Sichanjwi na nikifa roho yangu ikawe laana kwa kila kiongozi aliyesema chanjo ni mbaya

abdulhamis

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
1,436
2,292
Habari wadau, leo nimeona niiweke msimamo wangu juu ya chanjo sababu Maneno yamekua Mengi

Nasema hivi sichanji chanjo yoyote Ile sababu Serikali yangu ilikuwa kila nikilala nikiamka nakuta kuwa chanjo ya Corona haifai na watanzania tusikubali. Ikiwa kama viongozi wote walishiriki kutuambia hayo basi likitokea la kutokea Leo sio tu kwangu mimi hata kwa baadhi ya watanzania wengine ambao wanakataa chanjo kwa sababu ya maneno yao ya mwanzo Basi wa kulaumiwa ni Serikali

Pia ifike Hatua Serikali isituongoze kwa hisia tu sababu nchi ni moja watu wale wale lakini nashangaa Jana ilikuwa tunaambiwa hii sumu tena inaua halafu leo tunaambiwa hii dawa tena inatibu cha ajabu watu ni wale wale waliotuambia jana tena bila aibu leo ni Corona kesho itakuwa nini?

Viongozi wa Tz mbadilike
 
Waziri Gwajima alisema tule tangawizi na malimao,saa hizi kashachanjwa!
Usiwaamini wanasiasa,wakisema kumekucha kachungulie nje kama kweli kumekucha.
 
Kufa utakufa tu uwe umechanjwa au hujachanjwa,maana hakuna atakayeishi milele.
Hizo laana wapelekee ukoo wako wengine unapiga hewa.
 
Habari wadau Leo nimeona niiweke msimamo wangu juu ya chanjo sababu Maneno yamekua Mengi

Nasema ivi sichanji chanjo yoyote Ile sababu serikal yangu ilikua kila nikilala nikiamka nakuta kua chanjo ya corona haifai na watanzania tusikubali. Ikiwa kama viongozi wote walishiriki kutuambia hayo basi likitokea la kutokea Leo sio tu kwangu mimi hata kwa baadh ya watanzania wengine ambao wanakataa chanjo kwa sababu ya maneno yao ya mwanzo Basi wa kulaumiwa ni Serikali


Pia ifike Hatua serikal isituongoze kwa hisia tu sababu nchi ni moja watu wale wale Lakin nashangaa Jana ilikua tunaambiwa hii sum Tena inaua alafu Leo tunaambiwa hii dawa Tena inatibu cha ajabu watu ni wale wale walio tuambia Jana Tena bila aibu Leo ni Corona kesho itakua Nini?


Viongozi wa Tz mbadilike
Kama unategemea wanasiasa ndio waongoze maisha yako binafsi basi akili huna na Mbinguni huendi
 
'
20210731_064449.jpg
 
Mwisho utaomba viongozi wa Serikali waje wakuongoze kwenye mambo yako na mkeo chumbani.
 
Back
Top Bottom