa hiyo wasitajwe? Mkuu hapo umepotoka upinzani ni muhimu kwani ndio chombo pekee cha kufichua maovu
 
binafsi nadhani tuliwahi sana kufanya maamuzi ua kuwa na vyama vingi kwani sioni faida zake zaidi ya hasara zifuatazo

(1) nchi imekuwa ikiingia hasara kuwadhibiti wapinzani pale wanapoamua kusimamia kitu wanachodhani ni sahihi, kuandaa chaguzi, pia hela hizi zingeweza kufanya shughuli nyingine za maendeleo

(2) wapinzani wana taarifa nyingi dhidi ya serikali ambazo zikiwekwa wazi zinapandikiza sumu ya chuki kwa vizazi na hii inaweza kuvurugu "amani" ambayo tumejuvunia kwa muda mrefu

(3) hebu jazia zingine
1464666758308.jpg
 
serikali inatumia nguvu nyingi kudhoofisha upinzani badala ya kuleta maendeleo...Leo hii fedha zinazotumika kuficha " ukweli Wa baadhi ya mambo" zingeweza kuleta umeme hapa kijijini ninapoishi.
 
Nawashangaa sana baadhi ya watanzania km huyu aliyeta huu uzi
Sijui huwa wanafikiria nini
 
Kila MTU.ana Uhuru wa kutoa mawazo, huwezi jua labda katumwa ili aone watu watasema nini!
 
Nawashangaa sana baadhi ya watanzania km huyu aliyeta huu uzi
Sijui huwa wanafikiria nini
jana kuna mbunge wa chama chetu kileee kapigwa tanganyika jeki na askari kisha akafurumushwa nje ya bunge, halafu wabunge wa vyama vya upinzani wamezuiwa kuingia vikao vyote vilivyosalia sasa we unadhani kweli kulikuwa na umuhimu gani kuwa na hivi vyama?
 
Hawa wabunge wa ccm wakiomba bangi iruhusiwe makofi meeengi lakini zikiletwa HOJA za msingi *
 my friend bado sana kichwa kidogo kimepewa Jaz nzito
 
Back
Top Bottom