Siasa Zetu Na Ufisadi

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,140
3,209
Jamani tumepiga siasa za kutosha na mara nyingi tumekuwa tukitupia lawama utawala kitu ambacho ni sahihi tu kama pia wananchi nasi tunamikakati endelevu.

sisi wananchi pia kwa namna moja ama nyingine tu mafisadi maana hatuzitumii nafasi zetu ktk kubuni mikakati inayoeleweka ya kuiokomboa nchi na tumebaki kuingalia tu serikali ituletee maisha bora mlangoni wakati sisi tumeketi vijiweni na kupiga bao na sogo ,hapa nieleweke sio wote lakini tulio wengi ndivyotulivyo.

Kwa uelewa wangu mfinyu ni kua serikali kamwe haiwezi uondoa hali TETE tuliyo nayo ila inachoweza kufanya ni kutengeneza mazingira ambayo kwayo wananchi wabunifu wataweza kuyatumia na kujiletea maisha bora,yawezekana kupiga kwetu usingizi ndiko kunawapa nafasi mafisadi kuzifisadi pesa zetu ,ukiangalia hata majirani zetu mfano wakenya wamekua wakitumia usingizi wetu kujinufaisha kutoka ktk malighafi yetu wenda kabisa sisi niwapiga kelele tusio na lolote wala chochote.

Hivyo humu ndani naamini kabisa kuna wataalamu na wazoefu wazuri tu na niomba pia tuchangie ktk haya-
mfano mtu
1.akitaka kuanzisha NGO ni NGO ipi? itafaa zaidi ktk kuwaamusha watanzania usingizini walio wengi
2.Ni NGO ipi na yenye mtindo upi ambayo kwayo itakua rahisi kupata wafadhili ili ipate kuedesha shughuli kwa ubora zaidi.
3. je NGO ya mtindo upi iliyo muafaka kwa sasa.
4.je ni process zipi ambazo NGO inapitia ili ipate haki ya kuomba msaada mfano IMF na kwingineko

Naomba tujadili haya wenda tunaweza kuja na majibu mazuri zaidi badala ya kuitegemea serikali zaidi.
 
wataalamu wa NGOs na wenye ujuzi tutatulieni utata huu
 
Mkama,
wachamawe!! vipi Sato wanapatikana? boss tumeukumbuka ugali wa muhogo na sato,ugali huo wa muhogo unga wake uwe umetwangwa toka mwambani,radha yake chachu chachu hivi daaaa!!!!!

Mkama nadhani unashindwa kutofautisha ni kipindi gani tulichopo na sisi watanzania tuna hali gani kwa sasa, hoja yangu ni kuwa kwa kuwa wewe umeshaona kuwa serikali imeandaa mazingira mazuri ya kuboresha maisha kwa watanzania, ningependa utoe mchanganuo wa jinsi serikali yetu ilivyojipanga kuboresha maisha ya watz,
Lakini utwambie mara ya mwisho kurudi kule kjj kwenu ilikuwa lini? pia utwambie wale wanakjj uliwakuta wana hali gani kwa sasa?
 
Zanzibar inajifunza nini toka Bolivia.

KAMA kuna kura yoyote ya maoni inayohitajika huko Tanzania Visiwani basi ni ile ya kuwauliza Wapemba je wanataka kuwa jimbo huru ndani ya Zanzibar na Tanzania.

Mantiki ya hili ni kutokana na ukweli ambao CCM imeshindwa hadi leo kuuona. Na ukweli huo si mwingine ila Pemba nzima inaikubali na CUF na wanataka kutawaliwa na serikali ya CUF na sio SMZ.

Somo ambalo bado ni bichi kabisa ni lile la Santa Cruz [Pemba ya Bolivia] ambayo wananchi wake wametumia demokrasia kumpasha kiongozi wa nchi nzima, Bw. Evo Morales [Amani Abeid Karume wa Bolivia] kuwa wao wanataka kuliendesha jimbo lao wao wenyewe ili wahakikishe wanautumia uchumi wao kunufaisha watu wao.
Hili limewezekana kutokana na vuguvugu na harakati za wananchi, wafanyabiashara, wanasiasa jasiri na wasomi wa jimbo hilo la Santa Cruz kudai haki ya kuliendesha jimbo lao kwa namna ambayo wao wanaamini itakuwa bora zaidi kwao kuliko kushurutishwa kufuata kile uongozi wa nchi nzima unachokitaka [ambao wanaamini ni gharama na hasara kubwa kwao].

