Siasa zetu zimehamia hadi benki

Crocozilla

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
471
250
Leo ni siku ya huduma kwa mteja huko CRDB. Mmmmh Tanzania bado sana aisee. Huwezi amini nimekaa toka saa 4 asubuhi ndo natoka kwa issue ndogo tu ya kadi. Inauma sana sana.

Tubadilike Watanzania, angalia vibenki vidogo vidogo vya nje ambavyo vinaingia sokoni kwetu viko vizuri sana shida yao matawi machache. Tuache siasa Watanzania tuende na kasi ya serikali hii!!

Jamani mabenki yote badilikeni siyo CRDB pekee hata NBC kuna siku nilikaa saa 3 eti vibanda vipo 8 teller wawili pekee!!!! Shame!!!
 

Muyobhyo

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
8,161
2,000
yaani hawa dada yangu ni jipu, mara unaambiwa connection iko slow,
 

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,918
2,000
Mtandao huwa kuna kipindi ukataka kabisa mnakaa muda kusubiria NETWORK irudi
 

Faru Kabula

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
12,859
2,000
Siasa zetu zimehamia hadi benki
Ungekuwa unaelewa maana ya neno 'siasa', naamini usingethubutu kuweka title hiyo. Watanzania wengi hufuata mkumbo, akiongea mtu wengine wanafuatisha tu bila hata kutafakari. Yaani kutohudumiwa haraka benki basi ndio unaita kuna siasa huko? Kuna tatizo fulani la elimu
 

Philipo D. Ruzige

Verified Member
Sep 25, 2015
6,395
2,000
Sasa hapo siasa inahusika vipi?
Hayo ni matatizo kwenye mfumo wa uendeshaji wa tawi husika
Btw kama umekuta foleni lazima ukae foleni

Alaf pale benki c kuna sanduku la maoni, je umelitendea haki? Pia si kuna meneja wa kitengo ch a huduma kwa wateja, je umempa malalamiki yako? Au umekimbilia jf tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom