Sidanganyiki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sidanganyiki!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shedafa, Jul 15, 2009.

 1. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wandugu napenda kuelezea hisia zangu kwa hili tangazo la TAMWA, linalomuonyesha binti wa shule akipambana na vikwazo na majaribu mbalimbali nimelipenda sana. Siku zote nilikuwa nikifikiri njia mbadala za uhamasishaji wa mabinti zetu badala ya kutupa lawama kwa akina FATAKI tu, zinaweza kuwa na impact kubwa zaidi. Tangazo hili linawajengea kujiamini fulani hivi mabinti zetu, na kama ilivyo kawaida ya nguvu ya matangazo inatia raha sasa kila ukipita unasikia kabinti kanasema SIDANGANYIKI!. BRAVO TAMWA!
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ni kweli hawadanganyiki? Au imekuwa slogan tu mitaani kuwa mabinti siku hizi hawadanganyiki, na uku wanaendelea kukatizwa masomo kila kukicha?

  Hivi uhalisi wa mtoto wa kike wa Kitanzania, unampa usalama wa kutosha wa kutoweza kudanganyika?

  Nahisi kama Tamwa nao wapo kisanii, wanatwanga maji kwenye kinu.
   
 3. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kudanganyika au kutodanganyika inategemea mabinti wenyewe, hasa ukichukua na hali ya maisha hasa ya majumbani kwao. Kilichonipendeza ktk tangazo hili ni ile hali ya kuwafanya washiriki katika hii vita ya kuwalinda, sio siku zote anatafutwa mchawi tuu. Au siku zote ni kondomuu tuu, ni aina fulani ya kuwafanya waone wanaweza kujiamini na kushinda.
   
 4. GP

  GP JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  lile tangazo liko FINYU SANA, NO CREATIVITY THERE.
  liko finyu kivp?
  kwanza vishawishi vile ni vya chini sana, nikiwa namaanisha watoto wa kike hasa wanafunzi wanadanganywa siku hizi na vitu kama simu, au shopping za kufa mtu, outing za maana, mijichips kuku, lifti za magari, nk.
  sasa labda TAMWA waniambie waeweka mahususi kwa watoto wa vijijini, wewe mjini hapa kama dsm mtoto gani umdanganye kwa lifti ya baiskeli?, au penseli dukani?.
  labda waseme ni mahususi kwa vijijini, lakini je huko vijijini ujumbe unafika ipaswavyo?, kuna umeme?, kuna TV?.
  ni maoni yangu tu hayo na si msimamo wa JF.
  nawakilisha.
   
 5. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mi sioni jipya kwenye lile tangazo, zaidi zaidi ni poorly prepared and probably unreviewed ad!

  Watz tujaribu kuwa wakweli, leo hii nenda pale posta au mwenge au popote pale kwenye mikusanyiko ya mabinti wakienda huku na kule, jaribu kufanya utafiti wa kawaida kabisa na utagundua kwamba kwa kila mabinti 10 basi nane au zaidi utakaowatongoza watakubali ama kuonesha kukubali na baada ya hapo ukimpa outing mbili tatu basi mwanawane kiburudisho kitakuita majina yote mazuri!!

  Mi naona watz matatizo yetu ya umasikini ndiyo yanatuingiza kwenye mambo haya. Ndio maana mabinti wanababaika sana na vitu vidogo vidogo. Binti akijua una uwezo wa kumpa vipesa vya matumizi ya salon, pamba, lift akiwa anaenda job ama shule basi atakuganda mpaka basi.

  Naamini kama kila binti angekuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yake ya msingi kutoka kwenye familia yake basi haya mambo ya uhuni yangepungua sana.

  Watu tunawapa lift hawa mabinti na ndani ya gari yanapigwa matangazo kama haya lakini binti ndio kwanza anakwambia "tutapitia slipway kwenye ice cream dear?" Ukimwambia ngoja nikuwaishe nyumbani, utasikia "mi home ntawaambia nimechelewa kwa sababu ya usafiri"
   
 6. A

  Audax JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tangazo ni zuri na linawasidia saana wanafunzi,wajifunze kutoka kwa huyo bint.Wazingatie masomo maana mambo mengine watayakuta tu,hayana haraka.
   
 7. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  muangalieni kwa umakini huyo binti wa kwenye tangazo,anawakilisha ujumbe mzuri kwa mabinti zetu lakin kwa kumuangalia machoni kwake,hamaanishi kile akisemacho ndio akifanyacho, na hakika kabisa kapo ki tangazo zaidi lakini nupande wa pili kanadanganyika vizuri tu. chamsingi hapa ni kudili na wqatoto wetu nyumbani kuwapa mawaidha ya kutosha elimu ya jinsia wajitambue mapema na namna ya kuwakinga na mabaradhuli waliopo. tuanze sasa nyumbani tusitegemee hilo tangazo kutuokolea mabinti zetu.
  nawakilisha ni maoni yangu tu.
   
 8. a

  audrey Member

  #8
  Jul 16, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili tangazo nikichekesho tu lakin in reality si kwel.
  Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu flan cha Tanzania ninasoma BA(ED) wakati ninafanya field katika moja ya shule za sekondari Dar nilikutana na kioja kimoja ilikuwa hivi "katika jiji letu tuna tatizo la daladala siku hiyo nilimwomba konda ampakize mwanafunzi mmoja kwenye gar na niliahidi kimlipia nauli kilichotokea ni kuwa yule BINTI alikataa kupanda gar lile na mwishoe akaletwa na Fataki shuleni akiwa kwenye gar,nilipojaribu kumwoj BINTI alidai kapewa lifti mwishoni yule binti alikutwa na ujauzito" SWALI JE HUYU BINTI HADANGANYIKI????
   
 9. GP

  GP JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135

  sema wewe mkuu.......!, umeonaeeeeeeh
  halafu eti wanaleta mambo ya baiskeli, 1947
  mara 100 ya matangazo ya Fataki yanamaana, tena waelenga kote kote, kama ukikumbuka Fataki alikwenda kijijini pia akatoswa kwa blauzi ya 500 na ndizi!
   
 10. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Ukweli ni kwamba kwenye reality hili tangazo hali-apply. Hiyo sidanganyiki mimi naona kama ni slogan fulani, lakini mabiti wengi sana wanadanganywa kila siku. Matangazo ambayo yako kihalisia zaidi ni yale ya FATAKI.
   
 11. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi nafikiri iwekwe matangazo ya kuwabadilisha fikra watanzania na si kudhalilisha watoto.Kuna kubaka,kushawishi kwa fedha nk. cha muhimu watu wabadili fikra zao kuondokana na dhambi.
   
 12. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Matangazo kama lile la huyo binti nalifananisha na lile la DAWASCO la mama na mtoto wake wanaondoka nyumbani kwa sababu baba hajalipa bili ya maji.

  Matangazo haya yangeandaliwa vizuri zaidi kwa KUUZA KAZI ya kuandaa tangazo kwa WATU WENYE UELEWA WA SUALA ZIMA LA UANDAAJI WA MATANGAZO.
  Unatangaza KAZI , unatafuta kampuni tatu au zaidi zinazoweza kuleta proposal zao na associated costs za hizo proposals.

  Watu wanakaa chini wakutengenezee matangazo.Unachofanya wewe ni kuwapa MAUDHUI YA HILO TANGAZO.

  Wanatengeneza matangazo kama matatu ya aina tofauti na kuwasilisha kwenye menejimenti ya eg. TAMWA.

  Watu wanapitia na kuchangua lililo bora na finally MUANDAAJI ANATOA TOLEO LA MWISHO na kukabidhi kwa Wahusika eg. TAMWA na wao wanalipeleka kwenye vyombo vya habari kwa utangazaji.

  TANGAZO LILE LINAONYESHA NI AINA GANI YA VIONGOZI TULIONAO KWENYE TAASISI ZETU NYINGI.HASA ZA UMMA.

  SIFA ZAO: SHORT-SIGHTED, OLD-FASHIONED NA MENGINEYO YANAYOFANANA NA HAYO,LAKINI UJUAJI MWINGIIII.LOL

  MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 13. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2009
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pale ungeangalia vizuri penseli ilikuwa imeambatana na elfu 10 iliokunjwa.
   
Loading...