Siasa zetu na hatima ya uchumi wa Mtanzania

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
6,276
12,335
Halimashauri hazitoi lesseni kwa wakati hivyo wanalaza mitaji kwa muda mrefu hadi miezi mitatu

TRA wanafanya ukadiriaji kwa kukomoa

Makato ya kutuma na kupokea hela yameongezeka hivyo kuchangia kuua biashara.

Covid-19 imeongeza gharama nyingi za misiba na matibabu kwa ndugu wasiojiweza.

Gharama za internet na simu zimepanda.

Bei ya mafuta ya kula imepanda hivyo vyakula navyo vimepanda.

Bei ya ngano nako ipo juu.

Bei ya mafuta ya petrol ipo juu kwa uzembe na ongezeko la makato.

Ushuhuda
Mimi ni mkulima na mfungaji ila huwa nikipata hela naenda kuweka kwenye kiofisi changu Cha Mpesa hapo mjini ili izunguke na ipate faida kipindi nasubiri msimu wa kilimo lakini toka mwezi wa 7 hadi leo naona nimeingia hasara ya 2Milion Kati ya 11 nilizoweka kutokana na gharama kubwa za uendeshaji ofisi huku wateja wakiwa wamepotea.

Natarajia jumatatu niende TRA nikafunge biashara.Hela inapotea,madeni yanaongezeka ni Bora tu nibaki kijijini japo bei ya mahindi nako changamoto ila Bora nikachunge mbuzi na vijana kuliko kukaa mjini nikipoteza hela kwa ujinga wa wanasiasa wetu.

Je, vipi kwenu mmeona msaada positive wa siasa zetu kwenye ukuaji wa uchumi wa wananchi?

Je, serikali yetu haitukandamizi ili tudidimie?

Nimechoka naona umasikini ukinitafta natamani kujiua ili niepukane na hali hii iliyopo mbele yangu
 
Back
Top Bottom