Siasa zina tunufaisheje watanzania?

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,071
Tuna changamoto kubwa sana ya kuona ni jinsi gani siasa zinatunufaisha!
  1. Wengi wetu hasa wasomi wanasemaga hawataki siasa maana ni upuuzi ila wanashindwa kujua kuwa siasa ndio maisha yao asubuhi hadi usiku!
  2. Watu wa mtaani wanaona kuwa wanasiasa ndio wakupiga nao deal, labda waombe mlungula, au kuomba misaada tu!
  3. Watu wa dini na wale wa makabila wao wanaona watu wa jamii zao tu! Hawataki kujua votes zao au opinions zao zina impact kiasi gani ktk maisha ya umma!
  4. Mashabiki wa siasa wao na vyama na wagombea wao tu, hata kama ha!na tija wataendelea kuchagua haohao au vyama hivyo hivyo!
Hivi kweli kuna uwezekano wa kuwa na tija katika siasa zetu?
Je kuna haja ya kufuata just Sera na uwezo wa kiongozi rather than kuona factors nyingine ambazo hazi add values ktk utendaji wa viongozi?
Aina hizi za siasa kila baada ya miaka 10, tunaamka na matumaini na mashairi mapya (hapa kazi tu, ari mpya, kasi mpya etc, mabadiliko!!) Ila baada ya hapo tunaishi kwa mashaka na lawama kwa miaka mingine 10!
Je ni sisi tunakosea? Je ni wanasiasa ndio wanaokosea? Au hatujafikiri vya kutosha kuhusu siasa na manufaa yake kwa umma?
 
Hiyo ndio siasa na hata wewe katika hii thread unapiga siasa. Siasa haiepukiki labda uwe maiti. Bila siasa huna serikali, huna viongozi, huna mpangilio wa maisha na huna malengo katika maisha. Bila siasa huna tofauti na wanyama wa msituni au kwa lugha nyepesi huna akili.
 
Hiyo ndio siasa na hata wewe katika hii thread unapiga siasa. Siasa haiepukiki labda uwe maiti. Bila siasa huna serikali, huna viongozi, huna mpangilio wa maisha na huna malengo katika maisha. Bila siasa huna tofauti na wanyama wa msituni au kwa lugha nyepesi huna akili.
Hebu rudia tena kusoma post yangu!
Nadhani kuna kitu hujaelewa!
 
Back
Top Bottom