Siasa zisizokuwa na mlengo wa maendeleo tanzania

tata mura

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
275
49
Ndugu zangu wana Jr. tuweke ushabiki wetu pembeni, natuongelee uhalisia wa maisha ya Mtanzania bila kuangalia itikadi zetu. Ukubali/ Ukatae Vyama vyote vya Ki-Siasa vinategemea mapato/kodi ya wananchi chini ya Chama kinachotawala kwa wakati huo. Mimi nilitegemea mgawanyanyo wanaopeana kisheria wangekuwa wanatumia kusaidia wananchi kimaendeleo, mfano; Afya,Elimu, nk. Hivi tuulizane sote kwa pamoja kila Chama kingekuwa kinarudisha fadhila kwa wananchi kwa kusaidia shughuli za kimaendeleo si tungekuwa mbali sana kiuchumi? Au sheria haziruhusu kufanya hivyo ila zinaruhusu kunyonyana?. Mfano wa sasa Ccm wanapata ruzuku zaidi ya Million 400 Tshs kwa mwezi huku Chama kinachofuata Chadema kinapata Ruzuku zaidi ya million 233 Tshs kwa mwezi.

Kwa hivi Vyama viwili kama vingekuwa na mawazo endelevu kwa kuchangia maendeleo ya mtanzania maskini kwa kukubali kutoa kila mwezi Tshs. 5,000,000 kwa mwaka 60,000,000=/ kwa kila Chama tatizo la madawati shuleni lisingekuwepo, kwenye maendeleo Serikali ila kwenye uraji wote tupate. Haya yote yanawezekana kama Wananchi tukiamka kutoka kwenye usingizi mzito wa Kugubikwa na Siasa za maneno mengi vitendo zero. Endelea kulala utaishia kupigwa na kitu kirukacho na chenye incha kali na mwisho wa nyote utasahaulika tu. Hoja ya msingi hoji siyo kushabikia tu kwani kila king'aacho si dhahabu.

Mwisho wanasiasa wetu sera wanazipata huko huko kwenye mikutano/maandamano.Mfano; Ujumbe mkuu wa Chadema kwenye ziara zao Morogoro/ Iringa, je ulikuwa mauwaji (Ally Zona & Mwangosi)? Kwani hakuna kingine kilichosikika tofauti na mauwaji. Damu ya mtu mbaya sana inasumbua sana na ukisha onja unajiona kama hakuna cha kuogopa.

Nawasilisha; JINSI ULIVYOMTENDEA YULE MDOGO NDIVYO ULIVYO NITENDEA MIMI'MUNGU ASEMA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom