Siasa zetu hazina faida kwa wengi

pureman2

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
1,494
2,538
Sasa ni bayana Wananchi tuamke na kusahau siasa kama njia ya matumaini mapya.

Siasa imekua ulaji na mwenye kisu kikali ndo anayekula. Makundi ya watu wenye nguvu ndo wanufaika wa mfumo huu.

Kama mnajitoa kwa wana siasa hadi mnalipa gharama ya uhai wenu , kitiwa ulemavu, kusota rumande, kuchalangwa mapanga na virungu na kuacha mayatima ila baada ya hapo wanasiasa wanajifungia na kualikana mezani na kuanza kuifaidi nchi.

Lazima Wananchi tuione hila hii ya Wanasiasa. Tujiweke kando, tupigane kivyetu coz hakuna tumaini kwa hawa viongozi wa siasa.

Wamejaa ubnafsi, njaa, usaliti na roho mbaya. Hawajali maumivu wanayolipa wafuasi wao bali wao utanguliza maslahi yao.

Wakiwa mbele zetu utazani ni watu. Utulisha upepo na matumaini dake ili wao wapate fursa ya kuishi ndoto zao.

Tazama wanavyojilipa? Tazama wanavyojitungia sheria, tazama wanavyojipa kipaumbele. Kwa kazi ipi yenye kutumia akili na ubobezi wanayoifanya yenye kustahili mishaara minono na marupurupu kibao.

Wasikilize wanavyojenga hoja!! Watazame wanavyojipendekeza na kusahau wajibu wao!! Kipi so special cha kustahili upendeleo huo wanajipa?? Jibu ni lahisi tubkuwa siasa ni deal na wanudaika ni aao na washirka wao wanaopewa connection.

Mwananchi usilipe tena gharama ya kuwasupoort wanasiasa. Hawana la kukuongezea bali ukicheza tu watakutumia kama fursa ya wao kupanda ngazi ya ulaji

Tususie siasa hadi tuwe na katiba mpya inayoruhusu kuwafungulia mashitaka hata kipindi wawapo madarakani.

Inayoruhusu kuanzisha mchakato wa kuwatoa madarakani hata kabla ya kutimiza muda wa mzunguko wa uongozi.

Katiba itakayo wapokopnya mamlaka ya kutunga na kupitisha mambo ambayo wananufaika nayo right away
Katiba itakayotupa wananchi nguvu ya kupinga uhalali wao baada ya uchaguzi

Kifupi ni kuwa na katiba itakayotoa taswira kazi ya siasa ni utumishi na sio ulaji.

Pale watakapokua radhi kufanya siasa kwa ujira kama wa walimu, wauguzi na madaktari wetu.

Nje na hapo usifanye kazi yoyote ya kumsaport mwana siasa bila ya kukulipa.

Leo niishie hapa ila ndo nimetangaza harakati juu ya kupinga mfumo uliopo wa siasa nchini.
 
Naunga mkono hoja, hii nchi imejaa wafanyabiashara wa siasa, ni vyema raia tukatae kutumika kama ngazi ya kuwafikisha watu fulani kwenye neema.
 
Masikini wanauwana kwa faida ya watawala na wanasiasa. Police (masikini) wanatumwa na watawala kuuwa wafuasi wa wanasiasa (masikini) then wanasiasa na watawala ukaa meza moja baada ya arobaini kula keki na kunywa mvinyo huku mapolisi na wafuasi wa wanasiasa wakipiga miayo ya njaa.
 
Tuachane na Madj.....tuangalie familia zetu,Madj wametupotezea sana muda ilhali ni wafanyabiashara..!
 
Back
Top Bottom