SIBUKA fm huyu Mchambuzi wenu Kituko wa mpira Yusuph Kibai mmemuokota wapi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,516
108,791
Kwanza kabisa nianze kwa kuwapongezeni sana Uongozi mzima wa SIBUKA Media Company kuanzia kwa Mkurugenzi na Mmiliki wake Dr. George Nangale ( Mbunge Mstaafu wa Afrika ya Mashariki ) na Mkewe Madam Doreen ambaye pia ni Business Development Manager ( BDM ) wa Kampuni kwa kuifanya SIBUKA fm sasa kuwa juu, kusambaa eneo kubwa la Tanzania na kukubalika na wengi ( hadi Mimi pia )

Katika mambo ambayo naweza kuwapongezeni kabisa SIBUKA fm ni kitendo chenu kizuri kabisa cha kuamua Kututangazia mechi mbalimbali za hapa Tanzania huku mkiwa mna usikivu mzuri kabisa nadhani ni kutokana na Mitambo yenu mizuri hivyo kuweza kuanza ' kuwafunika ' kabisa TBC Taifa ( Redio ) ambao sasa wana mwezi ' wamesusa ' kututangazia mipira ya VPL na hawajatoa Kwetu taarifa yoyote hivyo na Sisi ' Wadau ' wao sasa tumeachana nao na tupo na SIBUKA fm mwanzo mwisho.

Nije sasa katika suala langu la msingi na ambalo kwakweli limekuwa ' likinikera ' kwa muda sasa ambalo linamuhusu mmoja wa ' Mchambuzi ' wenu mpya mliyemleta hapo anaitwa Yusuph Kibai kwa jinsi anavyochambua na kuharibu kabisa ile ladha ya mpira na dhana nzima ya uchambuzi wa mechi zenu ambazo huwa mnatutangazia.

Najua huyu ' Mchambuzi ' wenu anataka ' Kumfunika ' kwa haraka sana Yule ' Mchambuzi ' ambaye kiukweli bila ' Unafiki ' wowote kwa sasa hana mpinzani hapa Tanzania aitwae Mzee Kashasha ambaye mara nyingi amekuwa akisikika huko TBC Taifa akiwa na Watangazaji Jesse John na Enock Bwigane wakitiririka na kuserereka vizuri sana.

Naweka hapa chini baadhi ya mifano ya hawa ' Wachambuzi ' wawili ili muelewe vizuri ninachomaanisha halafu mtagundua ni nani akiwa anachambua Wasikilizaji wake ( akina siye GENTAMYCINE ) huwa tunamuelewa haraka na nani huwa anatuacha tu njia panda kila mara kwa kutomwelewa na huwa anatuboa kweli kweli....

Hivi ndivyo mara nyingi utamsikia Mchambuzi ' Kituko ' wa SIBUKA fm Yusuph Kibai akichambua mpira pale tu anapokaribishwa na Mtangazaji mwenye ' Uyanga Uyanga ' mwingi Mshamu Hassan a.k.a Baba Nurat Mfuga Njiwa

  • attacking move planning 3-2
  • leadership football 5-1
  • management defense 1-3
  • psychological environment 3-3
  • control room 2-1
  • environmental weather 1-1
  • discipline move 5-1

Hivi kwa uchambuzi huo wa hapo juu wa Mchambuzi ' Kituko ' wa SIBUKA fm Yusuph Kibai hapa msikilizaji ataelewa nini? Sasa kibaya zaidi bora atutajie hayo ' makhirikhiri ' yake kisha atutafsirie tumwelewe lakini huwa hafanyi hivyo. Nisiwaficheni Mimi akiwa tu sasa anakaribishwa Kuchambua huwa Kwanza nazima Redio na navizia dakika moja ipite amalize Kuchambua ndipo nawasha tena na kuendelea kusikiliza matangazo yao.

Ufuatao ni Uchambuzi murua na makini kabisa wa Mzee Wetu ' Fundi ' Kashasha wa TBC Taifa hasa pale akiwa anakaribishwa na Watangazaji ' mahiri ' na ' weledi ' kabisa Jesse John au Enock Bwigane

  • in swing corner ya Shiza Kichuya
  • bouncing header ya John Boko
  • acrobatic shot ya Emanuel Okwi
  • direct missile ya Said Ndemla
  • intelligence marking ya Yusuf Mlipili
  • midfield control ya Jonas Mkude
  • versatile style of playing ya Erasto Nyoni
  • marvelous total football ya Simba Sports Club na mwaka huu isipokuwa bingwa sijui

Na Mzee Kashasha akishamaliza tu kusema hivyo basi haraka haraka huwa anatutafsiria Wasikilizaji kwa Kiswahili chetu huku akinogesha kwa ' mbwembwe ' zake hadi kutufanya hata Sisi akina GENTAMYCINE tusio na Hela ya Kuingilia mipirani tujisikie kama vile nasi tupo Uwanjani wakati ukweli ni kwamba huwa tupo tu ' Vibarazani ' tumejilaza na Redio zetu pembezoni.

Enyi Uongozi wa SIBUKA Media Company mliopo hapo Bamaga jirani kabisa na Kebbys Hotel vukeni tu barabara hapo na huyo Mchambuzi wenu ' Kituko ' Yusuph Kibai mumpeleke hapo Studio za TBC jirani yenu akapate kidogo tu ' Mafunzo ' kutoka kwa ' Fundi ' mwenyewe Mwalimu Kashasha ili abadilike upesi kwani nina uhakika kuwa ' haniboi ' tu Mimi peke yangu bali tupo wengi anaotuboa.

Mwisho kabisa naomba muwe mnawaambia hao Watangazaji wenu hasa huyu Mwana Yanga ' Lia Lia ' Mshamu Hassan a.k.a Baba Nurat Mfuga Njiwa pamoja na huyu Mchambuzi wenu ' Kituko ' Yusuph Kibai ambaye nae pia anavimelea vya ' Uyanga Uyanga ' kwa Kazi yao kubwa ni Kutangaza na Kutuchambulia tu mpira na siyo kuanza kututabiria matokeo ya mechi zijazo za Simba SC kama ya Al Masry za Ligi kama ambavyo walifanya jana baada ya Simba SC kutoka sare ( draw ) na Washamba na Wakuja Stand United ambako hawa Wote wawili Mtangazaji na Mchambuzi walisema kwamba Simba SC itafungwa Kapu la Magoli Jumatano na Al Masry hapo Uwanja wa Mchina ( Taifa ) Mbona Yanga SC ikiwa inacheza huwa hamuichambui hivyo?

Ni matumaini yangu makubwa Uongozi wote wa SIBUKA fm mtafanyia Kazi hizi changamoto.

Nawasilisha.
 
TBC mbona wanarusha matangazo ya mpira daily

Mwezi mzima mbona nawasikia wakitangaza


Yaani unaacha kumsikiza mwalimu Alex kashasha akisema inswing corner,ball on the space ,man in the space ,semi volley pass ,zone marking nk unaenda kumsikiliza yusuph kibai


Nimekuvua manyota
 
Apo tatizo ni ‘u-simba’ Na ‘u-yanga’ na si vinginevyo......
Frankly speaking, hilo ndilo tatizo kubwa kwenye mpira wa Tz!
 
"Kwa mtanganyika ukiongea jambo la kipumbavu na la uongo kwa kiingreza atakuamini na kukuelewa sana kuliko ukiongea jambo la maana na la ukweli kwa kiswahili"--mwalimu
 
TBC mbona wanarusha matangazo ya mpira daily

Mwezi mzima mbona nawasikia wakitangaza


Yaani unaacha kumsikiza mwalimu Alex kashasha akisema inswing corner,ball on the space ,man in the space ,semi volley pass ,zone marking nk unaenda kumsikiliza yusuph kibai


Nimekuvua manyota

Mkuu Mimi mbona siku hizi huwa siwakamati TBC Taifa kwa 87.5 Mhz? au wamebadilisha? Wewe huwa unawakamata kwa ipi? Nitashukuru ukinijibu Mkuu kwani nimechoka na huyu Mchambuzi ' Kituko ' wa SIBUKA fm Yusuph Kibai na kibaya zaidi nimegundua ana ' Uyanga Uyanga ' basi ndiyo ' kanitibua ' kabisa.
 
Apo tatizo ni ‘u-simba’ Na ‘u-yanga’ na si vinginevyo......
Frankly speaking, hilo ndilo tatizo kubwa kwenye mpira wa Tz!

Kwani huko TBC Taifa hakuna Usimba na Uyanga? Mbona najua kabisa kwamba Jesse John ni Yanga SC tena lia lia na wala simlaumu? Enock Bwigane najua ni Simba SC mwenzangu ila huwa napenda tu anapokuwa akitangaza huwa anaweka ushabiki pembeni na anafanya Kazi.

Hao akina Mshamu Hassan Baba Nurat Mfuga Njiwa na mwenzake Yusuph Kibai wao mwanzo mwisho ni Kuiponda tu Simba SC na Kuisifia Yanga SC na hivi hata Bosi wao Mkuu ( Mkurugenzi na Mmiliki ) wa SIBUKA Media Company Dr. George Nangale ni Yanga SC kindakindaki / lia lia basi ndiyo taabu kama siyo balaa tupu!
 
Mkuu Mimi mbona siku hizi huwa siwakamati TBC Taifa kwa 87.5 Mhz? au wamebadilisha? Wewe huwa unawakamata kwa ipi? Nitashukuru ukinijibu Mkuu kwani nimechoka na huyu Mchambuzi ' Kituko ' wa SIBUKA fm Yusuph Kibai na kibaya zaidi nimegundua ana ' Uyanga Uyanga ' basi ndiyo ' kanitibua ' kabisa.
Hio hio 87.5 hata jana nilifuatilia mechi ya simba na Stand hapo ,enock bwigane na mwl kashasha wakiwa mubashara
.
Labda kama upo mkoani frequency zitakuwa tofauti
 
Asante GENTAMYCINE kwa kutoa yako ya moyoni umetusaidia sana. Tutarekebisha. Huyo mchambuzi ni Abbas Pira, siyo Hassan Kibai. Tutafuatilia uzoefu wa Mzee, ikibidi tuwe naye pia Sibuka FM kwani tumedhamiria kujiimarisha katika habari za michezo. Usimba na Uyanga ni jadi, Mfuga Njiwa na mwenzake wote ni Simba damu wale. Mie Yanga na Liverpool, lakini Sibuka FM haina timu!
 
Back
Top Bottom