SIASA ZAINGIA MAKANISANI! Ni maslahi au inakuaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SIASA ZAINGIA MAKANISANI! Ni maslahi au inakuaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Teamo, Feb 23, 2009.

 1. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Wapendwa wanajamii!
  Mishoni mwa wiki iliyopita nikiwa mbele ya televisheni,nilivutiwa kuangalia mahubiri ya kipindi kimojawapo cha dini ya kikriso katika moja ya televisheni maarufu yenye makao yake makuu jijini mwanza.

  Mahubiri aliyokuwa akiyatoa mchungaji huyu maarufu,ambaye pia ni askofu mkuu katika kanisa hilo husika lenye makao makuu maeneo ya rufungira barabara ya sam nujoma YALINITISHA KWELI KWELI.

  Sikuona umaana wa yeye KUWAPONDA HADHARANI wachungaji wenzie wanao 'display' akaunti za mabenki mbalimbali kwa ajili ya kuomba mchango wa uendeshaji wa vipindi KWA SABABU TU YEYE HAFANYI HIVYO.Inawezekana mchungaji huyu ana uwezo mkubwa sana kifedha kiasi cha kuzilipia hizo gharama,au pengine ANA WAFADHILI...!lakini pamoja na hayo yoote hakukuwa na maana ya KUWAPONDA WENZIE HADHARANI NA KATIKATI YA MAHUBIRI

  Sikuona umaana wa mchungaji huyu 'nguli' KUWAPONDA HADHARANI mama zetu wanaokwenda salon kuzitengenezanywele zao kwa kigezo eti WANAMSAHIHISHA MUNGU.Inawezekana wanakosea,lakini kibinaadamu jamani HAIPENDEZI.Kwa imani yangu ndogo sana mi naamini mbinguni hatuendi kwa kujionyesha ni mafukara sana,NI WALE WENYE MOYO SAFI WOTE.

  Sikuona umaaaaana wa mchungaji huyu mkongwe kabisa kwenye maswala ya dini kutumia muda wake mwingi KUMSAGA KWELI KWELI mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili aliyepata tuzo za kili-musics awards,kwamba hizo tuzo ni feki na kwanini anajiita MALKIA WA INJILI.inawezekana huyu mwimbaji ni mkosaji sana KWA MACHO YA KIBINADAMU,lakini jamii imemkubali,na kwa upeo wangu mdogo naona kama amekuwa chachu kubwa kabisa katika kuitengeneza ONESELF AWARENESS katika imani za watu wengi

  MTIZAMO WANGU SASA:Ninachokiona hapa wachungaji wa namna hii wanawapotezea waumini wao mwelekeo.Wamesahau kwamba uchungaji SIO MAJUNGU,NI KUMUHUBIRI KRISTO.Wanapandikiza majungu na chuki kwa waamini wao.

  Mchungaji huyu ameleta haduthi ya MWAMBA NGOMA....................!anajaribu kuwateka kondoo wake wasitafute malisho sehemu yoyote,au pengine kuwakaribisha kondoo wengine.NAONA KAMA ANALETA POLITICS KWENYE IMANI JAMANI!

  tunaenda wapi?
   
 2. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Huyu si mwingine ni Kakobe,Huna sababu ya kumficha kwani jamii inamwelewa jinsi asivyofungamana na wacha Mungu wengine.Hatumshangai kuyatoa hayo kwani mtu huyu huyu alisimama pale Jangwani 2000 na kumnadi mgombea mmoja kutuambia ndiye chaguo la Mungu kwa Watanzania? Hata kura zilipohesabiwa hatukumwona akiongoza Tanzania.
  Ni huyu huyu anajiita Askofu Mkuu akijua fika hana hata elimu ya theolojia moyoni mwake.Ni huyu huyu Kakobe anayeachanisha na kuvunja ndoa zilizofungwa kisheria na kuziita siyo ndoa takatifu.Basi tusimwaangalie kama kiongozi wa watu bali kiongozi tuu wa dhehebu lake lenye ushawishi wa kuwapata waumini wake kwa kuwaponda wahubiri wengine.
  Mchungaji wa kweli habagui wala haangalii nani kavaa nini na wapi ,Bali huwaangalia kondoo wa Mungu kiroho zaidi kuliko mwili upitao.
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  - KAKOBE ni Mjasiriamali: Kaanza kuuza kanda za muziki mitaa ya Temeke hadi U-Askofu mitaa ya Mwenge. Yeye amekaa kibiashara zaidi ila anatumia mgongo wa DINI. Waumini wake wanakuwa "brain-washed" na ndivyo anavyovuna pesa kutoka kwao - haitaji kuonyesha akaunti ya benki
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Brain Washing mbaya ndugu zangu!

  sasa akina mama mmesikia? Sii ruksa tena kusuka nywele..ni kuingilia uumbaji wa Mungu!

  Vipi yeye mbona anavyaa suti safi na tai???
   
  Last edited: Feb 23, 2009
 5. H

  Hidayante Member

  #5
  Feb 23, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 13
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  Mi naona na kucha tusikate, maana tutakuwa tunaingilia uumbaji wa Mungu. Au vipi Wakuu? Kwi kwi kwi!
   
 6. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Bunge watunge sheria inayovitaka vikundi vya kidini visivyolipa kodi vionyeshe hadharani mapato na matumizi yao.
   
Loading...