Tayari wana Santa Cruz sasa wanajiita wa-Crucenos na ushindi wao katika kura ya maoni ni tiketi ya kuwa na jimbo linalotawaliwa na watu waliowachagua wao na sio vinginevyo.

Kwa miaka mingi Bolivia nchi yenye utajiri mkubwa wa maliasili lakini ni masikini wakubwa imekuwa ikitawaliwa na madikteta na viongozi wabinafsi, mafisadi na wasioona mbali na mbele.

Wakazi wa Santa Cruz kama walivyo Wapemba wanaamini kwamba wana uwezo wa kufanya jimbo lao kuwa Dubai ya huko kwao.

Kama kawaida ya viongozi wabovu wanapoona sehemu fulani ya nchi yao inataka kujitenga na kujiendesha yenyewe kwa ustawi na ufanisi zaidi kwa watu wao, Bw. Morales na wafuasi wake walianza kuwahujumu wana Santa Cruz mara baada ya matokeo ya kura ya maoni kutangazwa. Achilia mbali maelfu ya watu waliokwaza katika kujiandikisha na kupiga kura kabla ya hapo.

Kinachotokea huko Bolivia ni mwanzo tu wa utabiri wa watu kama Alvin Toffler ambao wanaamini miaka ya 2010 kuendelea mbele itakuwa ni miaka ya watu na maeneo mengi zaidi toka Afrika hadi Uchina kudai haki ya kujitawala na kuendesha maisha yao wenyewe hata wakiwa wachache namna gani. Sababu kubwa ikiwa kukosa viongozi wanaoweza kuongoza watu wengi na maeneo makubwa vizuri.

Uwezo wa kuongoza duniani hivi leo umezidi kuwa dini kadri miaka inavyokwenda.

Ni dhahiri baada ya Santa Cruz majimbo mengine kadhaa ya Bolivia yanaweza nayo kuamua pia kuendesha mambo yao wenyewe chini ya serikali ya shirikisho.

Ujumbe kwa SMZ na serikali ya Muungano ya Tanzania ni kuwa wananchi wa Pemba wanashindwa kuwaelewa kwa kukataa muafaka na kutoa mwanya kwa watu wenye itikadi kama za wa-Crucenos wa Santa Cruz [Pemba ya Bolivia] na wao kuamua kudai haki ya kuongozwa na wale waliowachagua na sio vinginevyo. Hii ni haki yao, na hii ni demokrasia!
Hakika mkataa pema pabaya panamuita. Chagueni kati ya serikali ya mseto au Wapemba kuiga kutoka Santa Cruz siku moja ambayo si mbali sana kutoka sasa!

Tukiulize Chama cha Mafisadi [CCM] ni wapi zaidi ya kwa Robert Mugabe, huko Zimbabwe, wamewahi kuona mtu anashinda uchaguzi kisha anazuiwa kuwatawala waliomchagua kama sio tu Zanzibar!

mwisho
 
Isayamwita
Wachatata mwana wasu !!!ebwana sato na chengu kwa wingi wewe tembelea tu kule maeneo.

Hatujaelewena mkuu!!! mimi sijasema Serikali imeshakwisha andaa mazingira lahasha !! wasiwasi wangu wenda ukawa ni upeo wangu mdogo wa kuona mambo nikua watanzania tulio wengi tumejikita zaidi kuitegemea serikali ,yani serikali ituletee ajira pia maisha bora kitu ambacho hakiwezekani.
Na kelele nyingi tunapiga ukiziangalia kwa makini utakuta tunaitaka serikali ifanye mambo ya kimuijiza.

Mimi nafirikiri tungeipigia kelele serekali itutengenezee mazingira murua ,yani kulegeza masharti yakufungua makapuni ,NGOs pia na mashirika kwa watanzania na kuyapiga support ama kuyatwanga mikopo isiyo na urasimu makapuni yote ya watanzania yenye determinations ktk kuwezesha maisha bora kwa mtanzania.

Ndio maana Nikafikiri ni vyema kwa vile humu ndani kuna wataalamu tujadili jinsi na miundo ya NGOs zenye tija zaidi na tukishapata muundo tuanze kuishinikiza serikali itujengee haya mazingira.

Kule kijijini kwetu aisii ni choka mbaya tena mbaya ndio maana kunahitajika juhudi za makusudi za sisi kwa kila mmoja anakotoka akapaendeleze maana tukisubiri serikali Duuuuuuuuu maeneo mengine hata serikali haipooooo sisi ndio tunajua.
 
Zanzibar inajifunza nini toka Bolivia.

KAMA kuna kura yoyote ya maoni inayohitajika huko Tanzania Visiwani basi ni ile ya kuwauliza Wapemba je wanataka kuwa jimbo huru ndani ya Zanzibar na Tanzania.

Mantiki ya hili ni kutokana na ukweli ambao CCM imeshindwa hadi leo kuuona. Na ukweli huo si mwingine ila Pemba nzima inaikubali na CUF na wanataka kutawaliwa na serikali ya CUF na sio SMZ.

Somo ambalo bado ni bichi kabisa ni lile la Santa Cruz [Pemba ya Bolivia] ambayo wananchi wake wametumia demokrasia kumpasha kiongozi wa nchi nzima, Bw. Evo Morales [Amani Abeid Karume wa Bolivia] kuwa wao wanataka kuliendesha jimbo lao wao wenyewe ili wahakikishe wanautumia uchumi wao kunufaisha watu wao.
Hili limewezekana kutokana na vuguvugu na harakati za wananchi, wafanyabiashara, wanasiasa jasiri na wasomi wa jimbo hilo la Santa Cruz kudai haki ya kuliendesha jimbo lao kwa namna ambayo wao wanaamini itakuwa bora zaidi kwao kuliko kushurutishwa kufuata kile uongozi wa nchi nzima unachokitaka [ambao wanaamini ni gharama na hasara kubwa kwao].

Tayari wana Santa Cruz sasa wanajiita wa-Crucenos na ushindi wao katika kura ya maoni ni tiketi ya kuwa na jimbo linalotawaliwa na watu waliowachagua wao na sio vinginevyo.

Kwa miaka mingi Bolivia nchi yenye utajiri mkubwa wa maliasili lakini ni masikini wakubwa imekuwa ikitawaliwa na madikteta na viongozi wabinafsi, mafisadi na wasioona mbali na mbele.

Wakazi wa Santa Cruz kama walivyo Wapemba wanaamini kwamba wana uwezo wa kufanya jimbo lao kuwa Dubai ya huko kwao.

Kama kawaida ya viongozi wabovu wanapoona sehemu fulani ya nchi yao inataka kujitenga na kujiendesha yenyewe kwa ustawi na ufanisi zaidi kwa watu wao, Bw. Morales na wafuasi wake walianza kuwahujumu wana Santa Cruz mara baada ya matokeo ya kura ya maoni kutangazwa. Achilia mbali maelfu ya watu waliokwaza katika kujiandikisha na kupiga kura kabla ya hapo.

Kinachotokea huko Bolivia ni mwanzo tu wa utabiri wa watu kama Alvin Toffler ambao wanaamini miaka ya 2010 kuendelea mbele itakuwa ni miaka ya watu na maeneo mengi zaidi toka Afrika hadi Uchina kudai haki ya kujitawala na kuendesha maisha yao wenyewe hata wakiwa wachache namna gani. Sababu kubwa ikiwa kukosa viongozi wanaoweza kuongoza watu wengi na maeneo makubwa vizuri.

Uwezo wa kuongoza duniani hivi leo umezidi kuwa dini kadri miaka inavyokwenda.

Ni dhahiri baada ya Santa Cruz majimbo mengine kadhaa ya Bolivia yanaweza nayo kuamua pia kuendesha mambo yao wenyewe chini ya serikali ya shirikisho.

Ujumbe kwa SMZ na serikali ya Muungano ya Tanzania ni kuwa wananchi wa Pemba wanashindwa kuwaelewa kwa kukataa muafaka na kutoa mwanya kwa watu wenye itikadi kama za wa-Crucenos wa Santa Cruz [Pemba ya Bolivia] na wao kuamua kudai haki ya kuongozwa na wale waliowachagua na sio vinginevyo. Hii ni haki yao, na hii ni demokrasia!
Hakika mkataa pema pabaya panamuita. Chagueni kati ya serikali ya mseto au Wapemba kuiga kutoka Santa Cruz siku moja ambayo si mbali sana kutoka sasa!

Tukiulize Chama cha Mafisadi [CCM] ni wapi zaidi ya kwa Robert Mugabe, huko Zimbabwe, wamewahi kuona mtu anashinda uchaguzi kisha anazuiwa kuwatawala waliomchagua kama sio tu Zanzibar!

mwisho

Mkuu naheshimu falsafa yako lakini maada hii inahitaji kunyanyambua mbinu mhimu ktk tatizo lilo adresiwa hapo juu.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom