Side comments: Zitto in JF Exclusive Interview on the 22nd of November, 2012

Status
Not open for further replies.
Bila kumungunya kijana upeo anao.Mimi kwangu mtu mwenye kashfa za kimapenzi(NGONO).Hata awe mzuri vipi ni janga na hatari kwa taifa hili

Unalenga kusema nin mkuu..kashfa za kimapenzi wakat mwngine huja kama ajali au?
 
Kumbe Rais Kikwete huwa anasafiri mara nyingi na wabunge wa Chadema mie nilikuwa nadhani alikuwa anasafiri na Zitto peke yake. Zitto kaishasafiri mara mbili tu na Rais Kikwete.

Rais Kikwete ameishawahi kusafiri na Christina Lissu, walienda AUSTRALIA alisafiri na Grance Kiweli walienda nchi za SCANDINAVIA, alisafiri na Lucie Owenya walienda MAREKANI, Wenje naye alienda UTURUKI na Makamu wa Rais, Pinda naye anasafiri sana tu na wabunge wa Chadema.

Ni Kweli Mkuu na hata Dr. W Slaa hakuwahi katika Maisha yake KUTAKA Kugombea URAIS na Hata sasa hajatangaza. Je Ritz ulikuwa Unafahamu kwamba Mbowe naye alilazimishwa kugombea Urais?

Zitto Kabwe ni moja ya Fimbo ya Msonobari kwa Majangili na Magamba
 
Last edited by a moderator:
mimi siku zote huwa siwaelewi wenzangu ambao huwa wanafikiri mtu mzuri wa kugombea nafasi fulani ni lazima akubalike na watu wote,MH.ZITO namsifu kwa kuwa anafahamu demokrasia.Hivi mimi Temilugoda nikitangaza nia ya kugombea udiwani ama ubunge kata ya Ulanda na Jimbo la Kalenga mtawalia nitakuwa nimefanya kosa gani?Binafsi nawapinga sana ccm kwa mpango wao dhidi ya mh.ZITO na hili mh.ZITO alifanyie kazi,ccm wameandaa mpango wa kumsindikiza Zito katika nia yake,lakini mwaka 2015 watamgeuka kwa udini,watasema Muislam JMK amepita,sasa zamu ya mkristo.Kampeni hiyo itakuwa organized sana na ndiyo maana Wamewekwa wataalamu wa mikakati hiyo Kinana na Mangula,pia mwanajeshi msaafu Abdulrahaman Shimbo yumo katika timu ya kumgeukia Zito muda huo ambao mh.ZITO atakuwa ametangazwa kupeperusha bendera ya CDM.Kadhalika wameandaa mpango wa kumrubuni mh.ZITO kwa kueneza chuki endapo Mh.Zito hatashinda ndani ya CDM kuwa mgombea wa urais 2015 endapo katiba itaruhusu kwa umri wake.HIVYO MIMI NAONA KUNAHAJA YA PANDE 3 NDANI YA CDM KUWA TAYARI KWA MATOKEO YA NDANI YA CHAMA,KIJANA AKISHINDA BASI WAZEE WAZUNGUKE NCHI NZIMA KUMNADI KWA KUSHAMBULIA KONA ZOTE ZA NCHI KILA SIKU.

Maono ya wenye kuzitama hizi siasa wanasema kwamba zitto ni best candidate kwa chadema 2015,japo wapo wengi lakini uyu kimkakati ni mzuri,pia inaweza kufuta taswira ndan ya chadema kwamba ni chama cha kaskazini,na hata kuzika hoja mf za udini na propaganda zisizo na tija..inabidi zitto atumie muda mwingi kuimarisha chama akishirikia na na hawa viongoz wenzake wa cdm
 
FirstLady1 hauko mbali na muono wangu,

Mh. Zitto anaongea hoja zina ukweli fulani unaoshawishi...najaribu kufikiria iwapo Zitto anakuwa mgombea wa CDM hoja ya CCM juu ya ukristo na ukaskazini wa CDM inakuwa imekufa natural death.

CDM walitazame hili in the light of other attributes...CDM wajue 2015 is a do or die situation kwa hiyo waangalie maslahi mapana ya nchi hata kama kuna ambao tunadhani kuwa more presidential material

Hapo umesema mkuu! CHADEMA just think twise on t.
 
Nguruvi3, Jasusi,
..hata mimi sikuridhika na majibu ya Zitto kuhusu muungano.
..reading frm this interview sidhani kama yuko[zitto] current na madai na matamanio ya wa-ZNZ. sijui Zitto anapokutana na rafiki yake Ismail Jussa huwa wanazungumza kitu gani haswa.

..kulingana na maelezo ya Zitto, wa-ZNZ hawatakuwa na mamlaka na rasilimali zao[mafuta yao], na pia hawatakuwa wakitambulika kimataifa kwasababu masuala hayo yatakuwa chini ya Jamhuri ya muungano, na Raisi wa muungano.

..wa-ZNZ hawana haja tena na muungano, wanataka kuwa HURU, sasa it is about time Zitto na wenzake waheshimu matamanio hayo ya wa-ZNZ.
Zitto:
Kwanza kabisa niweke wazi kwamba mimi ni muumini wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Shirikisho la Afrika Mashariki na Mwanamajui wa Afrika (Pan Africanist). Lazima tuulinde muungano wetu kwa kuufanyia marekebisho makubwa sana ikiwemo kutoa uhuru mpana kwa pande za Muungano kufanya mambo yao. Muungano wenye Zanzibar na Tanganyika zenye Mamlaka ya kutosha (Kina ndugu Jussa wanasema Mamlaka kamili, ukisema mamlaka kamili ni sawa na kusema hakuna muungano). Baada ya utangulizi huu, ningependa muungano uwe na muundo gani?

Muundo wa Muungano uwe wa Nchi moja, Dola moja, Taifa moja. Serikali tatu. Kuwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye ni Mkuu wa nchi na Mtendaji kwenye masuala ya Muungano tu ambayo yatakuwa machache kama Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Sarafu, Sera za Fedha, Biashara ya Kimataifa, Kodi za kimataifa, usimamizi wa Rasilimali za Taifa, Uraia nk. Zanzibar watakuwa na Waziri Mkuu Mtendaji na Tanganyika hivyo hivyo. Chama chenye Wawakilishi wengi kwenye Baraza la Wawakilishi la Tanganyika kitatoa Waziri Mkuu na kuunda Serikali na Zanzibar hivyo hivyo. Bunge la Muungano litachagua wajumbe wake kutoka kwenye kila mkoa wa Tanzania wajumbe wawili. Maamuzi yataamuliwa kwa zaidi ya nusu ya kura kwa Wabunge kutoka kila upande wa Muungano.
Jasusi, jmushi1, Joka kuu. Nadhani katika hoja zinazokwepwa na wanasiasa hili la muungano ni mojawapo.

Ukimsoma Zitto utaona kuwa anatoa majibu yasiyoendana na hali halisi pengine tu kuwa mwana Majumuhi(Pan Africanism)

Zitto anasema kuwepo na serikali 3 na Rais wa jamhuri ya muungano atakayesimamia yafuatayo:

1. Mambo ya Nje.
Zitto amesahau kuwa ZNZ wanataka kiti UN, EAC na SADC, hata CHANEZAwanataka uanachama inter netball fed.
Huyu Rais wa muungano ataongoza nini ili WZN waridhike na kuacha madai yao?

2. Ulinzi na Usalama:
Hili ZNZ watalikubali kwasababu lina nafuu kwao,hawana bajeti hata senti tano
Tanganyika itajiuliza hivi kuna sababu gani za maana za kugharamia ulinzi na usalama wa ZNZ!!

3.Sarafu Moja:
ZNZ wanataka sarafu yao irudi tofauti na mtazamo wa Zitto

4. Sera za Fedha
ZNZ wanataka benki kuu yao irudi tofauti na mtazamo wa Zitto

5. Biashara ya kimataifa
ZNZ wanataka wajiunge na OIC, wasajili meli n.k
Huyu Rais wa muungano atawashawishiji nini kuhusu secular state wakati ZNZ inadai secularism ni Ukafir

6. Biashara za kimataifa
ZNZ inataka ifanye biashara zake bila ushirikiano na Tanganyika. Imesajili meli za Iran kwa jina la Tanzania, halafu
wanalalamika kuwa Tanzania inawawekea kauzibe na ndugu zao wa Iran.
Hapa kuna suluhu kama ndoto za Zitto zinavyoshawishi kweli!

7. Kodi za kimataifa
Hizi ZNZ watakubali kwasababu hata sasa hivi ndivyo wanavyofaidi. Mfano, wana ZMO, Kodi inalipa JMT.
Tanganyika itahoji ZNZ inaweka nini mezani ili kuleta uwiano bila kubebana?

8. Usimamizi wa Rasilimali wa Taifa
Zitto hajui kuwa ZNZ wamekimbiza mswada wa kudai mafuta na gesi si mambo ya muungano.
Hapa Tanganyika itamuuliza rais wa jamhuri, je umeme kama nishati kwanini uwe wa muungano?
Zitto alipaswa kujua kuwa kuna sheria mahusi za kulinda rasilimali za ZNZ na si Tanzania.

9. Uraia
Hiki ndicho WZN wankisubiri sana. Ukisikia kelele za muungano wa mkataba hakuna kingine isipokuwa Uraia.
Zitto anapaswa kufahamu kuwa kuna sheria ZNZ zisizomruhusu Mtanganyika kuajiriwa ZNZ, kumiliki ardhi.
Sasa tunataka uraia na ZNZ ili tunufaike na kitu gani hasa!!!!

Ukiangalia hoja hizo utaona Zitto ima haendi na wakati kuhusu suala la muungano, au ameamua kuwaridhisha Wazanzibar kwa maneno au hafahamu tatizo la muungano wa sasa kabisa.

Nadhani mapendekezo yake hakuwahi kuyajadili na mtu na hilo ni jambo la hatari sana kwa mtu anayeuangalia Urais.

Hatuwezi kuwa na muungano na ZNZ ambayo umimi ni uumini kwao na kibaya hawajui hasa matokeo ya madai yao.
Mathalani, ZNZ ikiwa na mamlaka kamili, Tanganyika itakuwa na mamlaka kamili na hapo muungano ZNZ inaolazimisha utakufa.

Sheria zilizopo ZNZ kuanzia ajira, umiliki wa ardhi, elimu n.k zitakuwa reflected na Tanganyika.
Waziri mkuu wa Tanganyika hatakubali vijana wake wazunguke wakitafuta ajira ili kuwafurahisha WZNZ waliojaa katika ajira huku bara. Wala hatakubali kutoa bajeti ili kuilinda ZNZ na wala hatakubali kodi za Matnaganyika zimlipie mzanzibar elimu n.k.

Madai ya ZNZ kuwa na sarafu yake ni ujinga maana trade yao na Tanganyika itakuwa ngumu.
In other words, WZNZ hawapo tayari kwa muungano ingawa wanafikiria sana muungano. Hawaangalii consequences za madai yao, wanachotaka ni muungano wenye ZNZ na mamlaka kamili. Lini utaungana na kubaki na mamlaka kamili?

Wanataka kutoka katika muungano wawe huru na wapumue, wakati huo huo wanataka muungano!! Think about this!
Mh Zitto hivi kweli huoni hapa mathematically tuna deal na unknown. Je unataka kurithisha adha hii kwa watoto wetu!

Nadiriki kusema Zitto hana hoja yoyote ya ushawishi kuhusu muungano. Inapaswa ajipange kwa hili na kulitazama kwa jicho mujarabu. Nimerudia tena majibu yake, nashawishika kusema hana hoja ya msingi! kwa hili hajaonyesha mtazamo!
 
Kipindi ni kizuri sana ila kimeletwa siku isiyo kabisa, ingefaa kama mahojiano haya yangefanyika j2.


J2 watu tunakuwa busy na mambo ya mungu pia kupumzika baada ya mambo mengi ya juma
Laptop pembeni kabisa ...kula ,kunywa ,kulala
 
Mzee Mwanakijiji wazee hamtakiwi huku mnaonekana mtapunguza kasi ya vijana kujitajirisha haraka.


Unajua hii hoja ya "Uongozi na Ujana" inabidi tuifunge sasa. Ni mojawapo ya hoja dhaifu sana ambazo zinaendekezwa. Inawezekana kuwa inasikika vizuri, ina mvuto sana na inashawishi hisia na akili ya baadhii ya watu lakini ikisogelewa kwa ukaribu siyo hoja nzuri kwa kweli na ni ya hatari ikikubaliwa.
 
"Kwa usalama wa nchi hii, CCM MUST GO in 2015" - ZZK

Hili ni la msingi sana kwa wanaoipenda nchi hii. I have been telling my friends about this. CCM wamechoka, hawana maono na wamepoteza dira. Hawawezi kujipanga wakiwa uwanjani....
 
Kuna jambo moja la hatari sana wanalohubiri CCM siku hizi, KUSHINDA CHAGUZI.
This has become their core motive, wanalofanya wakilala na kuamka ni kutaka kushinda chaguzi at any COST.

Nataka niamini kuwa lengo la chama cha siasa sio tu kushinda chaguzi lkn KULETA MABADILIKO CHANYA ktk maisha ya wananchi. CCM walipewa nafasi hawajafanya hayo lkn wanajipanga tena kushinda. ILI IWEJE?

HONESTLY, kwa yeyote, mwana CCM au asie na chama kama mimi, lazima we SHOULD THINK STRAIGHT FOR THE SAKE OF THIS COUNTRY, OUR KIDS....


