Sidanganyiki - Leo ndio mnajua Tanzania inahitaji katiba mpya?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,046
2,000
Mambo mengine yanashangaza sana; leo kila mmoja wa watu mashuhuri anatafuta gia ya "kutokea"; mwisho Rais na wajumbe wa Kamati Kuu nao watakuja na kusema "wanataka Katiba Mpya". Nimekaa naangalia wanaojitokeza kudai katiba mpya na wanaripotiwa huku wakibeba ujiko wa ofisi na vyeo vyao; ati kuanzia Mkapa na sasa Jaji Mkuu na wote wengine katikati yao ati wote sasa "wanataka Katiba Mpya"! Really? Why?

Ati leo viongozi wa dini nao wanajitokeza na kudai Katiba Mpya! Mwisho wataanza kuja na wabunge wa CCM wakidai Katiba Mpya! Utani mwingine jamani!

Katiba Mpya? Kwani hii iliyopo imegunduliwa ina matatizo gani ambayo hawakuyaona miaka 20 iliyopita? Kwamba mwaka 2010 ndio wamegundua kuwa Katiba ina matatizo? Naam, watasema imejulikana kuanzia 1992. Watasema kuwa miaka yote hii kumekuwa na "kilio" cha Katiba Mpya na wengine watatuambia jinsi walivyojaribu kuzungumzia hili miaka yote hii wakituambia juu ya Ripoti ya Nyalali n.k

Lakini miaka yote hiyo hawakujitokeza hawa kwa nguvu hivi kudai "katiba mpya". Lakini cha kuudhi na ambacho naamini ni cha uzugaji uliokubuhu ni kuwa wote hawa hawakuwa na ujasiri wa kudai Katiba Mpya kabla ya uchaguzi. Tangu 2005 hadi ulipofika uchaguzi huu wengi tumeandika na wengine wamelalamikia matatizo mbalimbali. Suala la ubovu wa tume ya uchaguzi halikuibuliwa kwenye uchaguzi wa 2010; wengine tulishabeza wapinzani kwenda kwenye uchaguzi huu uliopita wakiwa na tume ile ile na mfumo ule ule na tukasema mapema wasije kulalamika "tume ya uchaguzi, tume ya uchaguzi". Tulisema wamekubali kucheza kwa kanuni za mchezo na refa ambaye tayari alishajionesha kuwa ana upendeleo akiwavuruga wasilalamike. Sijui walisahau wapi yaliyotokea Kiteto? Walisahau vipi yaliyotokea Tunduru?

Lakini sasa siyo wapinzani tu hata viongozi wengine wa serikali na hata wa CCM wanaanza kudai Katiba Mpya. Kilichonishangaza ni kuwa Rais Mkapa anadai naye Katiba Mpya! Really? I mean Really? Alikuwa Rais kwa miaka 10; alisimamia mabadiliko ya Katiba ya 2005 - lakini hakutaka Katiba mpya then?

Lakini wote hawa wanaojitokeza kudai Katiba Mpya hawataki kusema kitu kilichowazi; Hawataki kusema hasa kwanini sasa baada ya uchaguzi wamepata ujasiri wa kudai Katiba Mpya. Walijua sheria ya uchaguzi, walijua mfumo wa tume ya uchaguzi; walijua malalamiko ya Katiba mpya lakini kwa miaka karibu ishirini walikaa kimya. Lakini sasa kuna kitu kimetokea; kitu ambacho hawana ujasiri wa kukisema au kukiita kwa jina lake.

Hoja ya kuandika upya katiba haiwezi kunogeshwa kwa kutokuwa tayari kuita ukweli kwa jina lake. Ni nini kilitokea baada ya uchaguzi; au swali sahihi zaidi ni nini kilitokea wakati wa uchaguzi ambacho kimewafanya watu waamke na kudai Katiba Mpya. Wakiseme kwanza na waseme wasimung'unye maneno; vinginevyo wapo ambao watawasaidia kukisema hicho kinachofanya hoja ya Katiba Mpya iwe na nguvu sasa kuliko 1992.

Dare to say it otherwise.. naomba tuachane na hoja ya Katiba Mpya hadi tutakapokuwa tayari kusema hasa ni kwanini tunataka Katiba Mpya hasa baada ya uchaguzi wa 2010.
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
56,213
2,000
Lo!
Hakika Gwa kumyitu umeongea jambo la maana sana.
Mkapa, kwanini hakuona kuwa katiba ina mapungufu kipindi cha utawala wake? Kaondoka madarakani ndio analeta kilimilimi
 
Butola

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
2,291
2,000
ati kuanzia Mkapa na sasa Jaji Mkuu na wote wengine katikati yao ati wote sasa "wanataka Katiba Mpya"! Really? Why?

Kilichonishangaza ni kuwa Rais Mkapa anadai naye Katiba Mpya! Really? I mean Really? Alikuwa Rais kwa miaka 10; alisimamia mabadiliko ya Katiba ya 2005 - lakini hakutaka Katiba mpya then? .

Ni sawasawa tu Nyerere alivyodai kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi mara baada ya kutoka madarakani, nyakati zinabadilika na fikra zinabadilika hasa unapokuwa nje ya uwanja!!
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,950
2,000
Hoja ya kuandika upya katiba haiwezi kunogeshwa kwa kutokuwa tayari kuita ukweli kwa jina lake. Ni nini kilitokea baada ya uchaguzi; au swali sahihi zaidi ni nini kilitokea wakati wa uchaguzi ambacho kimewafanya watu waamke na kudai Katiba Mpya. Wakiseme kwanza na waseme wasimung'unye maneno; vinginevyo wapo ambao watawasaidia kukisema hicho kinachofanya hoja ya Katiba Mpya iwe na nguvu sasa kuliko 1992.

Dare to say it otherwise.. naomba tuachane na hoja ya Katiba Mpya hadi tutakapokuwa tayari kusema hasa ni kwanini tunataka Katiba Mpya hasa baada ya uchaguzi wa 2010.

Mzee Mwanakijiji hapo umelonga....................msukumo huu umeekuja kwa sababu kila mtu ajua JK si Raisi halali wa nchi hii na ya kuwa dhuluma kamwe haitapeleka nchi hii kwenye neema..................sasa ndiyo maana kila mmoja sasa aona uhaja wa kuibadilisha katiba hii kwa minajili ya kutokomeza dhuluma au vinginevyo ile amani tuliyokuwa tunajivunia haiwezi kuwepo katika lindi hili la dhuluma ambayo taifa limeghubikwa nalo................................................

Hata hivyo siafiki kuwa tuache kushughulikia hili suala kwa hivi sasa.......tusipolishughulikia yaliyotokea Kenya yatajitokeza Uchaguzi ujao................................................Mungu ibariki Tanzania ..............Mungu Ibariki Afrika na Dunia yote...................Tuishi kwa kumwogopa Muumba wetu vinginevyo maafa yananukia........................
 
Abdulhalim

JF-Expert Member
Jul 20, 2007
16,726
2,000
Tuache udwanzi jamani..Hoja ya maana hapa ni kwamba tunahitaji katiba mpya au mabadiliko ya katiba ili kuvest matakwa na mahitaji ya sasa..habari ya nani kasema nini is immaterial.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,950
2,000
hongera mwanakijiji. Wakati wa mh makapa walikuwa kimya

Kauli hii yapotosha ukweli wa kihistoria....................wakakti wa Mkapa marekebisho mawili ya kikatiba yalifanyika.........hivyo siyo kweli walikaa kimyaa......................................kila awamu kulikuwa na marekebisho ya kikatiba ila yalilenga kuwanufaisha viongozi na wala siyo raia wote kwa ujumla..............................
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,046
2,000
Tuache udwanzi jamani..Hoja ya maana hapa ni kwamba tunahitaji katiba mpya au mabadiliko ya katiba ili kuvest matakwa na mahitaji ya sasa..habari ya nani kasema nini is immaterial.

kwanini sasa hivi tunahitaji sana "katiba Mpya"? nini kimetokea ambacho hao wanaodai Katiba Mpya hawataki kukisema. Kwa sababu as a matter of fact yote wanayoyasema yalikuwa kweli kwa miaka mitano iliyopita; why now?
 
Abdulhalim

JF-Expert Member
Jul 20, 2007
16,726
2,000
kwanini sasa hivi tunahitaji sana "katiba Mpya"? nini kimetokea ambacho hao wanaodai Katiba Mpya hawataki kukisema. Kwa sababu as a matter of fact yote wanayoyasema yalikuwa kweli kwa miaka mitano iliyopita; why now?

Kila jambo lina wakati wake wa kujitokeza..hata wewe Mkjj bila shaka una mawazo anuai kichwani kwako..je hutatafuta muda muafaka kwa kila jambo? utatekeleza yote kwa mkupuo? unayo capacity? etc etc?
 
Mubezi

Member
Sep 27, 2010
71
95
Kilichotokea si uchakachuaji wa matokeo,kwa mujibu wa habari nyeti waliopiga kura ni milioni 15 na dr slaa alishinda kwa alilimia 67,kura zikaaribiwa na tume,kila mtu serikalini anajua ilo,ndio man wanataka katiba mpya ambayo itakuwa na tume huru
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,062
2,000
kwanini sasa hivi tunahitaji sana "katiba Mpya"? nini kimetokea ambacho hao wanaodai Katiba Mpya hawataki kukisema. Kwa sababu as a matter of fact yote wanayoyasema yalikuwa kweli kwa miaka mitano iliyopita; why now?

MMM

Madai yalikuwapo tokea enzi, ila binafsi nadhani kwa sasa wale hypocrites wamepewa go ahead na kiongo wao na chama chao kudai hivyo ili kudivert attention ya watanzania kama ilivyo ada... sie ni wadanganyika, tumeshasau wizi wa kura, hali ngumu ya maisha, ufisadi, bajeti shenzi kwenda kwa GBS supporters na unafiki wao walioita wapinzani kokoto

TO ME HII VIGOR YA KATIBA MPYA INAPEWA PROMO ZAIDI NA WADANDIA HOJA WA KILA SIKU (CCM)

sababu kubwa ya pili ni kwamba the wind of change has blown and any resistance will just lead to ones peril (including hao wenye vyao kwa sasa)
 
kilemi

JF-Expert Member
Mar 13, 2009
536
225
Hawa ndo waswahili tulionao TZ, kudandia hoja za watu wengine! Kianchotafutwa hapa ni mtu kuitwa "mhamasishaji wa katiba mpya".
Niwakumbushe tu, si Nyerere wala CCM walionzisha mfumo wa vyama vingi! Ni mashinikizo kutoka nje hasa wahisani. Kinachoendelea leo kila mtu anajua!! "Kama sio CCM vyama vingi visingekuwepo"
Kesho tutasikia "kama sio Mkapa na Kikwete katiba mpya isengekuwepo"
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,046
2,000
Kila jambo lina wakati wake wa kujitokeza..hata wewe Mkjj bila shaka una mawazo anuai kichwani kwako..je hutatafuta muda muafaka kwa kila jambo? utatekeleza yote kwa mkupuo? unayo capacity? etc etc?

Hilo ni jibu jepesi; ingekuwa hivyo basi lingekuwa wazo la mtu mmoja mmoja; kwanini wote hawa wanajitokeza sasa? Nini kimetokea kwa sababu isije kuwa ni njia ya kutokea ambayo hawa wote wanaosimama hawtakuwa na ujasiri wa kusimamia hasa wakati jambo hili litakapopamba moto. Kwa sababu kwa kusema "wanataka Katiba Mpya" hawatuambii wanataka "katiba mpya gani"? Maana wote wanaweza kuwa wanataka katiba "mpya" lakini wakiwa na maana tofauti kabisa kwani wengine wanaweza kutaka Katiba Mpya itakayohakikisha mfumo wetu utawala ulivyo sasaa unadumishwa na kutengeneza mazingira ya wao kutawala milele - itakuwa mpya lakini ndicho tunachotaka?

Wanaposema wanataka Katiba Mpya watuambia iweje lakini waulizwe vile vile kwani iliyoopo ina matatizo gani ambayo wanayaona sasa? Kama suala ni timing kwanini wasisubiri hadi uchaguzi ujao wa 2015 ili wasionekane wamempania JK na CCM sasa hivi?
 
Butola

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
2,291
2,000
kwanini sasa hivi tunahitaji sana "katiba Mpya"? nini kimetokea ambacho hao wanaodai Katiba Mpya hawataki kukisema. Kwa sababu as a matter of fact yote wanayoyasema yalikuwa kweli kwa miaka mitano iliyopita; why now?

Miaka 5 iliyopita hakuna nchi katika Afrika Mashariki iliyokuwa na katiba mpya, walichokifanya Kenya mwaka huu ndicho kinachochochea wengi sasa kuona kuwa wakati wa kuitupa katiba ya mkoloni umefika.
 
Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
0
Mzee Mzima Mwanakijiji, habari zaasubuhi??

Vipi, nyumbani kwema??? Maana naona bado ni asubuhi hata kukusingizia jamaa atakua kalewa naona aibu hata kusema. Hizi kisrani na ufanano kati yako na Malaria Sugu na kwa muda ule ule mzee eehhh?? Au hizi ID zote mbili ni za kwako mzee.

Busara zinatuelekeza hivi, ukiona swala wakitimka katika kundi kubwa wakitoka porini walikojizoelea huku wakijaribu kunyang'anyana mlango na wewe nyumbani kwako WALA HUHITAJI KUULIZA KUNANI HUKO KWAO PORINI. Cha msingi na wewe timkia tu ndani mara moja ukingoja sasa SIMBA huenda akakugeuza kitoweo. Ndani ya chama kilichokua salama yetu sote Tanzania kumeingiliwa na MDUDU WA AJABU mzee. Ndio maana unaona hata na wazee wetu Mzindakaya Majiyatanga ambao kisiasa bado ni Vijana wadogo tu wamejiamulia kujitunzia heshima zao kwa kwenda nyumbani mapema. Hivi MM pamoja na MS niseme nini ndio tuelewane hapa???

Mada ya katiba yaliopamba moto hivi sasa wala halina jina nyingine bali ni kwamba Tanzania TUMETIWA AIBU KUBWA kimataifa na wanasiasa waroho na MAFISADI ambao kila kitu mali hakiwapiti mbali. Hebu angalia sasa hivi wanavyohangaika KUTAFUTA FEDHA ZA KUJA KUNUNULIA UCHAGUZI WETU 2015 yaani ni fedheha tupu na hawawezi kuyazuia tena kuonekana wazi mezani kwa sababi ni kwamba walishayasuka hivyo ni kuendelea kufumuka tu machoni mwetu.

Mwanakijiji swali lako halimtii shaka sana mwenye ananeemeka na CCM- Mafisadi ya sasa hivi. Lakini ukumbuke kwa CCM-Uadilifu wote tunawafahamu hadi dakika hii na ile CCM-Yatima ambayo nayo ni sampuli nyingine ya mafisadi ila tu wamefungiwa nje kwa sasa kwa sababu hawana vinasaba na wanamtandao nao pia tunawatambua bila kujali dini zao, Ubara wala Visiwani!! MM, Mwizi ni mwizi tu hata Lowassa hawezi kujificha nyuma ya madhabahu na tukamkubalia kamwe. Nitakushangaa sana, sawa sawa na ninavyomshangaa rafiki yangu MS ambaye pia nahisi ni wewe wewe hapo, kwamba badala ya kuona madai ya katiba kwa sasa ni matokeo ya wizi uliokithiri kila pembe ya nchi, kiburi cha sokwe mtu na dalili za mzaha kwa mambo ya msingi, yeye akawa anaona madai ya mabadiliko kwetu sisi vijana kwa sasa chini ya mawani ya udini - HOW MYOPIC here mzee??

Mwisho, ninalo swali rahisai tu, je huwa kuna KIPINDI FULANI KATIKA MAJIRA HIZI ZA MWAKA ambazo mtu au watu wakidai katiba ndio sahihi?? Ukumbuke wewe unahisi kana kwamba huenda umeshiriki kudai sana katiba kwa kalamu yako kipindi kirefu sasa lakini hilo tu peke yake haikupi uhalali wa kuhoji hata kidogo Mtanzania yeyote atakayejiamulia kudai katiba mpya hata kuanzia wiki ijayo.

Nadhani tuko pamoja rafiki yangu mwana-JF mwenzangu.
 
Hardwood

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
993
1,000
Jamani, kila jambo na wakati wake.... Hata mapinduzi ya Ufaransa yalichochewa zaidi na matusi ya mfalme kwa makabwela wa Ufaransa pamoja na kwamba hata kabla ya matusi hayo bado makabwela hao walikuwa na taabu zao nyingi tu....lakini wakati muafaka wa mapinduzi ulifika pale mfalme alipowatukana!!!

Nadhani cha muhimu kwetu ni kupima je wazee hawa wanaongozwa na dhamira safi katika kudai katiba mpya??? Isije ikawa they are there for initiating sham business!!!...Let's watch the game carefully...and we will see the truth
 
Abdulhalim

JF-Expert Member
Jul 20, 2007
16,726
2,000
Hilo ni jibu jepesi; ingekuwa hivyo basi lingekuwa wazo la mtu mmoja mmoja; kwanini wote hawa wanajitokeza sasa? Nini kimetokea kwa sababu isije kuwa ni njia ya kutokea ambayo hawa wote wanaosimama hawtakuwa na ujasiri wa kusimamia hasa wakati jambo hili litakapopamba moto. Kwa sababu kwa kusema "wanataka Katiba Mpya" hawatuambii wanataka "katiba mpya gani"? Maana wote wanaweza kuwa wanataka katiba "mpya" lakini wakiwa na maana tofauti kabisa kwani wengine wanaweza kutaka Katiba Mpya itakayohakikisha mfumo wetu utawala ulivyo sasaa unadumishwa na kutengeneza mazingira ya wao kutawala milele - itakuwa mpya lakini ndicho tunachotaka?

Wanaposema wanataka Katiba Mpya watuambia iweje lakini waulizwe vile vile kwani iliyoopo ina matatizo gani ambayo wanayaona sasa? Kama suala ni timing kwanini wasisubiri hadi uchaguzi ujao wa 2015 ili wasionekane wamempania JK na CCM sasa hivi?

Of course hoja ya katiba mpya ni hoja hot cake kwa sasa na ipo vichwani mwa wengi, whether wanaosapoti au wanaokataa..hivyo sio ajabu kukawa na matamko mengi kuhusiana na mambo ya katiba mpya...kwa sababu ni kitu kilichoibuka baada ya kumaliza zoezi la uchaguzi.

Suala la nini kibadilishwe hilo ni swali ambalo waandishi walitakiwa wawaulize hao watoa matamko, kwamba watoe mawazo yao kuhusu nini kifanyike kuboresha, na nini kiondolewe.
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,512
2,000
Waacheni nao waseme wanataka KATIBA MPYA. Sote tunaiona hali ilivyo sasa. Hata KATIBA hii tuliyonayo haina wa kuilinda wala kuitetea. Jana nilimwona Maalim Seif akiingia pale uwanja wa UHURU kwa itifaki ndefu wakati cheo chake hakimo kwenye KATIBA yetu!
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,046
2,000
naona watu mnashindwa kupata pointi yenyewe na kama kawaida mnaanza kuuliza kama niko bado na akili zangu timamu. Mnapenda mno mazingaombwe kiasi cha kushangilia mkiona sungura katolewa kwenye kofia na wengine wanaweza kuapa kabisa kuwa ni "muujiza". Sasa leo watu wanaanza kuimba "katiba mpya" basi watu wanatakiwa kushangilia:

Hawawaambii tatizo la Katiba ya sasa ni nini? - of course tunatakiwa tuwe tunajua sote
Hawasemi kwanini sasa hivi na haikuwa kabla- tunaambiwa ni muda tu
Hawasemi wanataka nini hasa - yale yale "katiba mpya" - upya wa nini?
Hawasemi ni vitu gani viboreshwe? Je wakibadilisha tu Tume ya Uchaguzi watu wataridhika? Kwanini isiwe kufanyia mabadiliko vipengele vinavyolalamikiwa halafu tukamaliza kwani hilo halihitaji siku nyingi hata kikao cha bunge kinaweza kufanya hivyo.
Ati Katiba iliyopita haikuandikwa na sisi - well kwani kuandika sisi wenyewe kunatuhakikishia vipi Katiba nzuri? Leo hii miaka 49 ya kujitawala mbona baadhi yetu hatujivunii kuoona tunavyojitawala? kwanini tuamini ati kwa vile tutaandika Katiba sisi wenyewe basi itakuwa nzuri? Jamani, kwani vyama vingine vilirudishwa vipi na leo watu hawafurahii wakati tulishirikishwa kuvirudisha?

Katiba Mpya? kwa manufaa ya nani? Siyo wote wanaosema "nyeupe" wanamaanisha "nyeupe pe" wengine wanamaanisha "rangi ya maziwa!"
 
Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,635
2,000
Hii ni hoja wa Chama kikuu cha upinzani kiitwacho CHADEMA. Serikali imesalimu amri baada ya aibu iliyoipata baada ya kuiba kura wazi wazi . Wafadhili wetu wamechukulia Chadema kuwa chama chenye busara kuliko vyama vingi vya aina hiyo Africa.

Kwa hiyo sababu ya Mkapa , Jaji Mkuu , Jk na wengineo sasa wanataka Katiba mpya ni dhahiri. Ni shinikizo la Chadema kupitia wahisani.

Wanaona aibu kutamka hadharani ndio maana wanawatumia akina Mkapa kinyemela .

Bravo Slaa .This is how intelligent people work. At last new katiba will eventually be in place.
 
Mabel

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
1,134
1,500
naona watu mnashindwa kupata pointi yenyewe na kama kawaida mnaanza kuuliza kama niko bado na akili zangu timamu. Mnapenda mno mazingaombwe kiasi cha kushangilia mkiona sungura katolewa kwenye kofia na wengine wanaweza kuapa kabisa kuwa ni "muujiza". Sasa leo watu wanaanza kuimba "katiba mpya" basi watu wanatakiwa kushangilia:

Hawawaambii tatizo la Katiba ya sasa ni nini? - of course tunatakiwa tuwe tunajua sote
Hawasemi kwanini sasa hivi na haikuwa kabla- tunaambiwa ni muda tu
Hawasemi wanataka nini hasa - yale yale "katiba mpya" - upya wa nini?
Hawasemi ni vitu gani viboreshwe? Je wakibadilisha tu Tume ya Uchaguzi watu wataridhika? Kwanini isiwe kufanyia mabadiliko vipengele vinavyolalamikiwa halafu tukamaliza kwani hilo halihitaji siku nyingi hata kikao cha bunge kinaweza kufanya hivyo.
Ati Katiba iliyopita haikuandikwa na sisi - well kwani kuandika sisi wenyewe kunatuhakikishia vipi Katiba nzuri? Leo hii miaka 49 ya kujitawala mbona baadhi yetu hatujivunii kuoona tunavyojitawala? kwanini tuamini ati kwa vile tutaandika Katiba sisi wenyewe basi itakuwa nzuri? Jamani, kwani vyama vingine vilirudishwa vipi na leo watu hawafurahii wakati tulishirikishwa kuvirudisha?

Katiba Mpya? kwa manufaa ya nani? Siyo wote wanaosema "nyeupe" wanamaanisha "nyeupe pe" wengine wanamaanisha "rangi ya maziwa!"

Mwanakijiji, usisahau sisi ni wadanganyika, mvua inanyesha siku moja Dar maji yanajaa mtera na tunaambiwa mgawo sasa unakoma, tunapiga makofi.

Watu wanashindwa kukuelewa hapa, hata kama ni suala la wakati ni kweli watu wote hawa kwa pamoja wanaona sasa ndio wakati wa kudai katiba mpya? Hapana kuna kitu hapa na kiko wazi.

Mambo mengi ni matokeo, na kelele zote hizi za katika mpya ni matokeo. Watanzania tuache unafiki tuseme kweli iliyo kweli.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom