notradamme
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 2,009
- 452
guuuuuud. nilikuwa napishana maneno na mmoja kati ya waandishi wa gazet la MWANAHALISI hili toleo la tarehe 08/12.2010Mzee Mzima Mwanakijiji, habari zaasubuhi??
Vipi, nyumbani kwema??? Maana naona bado ni asubuhi hata kukusingizia jamaa atakua kalewa naona aibu hata kusema. Hizi kisrani na ufanano kati yako na Malaria Sugu na kwa muda ule ule mzee eehhh?? Au hizi ID zote mbili ni za kwako mzee.
Busara zinatuelekeza hivi, ukiona swala wakitimka katika kundi kubwa wakitoka porini walikojizoelea huku wakijaribu kunyang'anyana mlango na wewe nyumbani kwako WALA HUHITAJI KUULIZA KUNANI HUKO KWAO PORINI. Cha msingi na wewe timkia tu ndani mara moja ukingoja sasa SIMBA huenda akakugeuza kitoweo. Ndani ya chama kilichokua salama yetu sote Tanzania kumeingiliwa na MDUDU WA AJABU mzee. Ndio maana unaona hata na wazee wetu Mzindakaya Majiyatanga ambao kisiasa bado ni Vijana wadogo tu wamejiamulia kujitunzia heshima zao kwa kwenda nyumbani mapema. Hivi MM pamoja na MS niseme nini ndio tuelewane hapa???
Mada ya katiba yaliopamba moto hivi sasa wala halina jina nyingine bali ni kwamba Tanzania TUMETIWA AIBU KUBWA kimataifa na wanasiasa waroho na MAFISADI ambao kila kitu mali hakiwapiti mbali. Hebu angalia sasa hivi wanavyohangaika KUTAFUTA FEDHA ZA KUJA KUNUNULIA UCHAGUZI WETU 2015 yaani ni fedheha tupu na hawawezi kuyazuia tena kuonekana wazi mezani kwa sababi ni kwamba walishayasuka hivyo ni kuendelea kufumuka tu machoni mwetu.
Mwanakijiji swali lako halimtii shaka sana mwenye ananeemeka na CCM- Mafisadi ya sasa hivi. Lakini ukumbuke kwa CCM-Uadilifu wote tunawafahamu hadi dakika hii na ile CCM-Yatima ambayo nayo ni sampuli nyingine ya mafisadi ila tu wamefungiwa nje kwa sasa kwa sababu hawana vinasaba na wanamtandao nao pia tunawatambua bila kujali dini zao, Ubara wala Visiwani!! MM, Mwizi ni mwizi tu hata Lowassa hawezi kujificha nyuma ya madhabahu na tukamkubalia kamwe. Nitakushangaa sana, sawa sawa na ninavyomshangaa rafiki yangu MS ambaye pia nahisi ni wewe wewe hapo, kwamba badala ya kuona madai ya katiba kwa sasa ni matokeo ya wizi uliokithiri kila pembe ya nchi, kiburi cha sokwe mtu na dalili za mzaha kwa mambo ya msingi, yeye akawa anaona madai ya mabadiliko kwetu sisi vijana kwa sasa chini ya mawani ya udini - HOW MYOPIC here mzee??
Mwisho, ninalo swali rahisai tu, je huwa kuna KIPINDI FULANI KATIKA MAJIRA HIZI ZA MWAKA ambazo mtu au watu wakidai katiba ndio sahihi?? Ukumbuke wewe unahisi kana kwamba huenda umeshiriki kudai sana katiba kwa kalamu yako kipindi kirefu sasa lakini hilo tu peke yake haikupi uhalali wa kuhoji hata kidogo Mtanzania yeyote atakayejiamulia kudai katiba mpya hata kuanzia wiki ijayo.
Nadhani tuko pamoja rafiki yangu mwana-JF mwenzangu.
na ugomvi wangu na yeye ni swali langu kwake kwamba (ni kweli mnadai katiba mpya kwa maslahi ya taifa au mna agenda nyingine ya kutaka kutambuliwa kama wanaharakati waliofanikisha uwepo wa katiba mpya??) alishindwa kunijibu na akahamia katika kutoa maneno machafu kwamba nami ni msujudia watawala!!!!!
hapa anachotuthibitishia MWANAKIJIJI ni ule wasiwasi wangu kuwa kuna watu wanataka waje wapate nafasi katika serikali zijazo kutokana na mchango wao katika kudai katiba mpya na mwisho wa siku waje kuwa MAFISI na MAFISADI.hawa ni mafisadi watarajiwa ambao wanaona kama wanaporwa nafasi yao ya kuwa WACHANGIAJI WAKUU katika mchakato wa kuelekea kuundwa kwa katiba mpya na hivyo wanaona kama vile malengo yao ya kisiasa(KIFISADI) YANAINGILIWA NA WATU KAMA MKAPA,JAJI MKUU NA WENGINE WENGI WATAKAOJITIKEZA.
Mwanakiji na wenzako wa aina yako mmejawa na tamaa kiasi cha kuwa tayari hata kuitupa na kuisagasaga dhamira yenu mlioipigania kwa muda mrefu(KATIBA MPYA), eti kisa tu......... mtakuwa avershadowed.
acheni ubinafsi,,, muundo mpya wa katiba ni muhimu kwa taifa zima bila kujali ni nani alifanikisha