CCM MUST GO...ENOUGH IS ENOUGH
 
Zitto anadai kuwa CCM wanaanza kuiga sera zao kuhusu suala la elimu ya bure. Kwa maoni yangu ili suala liwe swala la kitaifa. Na lijadiliwe kama vile tunajadili Jeshi la wananchi.

Ningependa tuwakabe hawa wanasiasa sio katika kutoa elimu bure, bali katika kukuza kiwango cha elimu. Je ni lini shule za msingi Tanzania zitafikia kiwango cha elimu kinachotolewa Mlimani Primary school au Olimpia? Asilimia 50% za shule zikitoa elimu ya kiwango cha shule hizo, inawezekana tukasahau huu mjadala.
 
Onyo: Watu hao hawawezi kummaliza Zitto kisiasa bila kuiathiri CHADEMA maana the imaage of Zitto is so intimately intertwined with CHADEMA that you couldn’t attack Zitto without jeopardizing the image of Chadema, and vice versa.

Wanaoeneza sumu hii hawana nia njema wala mapenzi na CHADEMA. Hawaelewi siasa. Wanafurahisha maadui wa CHADEMA. Maadui wanawachochea kwa kuwapa habari za uwongo na wao wanadhani watammaliza Zitto. Huwezi kummaliza Zitto bila kuiathiri CHADEMA. Hawatafanikiwa.
AshaDii

Usisahau kumwambi kuwa Kauli kama hizi kutoka kwake ni Kujidanganya, CDM ni taasisi, CDM sio mtu kama anavyotaka kutuaminisha/kupotosha na kauli hii, aondoke Mbowe, aondoke Slaa CDM will be there.
Hii kauli ukiiingalia kwa undani utagundua kuwa ni Vijembe kwa Viongozi wenzake wa CDM Zitto , Kaka CDM ni taasisi, hata ukiondoka kesho ukaenda CCM CDM Itaendelea kuwa mtoto wa kuotea masafa marefu
 
Last edited by a moderator:
Unajua hii hoja ya "Uongozi na Ujana" inabidi tuifunge sasa. Ni mojawapo ya hoja dhaifu sana ambazo zinaendekezwa. Inawezekana kuwa inasikika vizuri, ina mvuto sana na inashawishi hisia na akili ya baadhii ya watu lakini ikisogelewa kwa ukaribu siyo hoja nzuri kwa kweli na ni ya hatari ikikubaliwa.

The way I see it?

Hoja itajifunga yenyewe automatically baada ya 2015 baada ya kumaliza the specific purpose, THE GOAL itself!!
 
Mimi sikupata muda wa kuuliza swali,na nina mswali,pale mwanza diwa chabulani na mbunge wenje waliitisha harambee na yeye zito alikuwa awe mgeni rasmi ila baadae alichomoa pesa za harambee zilienda wapi ?na hiyo harambee ilikuwa na baraka za chama?
 
Je ni lini shule za msingi Tanzania zitafikia kiwango cha elimu kinachotolewa Mlimani Primary school au Olimpia? Asilimia 50% za shule zikitoa elimu ya kiwango cha shule hizo, inawezekana tukasahau huu mjadala.

Chifu, unazungumzia Shule ya Msingi Mlimani iliyo pale UDSM? Kama ndiyo, bila shaka unaongelea kiwango cha 1980s hadi mwanzoni mwa 1990. Pale shule ilipokuwa chini ya UDSM. Lakini baada ya kuwa chini ya serikali tu, matokeo yake yakaanza kuwa hovyo kabisa.
Ila nasikia kulikuwa na mpango wa kuirudisha chini ya UDSM, sijui umefikia wapi!
 
Unajua hii hoja ya "Uongozi na Ujana" inabidi tuifunge sasa. Ni mojawapo ya hoja dhaifu sana ambazo zinaendekezwa. Inawezekana kuwa inasikika vizuri, ina mvuto sana na inashawishi hisia na akili ya baadhii ya watu lakini ikisogelewa kwa ukaribu siyo hoja nzuri kwa kweli na ni ya hatari ikikubaliwa.
Baada ya miaka takribani 6 ya majaribio ya uongozi, vijana wame prove failure hadi akina Mangula na Kinana kuitwa tena.
Bado tunaaminishwa kuwa ujana ni silaha nzuri sana ya kukabiliana na matatizo tuliyo nayo.

Siku zote mwanasiasa anayevutia watu kwa jinsia, dini au umri anakuwa amefikia ukomo wa ushawishi.
Ni hoja dhaifu sana kwakweli.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom