Siasa Zakielemea Chuo Kikuu Mlimani

Ant-Ufisadi

Member
Mar 12, 2008
29
0
Uchaguzi wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu mlimani imeingia katika wakati mgumu baada ya vyama vya siasa na mafisadi kuingilia katika uchaguzi huo. Hadi kufikia sasa mgombea mmoja raia wa kigeni ambaye ameonekana ni tishio kwa chama tawala na mafisadi kuanza kutishiwa na kisha kusimamishwa masomo kwa muda usiojulikana yeye na kambi yake nzima ya kampeni.
Mambo yanayowezekana kuwa sababu ya yeye kusimamishwa ni pamoja na kuhoji matumizi ya hela za mradi wa MLIMANI CITY pamoja na kauli zake za kuwa wagombea wengine ni makada wa CCM, na kwamba yeye hata kuwa tayari kuendeshwa na wanasiasa
 
Uchaguzi wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu mlimani imeingia katika wakati mgumu baada ya vyama vya siasa na mafisadi kuingilia katika uchaguzi huo. Hadi kufikia sasa mgombea mmoja raia wa kigeni ambaye ameonekana ni tishio kwa chama tawala na mafisadi kuanza kutishiwa na kisha kusimamishwa masomo kwa muda usiojulikana yeye na kambi yake nzima ya kampeni.
Mambo yanayowezekana kuwa sababu ya yeye kusimamishwa ni pamoja na kuhoji matumizi ya hela za mradi wa MLIMANI CITY pamoja na kauli zake za kuwa wagombea wengine ni makada wa CCM, na kwamba yeye hata kuwa tayari kuendeshwa na wanasiasa


Ki-uhalali, sio vizuri na wala sio haki mtu kusimamishwa chuo kwa ajili ya hizi sababu. Kama ni kweli, na kama hakuna jambo lingine, basi inabidi kufanyike mapinduzi makubwa katika Elimu yetu ya Kitanzania.

Lakini ndugu yangu Ant-Ufisadi, hebu basi tenganisha kati ya Ufisadi na Chama tawala (CCM) maana hata vyama vya upinzani navyo kuna mafisadi lakini Chama Cha Mapinduzi (CCM) sio fisadi.
 
.

Lakini ndugu yangu Ant-Ufisadi, hebu basi tenganisha kati ya Ufisadi na Chama tawala (CCM) maana hata vyama vya upinzani navyo kuna mafisadi lakini Chama Cha Mapinduzi (CCM) sio fisadi.

Nadhani nimejitahidi kuunganisha matukio kwa uzuri. Jamaa wamesimamishwa masomo kwa kile kinachodhaniwa ni
1. Kusema CCM wanafadhili kampeni za mgombea ambaye wanamtaka wao
2. Mgombea huyo kusema atafuatilia matumizi ya pesa za mradi wa MLIMANI CITY.
 
UDSM kwachafuka

Mgomo mwingine wanukiana Lucy NgowiMGOMO mwingine unanukia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), sehemu ya Mlimani, baada ya utawala wa chuo hicho kusimamisha uchaguzi wa rais wa wanafunzi.

Uchaguzi huo umesimamishwa baada ya utawala wa chuo kuhoji uhalali wa kuwepo chuoni hapo mmoja wa wagombea urais, jambo ambalo wanafunzi wanalipinga pamoja na kusimamishwa kwa wanafunzi wengine watano kwa muda usiojulikana.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya chuo hicho vimeeleza kuwa, baada ya uchaguzi huo uliopangwa kufanyika juzi kusimamishwa, utawala wa chuo hicho ulitoa tangazo la kutomtambua mmoja wa wagombea.

Habari zinaeleza kwamba barua ya kutomtambua mgombea mmojawapo ambaye ni raia wa Uganda, Odong’ Odwar, ilitolewa na Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo na kusambazwa na Profesa Makenya Maboko anayeshughulikia taaluma, utafiti na ushauri wa kitaalamu.

“Barua hiyo ilionyesha kuwa imesainiwa na Profesa S. Luoga na kueleza kuwa ofisi yake inahitaji ufafanuzi wa kuwepo kwa Odwar kama mwanafunzi katika chuo hicho. Hivyo inamtaka apeleke vyeti vyake halisi alivyopata kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita na awe amevikabidhi ifikapo Jumatatu (kesho) saa 6 mchana,” alisema mmoja wa wanafunzi aliyezungumza na Tanzania Daima.

Kwamba iwapo Odwar atashindwa kuwasilisha vyeti hivyo, hatatambulika kama mwanafunzi wa chuoni hapo.

Habari zaidi zilieleza kuwa, hali hiyo imetokea baada ya uongozi wa serikali ya wanafunzi (Daruso), kuandika barua ya kupinga kusimamishwa kwa uchaguzi.

“Kinachotushangaza sasa hata tuweze kufikiria mbali zaidi juu ya uchaguzi huu kwamba unaingiliwa na baadhi ya vyama vya siasa, ni kwamba kwa kawaida wanafunzi wanapoomba nafasi ya kujiunga na chuo, huulizwa copy halisi za vyeti vyao vya kumaliza elimu ya sekondari, unapovionyesha ndipo unapopewa usajili.

“Lakini kwa mwenzetu huyu Mganda, chuo hakikumpa barua yoyote kuwa hakufanya taratibu hizo, na mwaka 2006/2007 alichaguliwa kuwa mbunge katika serikali ya wanafunzi, kutoka Kitivo cha Sheria,” kilisema chanzo chetu.

Wakati huo huo, taarifa nyingine zilizotufikia zimesema kuwa jana mchana wanafunzi watano wanaomuunga mkono Odwar walisimamishwa masomo na uongozi wa chuo kwa muda usiojulikana.

Mmoja wa wanafunzi waliosimamishwa alilieleza gazeti hili kuwa, alipokea barua iliyosainiwa na Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Rweikaza Mukandala ikieleza kuwa Kamati ya Nidhamu imemsimamisha kwa kumhusisha na utovu wa nidhamu, na hali ya kutokuwepo kwa amani chuoni hapo.

Hivyo kwa kutumia mamlaka aliyonayo, amewasimamisha chuo mpaka hapo hatua nyingine zitakapochukuliwa na wao kujulishwa. Pia wametakiwa kukabidhi vifaa vya chuo na kuondoka katika maeneo ya chuo hicho baada tu ya kupokea barua hizo.

Wanafunzi waliosimamishwa ni Clinde David wa mwaka wa pili, ambaye ni Katibu wa Kitivo cha Biashara na Uongozi, Salum Ali wa mwaka wa kwanza, ambaye ni mbunge mpya katika Kitivo cha Sheria, Owawa Steven mwaka wa pili na mbunge kutoka Kitivo cha Biashara na Uongozi, Ali Selemani mwaka wa tatu na mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Yona wa mwaka wa kwanza katika Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii.

Wakati matukio yote hayo yakitokea, kikao cha bunge la wanafunzi kiliendelea kwa siku nzima jana ambapo mbali na ajenda nyingine muhimu zilizojitokeza, iliundwa bodi mpya ya rufaa ya uchaguzi baada ya ile ya awali kujiuzulu, hali iliyosababisha uongozi wa chuo kusitisha uchaguzi.

“Kuna mambo mengi ya msingi yanayoendelea kujadiliwa katika kikao cha bunge kwani hali ni ngumu. Yaliyojitokeza ni mambo ya simanzi kwa wanafunzi. Kuna tafsiri nyingi kwa kila unayemuuliza kuhusu mkanganyiko huo uliojitokeza.

“Eti utawala umeanza kumhoji mgombea awape vyeti vyake original. Je, muda wote walikuwa wapi? Huyu Mganda utawala haumtaki,” alisema mmoja wa wajumbe wa kikao cha bunge la wanafunzi kilichokuwa kikiendelea.

Alisisitiza kuwa, endapo chuo kitamuondoa huyo raia wa Uganda, na pia hakitawarejesha wanafunzi watano waliosimamishwa, wanafunzi wameamua kugoma hata kama uongozi utaamua kukifunga chuo hicho.
juu
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 2 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
WANAFUNZI WAKIGOMA SABABU YA KUCHELEWESHA UCHAGUZI WAO CHUO KIKUU WANA AGENDA YA SIRI.
TUMEZOEA KUSIKIA WANAGOMA SABABU YA KUKOSA CHAKULA, POSHO NDOGO NA KUPANDA KWA KARO PENGINE NA KUTORIDHIKA KWA ELIMU WAPATAYO.


na Msomi TzDaima - 13.04.08 @ 10:28 | #6293

Kwa maoni yangu jinsi ninavyoona ni kwamba huyu mwanafunzi ,ameletwa na mtu mkubwa ,sasa baada ya kuona anaweza kuwa mwiba kwa wakufunzi,Ndiyo maana wamempa masharti ya kuleta vyeti, Siyo wote huwa wanakubali kile wanachotaka wakufunzi.Kwanini wakufunzi,Waanze kuuliza maswala ya vyeti ,kwani wakati anaingia hawakuliona hilo?Au wanaendesha chuo kama cha mtu binafsi.Kwanini wafukuze wanafunzi wakati wanatafuta viongozi wao?Je,hakuna sheria inayotoa mwongozo kuhusu usajili wa wanafunzi,na pia katiba ya uchaguzi.Mnajua nyie wakufunzi mnanichekesha,hicho ni chuo kikuu hakitakiwi kiwe na mambo kama haya ,inadhihirisha njinsi mnavyoongoza.Kwanza mnasomwa na dunia nzima kwenye magazeti,NAPIA TV RADIO.Tunatatizo la richmund,ufusadi,madini, mbuga zetu ,ardhi yetu,tunaingia kwenye ziwa Wanaweka kiwanda cha magadi,wawafukuze ndege na mazalia yao,Sakata la rada,Reli yakati kapewa mhindi,na wananchi kuteseka kwa usafiri na kupewa wafanyakazi mshaharamidogo,wanawafukuza wazawakwenye aridhi ya asili kuwapa muwekezaji,Haya ananichanganya ,Leo mnawafukuza vujana kwa sababu zenu binafsi.Nafikiri mnawaogopa hawa vijana wakiingia madarakani mtapata matatizo.Tanzania inaonekana kanakwamba serekali imehama ,na ipo kwenye mikono ya watu binafsi.Punguzeni matatizo vyuoni kwa kusaidia vijana pale wanapokosea muwasahihishe, na kuwakosoa kwa njia za kidiplomasia na siyo fukuza fukuza kwani watz tumechoka kusikia migomo.Ikitokea basi iwe niya kunga mkono kuhusu ufisdi au CAF NA MUAFAKA.

na mtz mwenye uchungu, tz, - 13.04.08 @ 11:00 | #6301

http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/4/13/habari4.php
 
hivi na vyou vya wenzetu wakianza kutufukuza kwa kutupa wiki moja kuja na vyeti halisi itakuwaje?
 
Hapo kazi ipo kweli kweli. Chuo kikuu ndio mahali pa kufanya kila aina ya majaribio ya uongozi. Sasa kama wanafunzi wanafukuzwa kwasababu hawaiungi mkono serikali kuu ya nchi, hapo ni tatizo kubwa kweli kweli.

Usipokuwa huru wa mawazo chuo kikuu, utakuwa huru wapi tena?

Wawaachie wanafunzi kuwa na mawazo yoyote yale ili mradi hawavunji sheria.

Huko mbele tutatoa graduates ambao wanaitikia kila kitu, watu kama hao hata kwenye jamii ni mzigo mtupu.
 
Hapo kazi ipo kweli kweli. Chuo kikuu ndio mahali pa kufanya kila aina ya majaribio ya uongozi. Sasa kama wanafunzi wanafukuzwa kwasababu hawaiungi mkono serikali kuu ya nchi, hapo ni tatizo kubwa kweli kweli.

Usipokuwa huru wa mawazo chuo kikuu, utakuwa huru wapi tena?

Wawaachie wanafunzi kuwa na mawazo yoyote yale ili mradi hawavunji sheria.

Huko mbele tutatoa graduates ambao wanaitikia kila kitu, watu kama hao hata kwenye jamii ni mzigo mtupu.Mkandara hakuwekwa pale kwa kunahatisha .CCM knew what they were doing .Mtashuhudia mengi sana .Mara gavana Butiama huku pesa za EPA inakuwa giza nene mara UDMS lazima kiongozi awe CCM wanaogopa kuwapata akina Zitto wengine .Pole zao Dunia inakuwa kijiji na moving so fast.Walianza kw aubaguzi kwamba ni Muganda kisa anataka madaraka typical CCM sasa wana hoji vyeti sawa na Ulimwengu na yule aliyekuwa CCM kule Uhayani .

Mkishindwa hoja inakuwa vioja na hapa ndiyo ishara kwamba wakishindwa kwa hoja na kuhonga huanza mambo ya ajabu sana .Hii ni reflection ya mambo kama Mwafaka na uchafu mwingine wa CCM .
 
Uchaguzi wa wanafunzi ulisimamishwa juzi usiku kwa barua ya kaimu makamu mkuu wa chuo profesa Maboko Makenya kwa kusema eti kwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya rufaa amejiuzulu basi wanafunzi hawatatendewa haki haswa watakao kuwa na rufaa zao ila la kuustaajabisha ni kuwa aliruhusu uchaguzi wa makamu wa rais uendelee na huku akiusimamisha ukle wa nafasi ya urais pamoja na wenyeviti wa vitivo.

Jana kuna wanafunzi watano ambao mmoja wapo alikuwa ni meneja wa kampeni wa huyu ndugu kutoka Afrika ya m,ashariki UGANDA ambaye anaitwa Odory Odwang na meneja wake wa kampeni anaitwa Ole Wawa pamoja na wanafunzi wengine watano wamesimamishwa kwa muda usiojulikana sasa huu ni uhuni na wapenda demokrasia wote tusiangalie tuu kule kwa Mugabe na kulalamika hata hapa kwetu kuna wahuni wa kiutawala kama chuo kikuu cha DSM ,nawatafuta waadhirika na huenda leo jioni nikaweza kuonanan nao ili wanipe hizo barua na nyaraka then nitaweza kuwaletea hapa na kuona jinsi wahuni hawa wanataka kuendesha chuo kama tawi la CCM.

hii ni mara ya tatu kwa wanafunzi kutoka Afrika mashariki kunyiwa fursa ya kuongoza hapa chuoni, itakumbukwa habari ya yule kijana wa kenya mika ya tisini pamoja na yule msichana kutoka kenya pia miaka ya tisini.
 
Ki-uhalali, sio vizuri na wala sio haki mtu kusimamishwa chuo kwa ajili ya hizi sababu. Kama ni kweli, na kama hakuna jambo lingine, basi inabidi kufanyike mapinduzi makubwa katika Elimu yetu ya Kitanzania.

Lakini ndugu yangu Ant-Ufisadi, hebu basi tenganisha kati ya Ufisadi na Chama tawala (CCM) maana hata vyama vya upinzani navyo kuna mafisadi lakini Chama Cha Mapinduzi (CCM) sio fisadi.

Kama viongozi wa juu wa ccm ni mafisadi na wanaendeleza ufisadi then hicho chama utakiita vipi? chama kisafi lakini chenye viongozi wote mafisadi? kwa nini utumie jina refu hivyo wakati unaweza kufupisha tu na kusema chama cha mafisadi?
 
Hivi wasomi wa udsm yani wadhamili kweli wamebobea?? hiki chuo hakiwezi pitisha miezi miwili bila wanafunzi kukaa nje ya madarasa siku kadhaa.
udsm ni badala ya kusaididia inakua mzigo kwa taifa.
 
Mimi ndiyo maana wanafunzi wetu wakifanya fujo nawaelewa. Sikubaliani nao lakini nawaelewa!


Wewe shy ndiyo maana unajiita mchambuzi Uchwara nadhani ni njaa inakusumbua .Samahani wana bodi umri wangu na maneno machafu haya ni tofauti lakini huyu traitor mwendekeza njaa anajiita mchambuzi wakati bado ananuka ubwa ubwa wa shingo kanitia hasira .Museveni kafanya nini hadi useme analeta tamaa zake ? Mimi nina wasi wasi na Diplomatic raw maana jamaa ataenda Ubalozini na kisa itakuwa ni CCM kumletea zengwe .Majuzi tulipiga kelele ubaguzi kwa vijana wetu nje ya Nchi leo Chuo na serikali ina simamia ubaguzi ? Museven am sure atataka kujua zaidi maana huwa anawapa support sana wananchi wake .Ndiyo kwanza kazi imeanza .Uongozi wa mabavu hongo na kuunga unga una madhara sana tumevuka mipaka sasa .Kisa tuna watu wana akili kama za shy .Hii bwana shy si ishu ya vijana wa JF na uchakubimbi wako .
 
Siku hizi siasa za Tanzania zinaingilia kila sehemu hata mashinani. Hapa naona hata chuo vyama vina mikono yake. Mkimchagua muganda atafumbua watu macho, halafu hawa hawawezi kuahidiwa mambo matamu kama baadhi walioweza kubadilishwa baada ya kupata uongozi.

Hii ndiyo watu wanasema Tz tuna demokrasia. Demokrasia ya tanzania nahisi imekaa kimafia mafia.
 
Hawa jamaa inaonyesha kweli wanawasiwasi na huyu jamaa na kumwogopa kama atawaumbua.
Ndio maana unapotaka kuwa kiongozi ama mushindani unatakiwa usiaje loop hole kiasi kwamba mpinzani wako akatumia hicho kukuangusha.
Hapo wakituambia tunapitia nyaraka za wagombea wote ili kuona kwamba wako chuoni kiuharani ili wasije ikawa badaye wana kiongozi mwenye walakini .
Sasa jamaa kama vp afanye mpango kwao wamtumie vyeti fast.Au kama anavyo hapo awape.
Ila swali linabaki kama itakuwa hana vigezo walimpaje registration?
 
Hawa jamaa inaonyesha kweli wanawasiwasi na huyu jamaa na kumwogopa kama atawaumbua.
Ndio maana unapotaka kuwa kiongozi ama mushindani unatakiwa usiaje loop hole kiasi kwamba mpinzani wako akatumia hicho kukuangusha.
Hapo wakituambia tunapitia nyaraka za wagombea wote ili kuona kwamba wako chuoni kiuharani ili wasije ikawa badaye wana kiongozi mwenye walakini .
Sasa jamaa kama vp afanye mpango kwao wamtumie vyeti fast.Au kama anavyo hapo awape.
Ila swali linabaki kama itakuwa hana vigezo walimpaje registration?

Hawa jamaa ma prof uchwara ni wapumbafu tu,kuwaita ma prof nikudharirisha u prof.
Yani ktk hali ya kawaida wao ndio walipaswa kufukuzwa kazi na wapigwe jela ndio huyo mganda naye afukuzwe shule.
Ina maana huyo mganda aliingia ofisini mwao akajifanyia usajiri,kila mwaka anajitengenezea ID ,pia INDEX hua anajisainisha mwenyewe na kujipitisha mwaka mwenyewe.au UDSM hawana INDEX ??
Hao wahafidhina wa UDSM wala hawafai kuwa watu waliomaliza hata form six.kuwaita prof ni kudharirisha Elimu, prof hawazi kuwa mjinga kiasi hicho.
 
Hawa jamaa ma prof uchwara ni wapumbafu tu,kuwaita ma prof nikudharirisha u prof.
Yani ktk hali ya kawaida wao ndio walipaswa kufukuzwa kazi na wapigwe jela ndio huyo mganda naye afukuzwe shule.
Ina maana huyo mganda aliingia ofisini mwao akajifanyia usajiri,kila mwaka anajitengenezea ID ,pia INDEX hua anajisainisha mwenyewe na kujipitisha mwaka mwenyewe.au UDSM hawana INDEX ??
Hao wahafidhina wa UDSM wala hawafai kuwa watu waliomaliza hata form six.kuwaita prof ni kudharirisha Elimu, prof hawazi kuwa mjinga kiasi hicho.Inaonyesha kuna jambo na maprof wa UDSM, weka hoja sio matusi, ni nini hasa?
 
Inaonyesha kuna jambo na maprof wa UDSM, weka hoja sio matusi, ni nini hasa?

Wewe unaona ni sahihi eti? vitu vingine vinaudhi hadi unashindwa jizuia.
kujenga hoja vizuri naomba unijibu maswali haya marahisi kabisa?
1.UDSM ID zao ziko valid mda gani?
2.UDSM wanawapa wanafunzi wao INDEX au La??
3.je hua wanatumia staili ipi kujua huyu kapanda mwaka/ama karudia somo.?
4. Je UDSM hua hakuna vipindi ambavyo ni kompasare ambavyo prof/tutor anaitisha mahudhurio.?
5.UDSM hua wanasajiri watu kiholela tu harafu wakishaingia chuoni ndio wanaitisha vyeti kuona uhalali wao wakuwepo chuoni?? ama huwa wanasajiri vipi wanafunzi wao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom