Siaza za Ufisadi Safi, Mwizi wa kuku na Wananchi wenye hasira KALI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siaza za Ufisadi Safi, Mwizi wa kuku na Wananchi wenye hasira KALI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fikirikwanza, May 24, 2012.

 1. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Naomba wataaluma wa maswala ya ubinadamu, sheria za nchi, katiba, na saikolojia ya binadamu mnisaidie, tena mnisaidie sana. Nawakaribisha hata raia kama mimi wasio wataaluma wa maeneo hayo kutoa tafakuri zao.

  Katika jamii yetu kuna mdudu, mdudu mbaya sana anaitwa community interferences, hivi karibuni katika jamii yetu hii ya kitanzania, ukifanya kazi kidogo ukajenga banglow, kununua gari, maisha bing bing kila mwanafamilia anakuhusudu, kila mwanajamii anakuhusudu, tena unatolewa mfano kwenu vikao mbali mbali kama sherehe au vilio kama mtu wa kuigwa.

  Katika jamii yetu hii hii, kuna watu wanaitwa wananchi wenye hasira kali, hawa ni wale ambao kimsingi wamewahi kukutana na shubiri ya vibaka, walijeruhiwa. wakisikia kibaka yuko sehemu fulani wanakodi taksi kwenda na dumu la petroli ambayo wamenunua kwa pesa zao, huwaua hawa vibaka ambao huwa wameiba simu, nguo, ndoo, pochi yenye laki, jiko la mkaa etc. Ni mbaya mtu kuwa mwizi, lakini ni mbaya zaidi kufa bila msaada, ninarudi kwenye huruka ya binadamu, lazima ajisaidie kabla ya kusaidiwa, kosa lao hawa wanajisaidia kwa watu wanyonge ambao pia wanahitaji msaada wa watu wengine, vibaka hawaendi masaki, oysterbay etc ni kwetu buguruni kwa malapa, mtoni kwa azizi ali, keko, mwenge malalakuwa etc Hii ni hasira ya wananchi,wanahasira ya kuibiwa mali zao, ni haki yako kimsingi kukasirika, wanyonge tunanyongana, wababe wanabebana.

  Je wananchi wenye hasira kali mbona hawaonekani kwenye ufisadi??? mbona mali inaibiwa tena ya taifa zima lakini sijasikia wananchi wenye hasira kali; kwani hasira ya pochi/kuku/simu inalingana na milioni 52 kwa siku???? RICHMOND, EPA etc??? Kama ukifanya kazi mwaka mmoja unagari nyumba na makorokolo kibao unasifiwa na familia/jamii kwa ujumla wakati huo ni wizi mweupe peeee, mbona fisadi anafukuzwa kazi baadhi yetu tunaandaa mapokezi ya kifalme???? kibaka anagundu gani??? jamii mbona haiko fair???? VIBAKA Nanyinyi Mkome japo adhabu yenu ni kubwa kuliko ya Mafisadi.

  JE TUANZE KUONA WANANCHI WENYE HASIRA KALI KWA MAFISADI, petroli iko wapi kwa mafisadi??? Wezi wa mali ya UMMA, wezi wa Madaraka? Jee mkakati wa kuondoa vibaka kitaifa ni upi???

  Nawasilisha.
   
 2. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dah, mkuu hili nalo neno ngoja jamaa wanakuja watakusaidia mi nimeshindwa hata kukubeba.
   
 3. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Ndugu fikirikwanza, pole sana na maswali yanayoumiza rohoni.
  Uko sahihi sana. Mtu ameiba mkate kwa kutokula siku mbili, anachomwa. Wakati yule aliyechukua hisa ya mkate wa huyu aliyechomwa kwa wizi, na kujilimbikizia anapigiwa magoti na kunyenyekewa na hawa hawa waliomchoma aliyeiba mkate! Inauma sana! Wangapi tunazungukwa na migodi yao, tena wengine wageni wanachota salama na kuondoka salama, tunabaki kuimbishwa nyimbo tusizozijua wala kuamini mali zinayoyoma, mara "demokrasia" "haki" "uhuru" "kwenda na wakati" "matakwa ya nyakati" "usasa" "......." nk. Tutaamka lini?
  Tumebaki kuhanja kwenye majukwaa ya sia kusikiliza porojo mara KASI, HARI na NGUVU MPYA, kwanini hayo yasiwe juu ya hawa wezi wa mikate yetu, twalala njaa kufikia kuiba hadi moto, kisa tu ubinafsi wa wachache.
  Iko wapi NGUVU YA UMMA katika hili, kwanini inaonekana kwa wanyonge tu? Kwanini isiwe kwa wezi wetu? SIASA...!!!?
  Hata siku moja NGUVU YA UMMA haijawahi kuishi kwenye masanduku ya kura, na mikutano ya siasa, NEVER! Nguvu ya umma ni "Vitendo".
  Mkiwa tayari tutaunganisha nguvu zetu, katika mabadiliko ya kweli.
  "It is self illussion trusting in Democtratic Politics"
  Mungu wetu anaita!
   
 4. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Inauma sana kuona Mtanzania aliyeibiwa mabilioni kwa mabilioni, amekosa hata hela ya kula, kazi wanaajiriwa wazungu hata zile za kawaida harafu anaiba mkate ili yeye ale au familia yake anakamatwa anachomwa anawaka, mtendaji wa kata au kijiji anapewa nauli kama nauli tu labda 30,000/-TZ eti anakamatwa rushwa anafukuzwa kazi, anafungwa.

  Waziri anaenda kusaini mkataba feki kinoma tena nje ya nchi, analipiwa kila kitu aidha na serikali au mwekezaji (mwizi mwenzake) mwenyewe, anaiba mabilioni anaulizwa anasema ni vijisenti ; yeye anatembea kifua mbele wala hana wakimshitaki, wala wa kumchoma moto. Waliomchoma moto aliyeibiwa na huyu kiongozi wako wapi? kwani wasimchome moto na huyo mwizi mkubwa??? Mtu kauza twiga twiga wa tanzania anajulikana dunia nzima hafanywi kitu, eti serikali inalalamika eti ni watu wenye nguvu, waziri anasema ukienda vibaya wanakuong'oa uwaziri, je ana maana wanashirikiana na rais? watakutoaje uwaziri bila ushrika na rais????

  Tatiza la kupanda mlima ukifika kileleni, unaona milima mingine mikubwa iliyoko mbali ambayo utahitaji kuipanda siku moja kabla maisha hayajaisha. TUWACHOME MOTO MAFISADI, Uwekezaji bila sera sahihi ni Wizi na Ukoloni; Mtanzania anahela gani ya kuwekeza?? kama sio platform ya wakoloni kutunyonya??? Fikiria UPYA CHUKUA HATUA MADHUBUTI
   
 5. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Well said mkuu!
  Sasa, unaitambua minyororo yetu utumwani humu? Je, uko tayari kuifungua?
  Mimi na wewe, pamoja tukithubutu tunaweza.
  Chunguza mahusiano yetu, Chunguza mifumo yetu ya kiuchumi na siasa, Chunguza tamaduni tulizonazo, je zina tija katika mazingira yetu na nyakati tulizonazo? Sioni! NGUVU YETU NI KUTHUBUTU! Umoja kwanza.
  Mungu wetu anaita!
   
 6. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Nami tumwambie hizi shida zetu?? Dr. Slaa, Zitto, Kikwete, Makamba, Mbatia, Mbowe, Mrema, Mukama, Prof Lupumba, Wanasheria??? nani tumwambie???

  WANANCHI TUUNGANE KUSEMA ILITOSHA UKOLONI NA UTUMWA WA MINYORORO, Africa is for africans, others should come as visitors who should leave when it is due or when the hosts say so.
   
 7. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Hakuna mtu wa kumwambia ndugu, ila nafsi zetu kwanza. Kipi kipo ndani ya nafsi zetu chenye mantiki katika tafsiri ya maisha. UTU KWANZA! UTU haujawahi kuwemo kwenye demokrasia wala haki za binadamu. Tena hauwezi kuishi katika tamaduni na mifumo ya kuiga kutoka ng'ambo, UTU ndio UAFRIKA wetu! Unapaswa kuwepo kwenye mahusiano yetu ya kijamii, tamaduni, mifumo ya kiuchumi na siasa!
  TUNACHOJARIBU NI KUPINGANA NA UKWELI, aidha kwa kutengenezwa au kutotaka kuumiza kichwa! Naamini kabisa, kama hatutazinduka mapema na kubuni mifumo yetu wenyewe kulingana na mazingira yetu na nyakati, basi tusitarajie mabadiliko yoyote. Tunaweza tukawa na magorofa makubwa nchi nzima, barabara angani, hospitali, shule na vyuo vya hadhi ya juu, lakini watakaotumia ni wageni na vibaraka wao wachache, zaidi ya 90% tutabaki kusubiri makombo kwenye meza za hao wachache. Mnang'ang'ania tu sijui demokrasia, ccm, chadema, cuf, nccr, ccj na upuuzi mwingine kama huo, kwanini tusiamke? Pu***V*! Haiingii akilini kuona haya, mbaya zaidi giza hili linawashika vijana mashuleni, vyuoni, mtaani, na wale vijana wa kesho. Inauma!
  Naisikia sauti ya Mungu wetu, inaita sasa! Nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU tu!
  Mungu wetu anaita!
   
 8. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Nani aliyetunga sheria ambazo hakimu anakwambia hii inakutia hatia na hii inakuweka huru?? ni bunge hili hili au nani alikuja na mpango huo??? mi nauona ndo chanzo cha ufisadi na rushwa; maana kufungwa au kuwa huru sio suala la sheria na haki, ni matakwa ya hakimu atumie sheria ipi na ungangali wa wakili wako-alikomaa vipi wakati wa kutoa utetezi, hali hii ndo rushwa/ufisadi yenyewe.
   
Loading...